#COVID19 Ujerumani inatafakari kuondoa upimaji COVID-19 wa bure

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Mswada wa pendekezo umefichua mpango wa majimbo 16 ya Ujermani na wa serikali kuu juu ya kuacha kuwapima watu maambukizi ya virusi vya corona bila ya kulipia.

Wabunge wa Ujerumani wanatarajiwa kuupitisha mpango huo mwezi wa Oktoba. Kwa mujibu wa taarifa pendekezo hilo limetoka kwenye ofisi ya kansela na litajadiliwa leo na mawaziri wakuu wa majimbo yote 16 ya Ujerumani.

Pendekezo hilo limetokana na kauli zilizotolewa pia na waziri wa afya wa Ujerumani Jens Spahn aliesema kwamba watu waliokataa chanjo watapaswa kujilipia wenyewe endapo watataka kupimwa maambukizi ya virusi vya corona.

Amesema madhali wananchi wote wa Ujerumani wamepewa fursa ya kupata chanjo si lazima kwa serikali sasa kuwalipia watu wanaotaka kupimwa maambukizi ya virusi.
 
Hivi we ni roboti au mtu?
 
Back
Top Bottom