Ujerumani yathibitisha mgonjwa wa kwanza wa Corona. Dawa za UKIMWI kuanza kutumika kwa wagonjwa wa Corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Mgonjwa wa kwanza wa maradhi yanayosababishwa na virusi vya Corona amethibitishwa nchini Ujerumani. Msemaji wa wizara ya afya mjini Munich, amesema jana jioni kwamba mgonjwa huyo ni mwanaume anayetokea eneo la Stanberg, katika jimbo la Bavaria, kiasi kilomita 30 kusini magharibi mwa Munich.

Jamaa wa karibu na mgonjwa huyo wameelezewa kuhusu dalili za maradhi hayo, hatua za usafi na namna virusi hivyo vinavyosambaa.

Kirusi hicho kipya aina ya Corona kimetokea katika mji wa Wuhan nchini China hadi sasa kimesababisha vifo vya takriban watu 106. Tume ya afya katika jimbo la Hubei ambako ni kitovu vya maradhi hayo imesema watu wengine 24 wamekufa na 1,291 wameambukizwa, idadi inayofanya jumla ya watu walioambukizwa hadi sasa kufikia 4,000 kote nchini humo.

Visa vingine vya Corona vimeripotiwa Korea Kusini, Taiwan, Thailand, Nepal, Vietnam, Saudi Arabia, Singapore, Marekani, Ufaransa na Australia.

Chanzo: DW


==========

Mkurugenzi wa Idara ya Afya wa jiji la Beijing, China amesema wanatumia dawa za wagonjwa wa VVU na UKIMWI za Lopinavir na Ritonavir kusaidia wagonjwa wa homa iliyozuka ya #Coronavirus

Mpaka sasa hakuna tiba ya ugonjwa huo huku Marekani ikisema iko maabara kutengeneza chanjo yake

Hadi sasa watu 106 wamepoteza maisha kutokana na virusi vya Corona huku zaidi ya watu 4000 wameambukizwa
 
... taarifa ya habari jana, waziri wa kilimo Kenya anasema wameishiwa dawa ya kupambana na nzige na ni very expensive. Hata hao nzige kupambana nao lazima mrudi kwao kuomba misaada.

Dawa ya nzige ni kuwala tu, na waje huku kwetu watajuta.
 
Back
Top Bottom