UJINGA: "Ajiona samaki kwasababu amezungukwa na maji?"

FrediusSnowden

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
269
224
Habari za leo wakuu.. Naomba tufikirishane masuala..

Ni hii leo pale Mbeya, ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Rungwe, Mbeya kimemfuta uanachama na kumvua udiwani wake wa Kata ya Kambasegela, Kiswigo Mwakalebela kwa kile ambacho kinadaiwa ni kukiuka taratibu na kanuni za CHADEMA.

Ajabu ni jamaa mwenyewe Bw. Mwakalebela mwenyewe kusema kuwa amejivua uanachama na kuhamia CCM na kusema anashindwa kufanya kazi kwa kuwa "amezungukwa na viongozi wengi wa CCM". Hapa ndipo kichwa cha habari cha mada yangu inapo anzia. Ukiwa kama binadamu inawezekana vipi kujiita samaki eti kwasababu umezungukwa na maji.?

Ukweli ni kwamba toka mwanzo kabisa, intelijensia ya CHADEMA ilifuatia mwenendo wa Mwakalebela na kubaini kuwa amekuwa akiivunja katiba ya chama, ikiwemo kuwa "double standard" hivyo hawawezi kuvumilika.
IMG_20180808_131752.jpg
 
Tunaingia kwenye gharama za uchaguzi kwa sababu ya kukosekana umakini ndani ya chama katika kuteua wagombea wake!
 
Enzi ngumu sana hizi kwa wanasiasa. Wakati mwingine tuwahurumie tu.

Kosa ni kufikiria watatutatulia matatizo yetu kama taifa. Tunasahau siasa kwao ni ajira.
 
Back
Top Bottom