Nataman huyu corona angekuwa anawapata wenye ngozi nyeupe tu,sisi wenye ngozi nguvu tuliyo nayo yanatutosha
WE JAMAA ACHA KUNICHEKESHA USIKU HUUHaya ndo madhara ya uroho na ulafi Ya kula wadudu na Viumbe wa Ajabu..
Inasemekana Chanzo cha huu Ugonjwa ni Supu ya Popo
hivi mbona hata wapemba wanakula popo imekaaje hii na corona mkuu?Haya ndo madhara ya uroho na ulafi Ya kula wadudu na Viumbe wa Ajabu..
Inasemekana Chanzo cha huu Ugonjwa ni Supu ya Popo
Mgonjwa wa kwanza wa maradhi yanayosababishwa na virusi vya Corona amethibitishwa nchini Ujerumani. Msemaji wa wizara ya afya mjini Munich, amesema jana jioni kwamba mgonjwa huyo ni mwanaume anayetokea eneo la Stanberg, katika jimbo la Bavaria, kiasi kilomita 30 kusini magharibi mwa Munich.
Jamaa wa karibu na mgonjwa huyo wameelezewa kuhusu dalili za maradhi hayo, hatua za usafi na namna virusi hivyo vinavyosambaa.
Kirusi hicho kipya aina ya Corona kimetokea katika mji wa Wuhan nchini China hadi sasa kimesababisha vifo vya takriban watu 106. Tume ya afya katika jimbo la Hubei ambako ni kitovu vya maradhi hayo imesema watu wengine 24 wamekufa na 1,291 wameambukizwa, idadi inayofanya jumla ya watu walioambukizwa hadi sasa kufikia 4,000 kote nchini humo.
Visa vingine vya Corona vimeripotiwa Korea Kusini, Taiwan, Thailand, Nepal, Vietnam, Saudi Arabia, Singapore, Marekani, Ufaransa na Australia.
Chanzo: DW
==========
Mkurugenzi wa Idara ya Afya wa jiji la Beijing, China amesema wanatumia dawa za wagonjwa wa VVU na UKIMWI za Lopinavir na Ritonavir kusaidia wagonjwa wa homa iliyozuka ya #Coronavirus
Mpaka sasa hakuna tiba ya ugonjwa huo huku Marekani ikisema iko maabara kutengeneza chanjo yake
Hadi sasa watu 106 wamepoteza maisha kutokana na virusi vya Corona huku zaidi ya watu 4000 wameambukizwa