Ujerumani kuzipiga faini facebook,twitter na google kama hadi Januari hawatafuta habari za kichochez

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,745
2,000
Serikali ya Ujerumani ikiongozwa na waziri wa Sheria Heiko Maas inatarajia kuwawekea vikwazo ikiwepo FAINI makampuni makubwa ya Mitandaoni Facebook na GOOGLE kama hawatafuta Hotuba za Chuki kwenye mitandao yao .

Tayari kikosi maalumu cha FACEBOOK,TWITTER na GOOGLE kilikaa mwaka jana kushughulikia tatizo hilo lakn report ya serikali hadi hivi majuzi imeonyesha bado Taarifa hizo nyingi hazijachukuliwa.

Tayari kwa Upande wa Facebook Hivi juzi wamezindua SOFTWARE maalum ya kugundua Taarifa Feki katika mtandao wake kabla haijarushwa.

Kuna kitu cha kujifunza;
Soma habari nzima hapa chini

Germany to force Facebook, Google and Twitter to act on hate speech
 
Mwelewa

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,356
2,000
Hii maana yake nini? Kwamba tuone serikali ya Magu ipo sawa kuishurutisha JF? Kwamba kushikiliwa kwa Max ni sawa tu? Kwamba serikali inania njema sana?

Kama lengo kuleta habari hii ni kuonyesha mlinganisho ili serikali ya Magu ionekane inachapa kazi mimi nasema jibu ni HAPANA. Fungua macho utazame mambo kwa hekima......suala la sheria ya mitandao Tanzania lengo lake ni KULINDA DOLA TU. Logically utaona haina maana utasema sheria imetungwa na bunge hainabudi itekelezwe.....lakini ukitazama uhalisia sheria hii ya mitandao niyakikandamizi tu.....italinda dola mwananchi masikini wala hatoona faida yoyote zaidi yakuwavunja moyo wajasiriamali kama Max.

#freemaxencemelo#
 
MOTOCHINI

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
25,817
2,000
Ujerumani wakifanya wale Vibendera powaaaa
Tanzania ikifanya full kutapika viroba hovyo!!!

Ustaarabu muhimu ktk taifa

Maneno ya chuki,Uchochezi,Uzushi ndio msingi wa malalamiko haya yote.
Hata ikitokea miujiza ya mungu cdm itawale(ndoto) haita unga mkono uchochezi ndani ya mitandao,

Tuitumie Mitandao vizuri na kuheshimu Mamlaka
 
LebronWade

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,615
2,000
Serikali ya Ujerumani ikiongozwa na waziri wa Sheria Heiko Maas inatarajia kuwawekea vikwazo ikiwepo FAINI makampuni makubwa ya Mitandaoni Facebook na GOOGLE kama hawatafuta Hotuba za Chuki kwenye mitandao yao.

Serikali hiyo imewapa hadi masaa 24 yajayo wasipofuta habari hizo za chuki watapigwa fine isiyopunga TSH 1 Billion. Tayari kikosi maalumu cha FACEBOOK,TWITTER na GOOGLE kilikaa mwaka jana kushughulikia tatizo hilo lakn report ya serikali hadi hivi majuzi imeonyesha bado Taarifa hizo nyingi hazijachukuliwa.
Tayari kwa Upande wa Facebook Hivi juzi wamezindua SOFTWARE maalum ya kugundua Taarifa Feki katika mtandao wake kabla haijarushwa.

Kuna kitu cha kujifunza;
Soma habari nzima hapa chini

Germany to force Facebook, Google and Twitter to act on hate speech
Ndio upuuzi wa "Fake News" traditional media zimeamua kupiga propaganda....

Yaani huu ujinga ni wa ajabu kabisa...

CNN akitoa habari hiyo hiyo sio Fake News akitoa Alex Jones wa Infowars ni Fake News...Makampuni makubwa ndio yana mandate ya kuamua hii ni Fake News na hii si Fake News wakati huo huo na wao ni watoa news kama wengine...

Ujerumani wanasema hate speech,wana kipimio kipi cha kujua ni hate speech?

Hizi propaganda ndio Dems walikua wanazitumia na traditional media such as CNN,MSNBC,etc...na Trump kaingia,hafagilii wanene...simple Youtube Channels ndio zilimpigia kampeni Trump na akashinda,haya ma media houses makubwa yanaita ni hate speech au fake news na Ujerumani kavamia,we will see watafika wapi na claims za uongo hizo just to shut down small independent online news companies
 
MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,745
2,000
Hii maana yake nini? Kwamba tuone serikali ya Magu ipo sawa kuishurutisha JF? Kwamba kushikiliwa kwa Max ni sawa tu? Kwamba serikali inania njema sana?

Kama lengo kuleta habari hii ni kuonyesha mlinganisho ili serikali ya Magu ionekane inachapa kazi mimi nasema jibu ni HAPANA. Fungua macho utazame mambo kwa hekima......suala la sheria ya mitandao Tanzania lengo lake ni KULINDA DOLA TU. Logically utaona haina maana utasema sheria imetungwa na bunge hainabudi itekelezwe.....lakini ukitazama uhalisia sheria hii ya mitandao niyakikandamizi tu.....italinda dola mwananchi masikini wala hatoona faida yoyote zaidi yakuwavunja moyo wajasiriamali kama Max.

#freemaxencemelo#
mkuu hakuna anayeunga mkono vile anavyofanyiwa Max, hili liko wazi lakini pia ni ajabu kama tukishabikia matusi na vitu vusivyofaa kwa jina la uhuru wa kuongea. Tunanafasi ya kujirekebisha na kujitafakari kama kweli na sisi kuna sehemu tunaenda nje ya mstari. Lengo la Jukwaa ni kuonyesha nini kinaendelea huko duniani. Tafsiri yake inabaki kuwa maoni ya msomaji. Kila mwana JF anahuzunika kwa Kukamatwa kwa MAX. Nilidhani tungejadili kwa unbiased mind, hii ni habari kama habari nyingine tu. Fungua link soma. Mfano Ujerumani hawajamtia ndani MArk Zugerberg au kuwaagiza US wamkamate bali wanampa nafasi ya kuboresha mtandao wake kitu ambacho huku hatukioni
 
mahutu

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
766
1,000

Kwa hiyo unashauri tuendelee kuripoti uongo...na kutoka matamshi yasiyo na hekima...na kuwakejeri viongozi....si ndo unamaanisha hvo....
 
Lancanshire

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
14,019
2,000
Counterattack kwa JF siyo?
Free maxiencemelo

Hata magazeti ya huko ujerumaini wamesema max na Uhuru wa habari kwa ujumla upo kwenye hatari Tanzania
 
Mwelewa

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,356
2,000
Kwa hiyo unashauri tuendelee kuripoti uongo...na kutoka matamshi yasiyo na hekima...na kuwakejeri viongozi....si ndo unamaanisha hvo....
Watu kuzungumza kwa uwazi ndiyo uwongo?

Hapa JF tunaruhusiwa kutoa habari kama "tetesi" na kama habari ikithibitika uwongo modertors wanaiondoa mara moja. Huu ndiyo umekuwa utamaduni wetu hapa JF. Acha kushikiwa mawazo na system ndugu. Mbona mnaogopa sana kukosolewa? Kama huna ngozi ngumu usiwe kiongozi........hii nchi inawatu milioni 50 lazima tukosoe tu hatuwezi kaa kimya
 
Lupyeee

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
2,685
2,000
Hamna anayehangaika na mafisadi chadema kwa sasa.

Hasa hiki kitendo Cha Mbowe kwenda ulaya kutoa hotuba za kuichafua nchi kimewaudhi sana watanzania.

2020 chadema wajiandae kupungua bungeni.
 
Mwelewa

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,356
2,000
mkuu hakuna anayeunga mkono vile anavyofanyiwa Max, hili liko wazi lakini pia ni ajabu kama tukishabikia matusi na vitu vusivyofaa kwa jina la uhuru wa kuongea. Tunanafasi ya kujirekebisha na kujitafakari kama kweli na sisi kuna sehemu tunaenda nje ya mstari. Lengo la Jukwaa ni kuonyesha nini kinaendelea huko duniani. Tafsiri yake inabaki kuwa maoni ya msomaji. Kila mwana JF anahuzunika kwa Kukamatwa kwa MAX. Nilidhani tungejadili kwa unbiased mind, hii ni habari kama habari nyingine tu. Fungua link soma. Mfano Ujerumani hawajamtia ndani MArk Zugerberg au kuwaagiza US wamkamate bali wanampa nafasi ya kuboresha mtandao wake kitu ambacho huku hatukioni
Sawa........lakini kwa Max si umeona wamemkamata, wamemlaza ndani siku tatu, hawa lengo lao si jema.
 
Marlex Jr El

JF-Expert Member
Nov 6, 2015
1,785
2,000
Mlengo wa ujerumani ni tofauti kabisa na wa hapa kwetu... Tukubali tukatae tulikosea kuchagua kwahy tusialalishe kilichokwisha chacha.
 
Polycarp Isaya Urio

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
2,008
2,000
Hii maana yake nini? Kwamba tuone serikali ya Magu ipo sawa kuishurutisha JF? Kwamba kushikiliwa kwa Max ni sawa tu? Kwamba serikali inania njema sana?

Kama lengo kuleta habari hii ni kuonyesha mlinganisho ili serikali ya Magu ionekane inachapa kazi mimi nasema jibu ni HAPANA. Fungua macho utazame mambo kwa hekima......suala la sheria ya mitandao Tanzania lengo lake ni KULINDA DOLA TU. Logically utaona haina maana utasema sheria imetungwa na bunge hainabudi itekelezwe.....lakini ukitazama uhalisia sheria hii ya mitandao niyakikandamizi tu.....italinda dola mwananchi masikini wala hatoona faida yoyote zaidi yakuwavunja moyo wajasiriamali kama Max.

#freemaxencemelo#
Usipotoshe watu comrade.Swala tayari lipo mahakamani.
 
Mwelewa

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,356
2,000
Usipotoshe watu comrade.Swala tayari lipo mahakamani.
Wapi nimepotosha? Wapi nimesema suala halipo mahakamani? Wewe unaona hii issue ya Max polisi wame handle vizuri? Unafahamu usumbufu anaopata kukaa sero siku tatu? Wewe umetoka kula ugali kwa raha zako Max yupo behind bars anawaza mashtaka ambayo unaona tu wazi ni politically motivated
 
Polycarp Isaya Urio

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
2,008
2,000
Wapi nimepotosha? Wapi nimesema suala halipo mahakamani? Wewe unaona hii issue ya Max polisi wame handle vizuri? Unafahamu usumbufu anaopata kukaa sero siku tatu? Wewe umetoka kula ugali kwa raha zako Max yupo behind bars anawaza mashtaka ambayo unaona tu wazi ni politically motivated
Acha sheria ichukue Mkondo wake,Kesi ilianzia Polisi wakakamata,wakapeleleza,wakampelekea jalada Wakili wa Serikali akalisoma akaona Kuna ushahidi,akaanda hati ya mashitaka na kesi ikaenda mahakamani na jamaa kakosa dhamana ya Mahakama, wewe hapo umewaona Polisi tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom