Ujinga Mtupu! Kwa nini Ukusanye Kodi Kwao!

1954tanu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,041
1,250
Mfumo wa vyama vingi umekuja na kuibua mambo mengi.Mfumo huu umewaibua wajinga wengi na pia umetumiwa kuwafanya wengi kuwa wajinga.Miongoni mwa dalili za ujinga huo ni kauli kama hizi:(i). Toka chama chao kiundwe je kimewaletea maendeleo gani? Hawaja wajengea hata daraja moja.(ii). Daraja tujenge sisi,,halafu wao wanadai wamewaletea maendeleo.(iii).Mkichagua upinzani basi msahau maendeleo.Kawaida serikali hukusanya kodi toka kwa wananchi wote bila kujali kama wananchi hao walikichagua chama chenye kuunda serikali au la.Kodi ni kwa maendeleo ya wote. Kauli kama hizi " ...daraja tujenge sisi halafu wao wadai wameleta maendeleo..." ni za kipuuzi.Hao waliojengewa daraja ni walipa kodi.Matumizi ya kodi yao ni pamoja na kujengewa miundo mbinu,huduma za shule,hospitali nk.Watz wa leo sio wale wa mwaka 47.Chama chenye kuunda serikali hupaswa kuisimamia serikali yake itumikie wananchi. chama kinacho ungana na serikali kuwaibia wananchi wake kwa kubariki uzandiki wa serikali yake hakiwezi kuwa na mvuto kwa umma.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom