Ujinga mkuu WA CUF au huu kidogo wa NCCR usiwadanganye CHADEMA kujiona wana akili, ACT wamejiongeza

Pro Magufuli Wa 47

Senior Member
Mar 5, 2016
188
58
Hapo zaman za kale Kulikuwa na CUF, NCCR, CHADEMA.
Mmoja uroho wa kula posho za chama ulikifanya chama kikapotea dira pamoja ya Kwamba kilikuwa chama chenye nguvu.
Ukitaka kujua "Njaa mbaya sana" waulize NCCR.
Mwingine alijijenga vibaya na hivyo kukifanya chama kionekane ni cha watu fulan tu licha ya kuwa na policy nzuri na zinazotakiwa Tanzania ya leo. Pengine kujikita zaidi kule kwenye koloni letu kumewaghalimu.
Nawakumbusheni tu, CUF Usawa unataka Usawa.
Lakini kulikuwa na hawa wajanja wa CUF na NCCR, yaani CDM.
Yaani hawa jamaa wameweza kuwaficha kabisa wenzao kuanzia kwenye harakati za uchaguzi 2015 na hadi siasa endelevu zinazoendelea sasa.
Kwa uroho wa madaraka na Njaa ya baadhi ya viongozi wa CUF na NCCR, CDM wameweza kufanya maamuzi ambayo yamekuwa yakiwaumiza CUF/NCCR na kujijenga zaidi wao kama wao.
Wengi wanajutia sana walichofanya na walichofanyiwa ila wanaendelea kurudia makosa yaleyale.
CUF imechangia pakubwa ukawa kushinda DSM, lakini kwanini awajapewa Umeya angalau manispaa moja?
CUF wameshinda au wangeshinda Zanzibar, kupokea maelekezo ya kususia uchaguz toka kwa makada wa CDM kumewafanya CUF kuwa wanyonge na kuna hatari ya kutoweka kule visiwani.
Ndoa yao batili, imewafanya wapoteze baadhi ya Viongozi makini, Wenye maono na muhimu, mfano Prof Lipumba ambaye alihoji nafasi ya CUF ndani ya UKAWA na kuonekana msaliti.
Na kibaya zaidi ni wao kukosa majimbo ambayo ushindi ulikuwa wazi kisa tu, usaliti wa CHD. Mtatilo analijua hili.
NCCR wamekosa baadhi ya majimbo kwa sababu ya CDM kusimamisha wagombea pia kinyume na makubadiliano.
NCCR wamepoteza wanachama na viongozi wao makini, kisa kiu ya Mbatia kuwa waziri mambo ya Nje under Ukawa.
Cha ajabu mnaendelea kutumika na CHADEMA kisiasa Bungeni na kila pahala!
Shtukeni mnaibiwa geukeni na msawazishe mlipokosea, CDM ni baba wa vigeugeu, Mama wa wanafiki, kaka wa Ubinafsi na ni Dada wa wasiojielewa.
Hongereni ACT kwa kusimamia mnachoamini na kwa kutanguliza maslah yenu kila mnapojaribu kuungana na hao Vigeugeu.
Najua mnafanya hivi kwa sababu ya kuijua vyema CHDM na wizi wa kisiasa wanaoufanya.
 
Back
Top Bottom