Ujerumani: Tunaionya Marekani, iache kutupangia nishati ya kutumia

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,320
Ujerumani imesema inaionya Marekani iache kuwapangia nishati ya kutumia kwani kila nchi ina uhuru wa kuamua itumie nishati gani.

Ujerumani inashirikiana na Urusi kujenga bomba la gesi, Nord 2 kutoka Urusi hadi Ujerumani lakini Marekani ametishia kuliwekea vikwazo hilo bomba lisikamilie au likose vifaa ama fedha ili lisikamilike.

Ujerumani inategemea gesi nyingi na ya bei nafuu kutoka Urusi ila Marekani anatishia kukwamisha huo mradi kwa kuuwekea vikwazo vya kifedha na kiutaalamu ili ufe. Ujerumani anasema Marekani akifanya hivyo ni kuwapangia ama kutaka kuwapangia nishati gani watumie.

Germany warns US against imposing sanctions on Nord Stream 2, says no country has right to ‘dictate’ its energy policy
 
Hao jamaa saizi hawajiamini, wanahisi watapoteza ushawishi wa dunia hasa katika nyanja za Tecnolojia na Biashara.

Anapambana sana kuhakikisha Urusi na Mchina hawatoboi.

Angalia anavyouwa Tik tok kwa nguvu zake zote, kwakuwa ni tishio kwa akina Instagram. Anapambana kuiuwa HUAWEI baada ya kuiua ZTE iwaiuwa ni tishio la Akina Apple na Telecommunication industry

Mchina ananawiri, jamaa anapigana kibabe sasa
 
Hata nchi za Ulaya zilivunja makubaliano yao ya kibiashara na Iran,si kwa kupenda wenyewe bali msukumo kutoka US naona Germany kamchoka liwalo na liwe.
 
Duuu USA ni mbabe hatari
Huu ubabe utamponza maana watamchoka sidhani kama hivyo vikwazo atakavyoiwekea Ujerumani Umoja wa ulaya watakubariana navyo. Na akiendelea huenda wakaamua kuungana na MChina maana mwenzako akinyolewa zako tia maji.
Haiwezekani yeye kila anachoamua ndicho kiwe sawa huyu Trump huenda ametengeneza Uchumi wa USA ila ataiangusha litakapokuja swala la diplomasia na political influence maana sasa anaaza kuvuka mipaka kila mtu anataka mlima vikwazo
 
Mpaka ujerumani wamesema hivyo ni wazi wameshaichoka USA ... Miaka sio mingi USA itafikwa na anguko kubwa sana

Ujerumani ni Moja ya nchi ambazo zinauchumi mkubwa sana duniani ipo katika zile top 5 country zenye ukwasi na ushawishi mkubwa wa kisiasa ..ni rahisi kwa taifa kubwa kama la ujerumani kuleta ushawishi wa kisiasa kwa mataifa mengine ambayo yana chukizwa na mienendo ya kimabavu ya USA na kuamua kuliangusha taifa hilo ..... Usa Wanapaswa kuwa makini sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom