Ujinga mwingine ambao kina dada mnafanya ni zaidi ya ujinga! Acheni kabisa!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,595
36,015
Hii tabia ambayo inafanywa na hawa dada zetu huwa inatukera sisi wanaume. Wapo wanaume baadhi wanaougulia moyoni kwa kuogopa kuonekana ni wa aina fulani.

Ni hii tabia ya kuhamishia matatizo ya mashoga zao ama mashost zao kwa wapenzi wao! Utakuta mpenzi wako pale ambapo shost wake amepatwa na janga anakuja mbiombio kupiga mizinga kwa mwanaume wake huku akitoa kila aina ya kilio! Hali hiyo inamfanya jamaa kuwa bize kushughulika na mizinga tu! Mara kwako mara kwa mashost yani daily wewe ni kukamua tu! Acheni hizo!

Nasema hivyo kutokana na kupokea malalamiko na sasa imekithiri sana! Majamaa yanakufa tu na tai shingoni kwa kuogopa kuonekana wabahili au wachovu!

Mfano juzi kuna dada mmoja kaibiwa shilingi laki sita kwenye biashara yake basi shost wake akampa huo msala jamaa wake huku akitoa blah blah kibao! Basi jamaa kuona soo akajipiga kisela akatoa laki nne kumpooza huyo dada! Dah baada ya hapo mshikaji akabaki kulalama tu kwani ndani ya mwezi huu katoa gharama kibao kwa mpenzi wake, bado haitoshi analeta na shost! Hivi huwa mnawaza kuwa tunatoa jasho la damu kuipata shilingi? Emb acheni ujinga maana inakera sana! Jamaa atakuwa anacheka na wewe ila nyuma ya pazia anakuona zaidi ya rumbesa! Unachosha hadi kero! Usichukulie kupendwa ukawa unafanya majaribio ooohooo! Washikaji zenu hawapendezwi kabisa kabisa msione wanacheka na nyie mkachukulia poa! Huku mitaani wanawasema sana na ndo maana dada utakuta ukikatiza hamna mtu mwenye muda na wewe! Walishasikia story zako kutoka kwa mwenza au wenza na wana details zote kuhusu wewe hivyo wanakukwepa!

Futeni kabisa huo ujinga kwenye akili zenu ili mkombolewe!!
 
Huyo jamaa yako aliyetoa hiyo laki nne ndo mpumbavu.Ninachojua haya yanawatokea wanaume wanaojifanya wanazo kwa madem wao.Ukiishi katika reality haya hayatakupata.Ngoja muendelee kuumia kwa kuwa mu wapuuzi
 
Huenda huyu mwenye mkasa akawa ni wewe,kwani mnawaogopa nini kuwaambia mpaka mje kulalama? Si muwaambie hukohuko? Kama mwanamke akishaujua msimamo wako sidhani kama atakuwa haeleweki. Nyie wenyewe mnayumba na kutaka kuonekana mna hela at the same time huyo jamaa angeombwa na wanafamilia angempa kalenda. Badilikeni na wao watabadilika. Untill then acheni kulalamikia kina mama because wanaume wamekua wapiga mizinga wakubwa in this era!
 
Wewe mwenyewe acha hizo, kuleta malalamiko ya majamaa zako jf
 
Naona kuna mwamko mkubwa sana wa kuleta post zinazowalaumu kina dada kunani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom