Ujerumani yasisitiza Ulaya kuitenga marekani katika mfumo wa kifedha

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,990
17,879
Kwa mara nyingine Ujerumani yaihimiza Ulaya kuitenga Marekani katika mfumo wa fedha
Kwa mara nyingine tena, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumiani amezihimiza nchi za Ulaya kutafuta njia za kuwa na mfumo wao wa kujitegemea wa kifedha kama njia ya kudumisha mapatano ya nyuklia na Iran yanayojulikana kwa kifupi kama JCPOA.
Haiko Maas amesema hayo katika mazungumzo yake na mawaziri wenzake wa Ulaya mjini Vienna Uswisi na kuongeza kuwa, kuna wajibu wa kuzungumzia njia za kuwa na mfumo huru wa kifedha wa Ulaya kwani kama hazitofanya hivyo, Wachina wataanzisha mfumo huo na hilo litakuwa ni kwa madhara ya nchi za Ulaya.
Kabla ya hapo pia, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani aliashiria ulazima wa kulindwa na kuhifadhiwa mapatano ya nyuklia na Iran akisisitiza kuwa moja ya njia za kuyalinda mapatano hayo ni kuiweka pembeni Marekani na kuanzia mfumo wa malipo ya fedha wa Ulaya unaofanana na ule wa SWIFT bila ya kuishirikisha hata kidogo Marekani.
Itakumbukwa kuwa tarehe 8 Mei mwaka huu, serikali ya Donald Trump ilitangaza kuitoa Marekani katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA licha ya hatua hiyo kupingwa vikali na nchi za Ulaya pamoja na China na Russia ambazo ni sehemu ya kundi la 5+1 lililofikia mapatano hayo ya nyuklia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Tehran imezitaka nchi za Ulaya kuchukua hatua za kivitendo za kuyalinda mapatano hayo vinginevyo hayataweza kudumu kwa maneno matupu.
Ukitoa Marekani, pande nyingine zote zilizofanikisha mapatano ya JCPOA zimesema zitahakikisha mapatano hayo yanalindwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marekani amecheza karata yake kwa umakini wa hali ya juu!!!

Mataifa ya ulaya yalijisahau sana kwa Marekani na wameshachelewa sana!!!!....

All you need is power then the rest are yours!!!!......

Kwa mfumo wa fedha na kiuchumi ulivyo kidunia ni dhahiri huwezi kumweka kando Marekani kwa namna yoyote ile!!!!!

Kama ingekuwa rahisi China angeshafanya hivyo kipindi kirefu sana....lakini anajua ni kiasi gani itaigharimu nchi yake kiuchumi kufanya hivyo na mchina hataki kurudi kule alikokuwa mwanzo
 
Back
Top Bottom