Ujerumani imepata Tanzania msaada wa Euro milioni 71, sawa na takriban Sh190.5 bilioni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Ujerumani imeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 71, sawa na takribani Sh190.5 bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi kadhaa ikiwemo maji, uendelezaji wa maliasili na utalii, afya ya mama na mtoto pamoja na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Fedha na Mipango Oktoba 26 2021 nyaraka za makubaliano ya msaada huo zimetiwa saini kati ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayesimamia masuala ya Fedha za Nje Amina Khamis Shaaban na Kiongozi wa ujumbe wa Serikali ya Ujerumani Marcus Von Essen.

Akizungumza baada ya kutiwa saini kwa nyaraka hizo, Naibu Katibu Mkuu Amina Khamis Shaaban aliyataja maeneo yatakayonufaika na msaada huo kuwa ni afya ya mama na mtoto iliyotengewa Euro milioni 24 na mradi wa kuzuia migogoro baina ya wanyamapori na binadamu, utakao tumia Euro milioni 6.

“Maeneo mengine yatakayonufaika na fedha hizi ni mpango wa kufidia upotevu wa makusanyo ya maduhuli katika sekta ya utalii kutokana na upungufu wa watalii walioingia nchini kwa sababu ya ugonjwa wa Uviko -19,”amesema.

Ameyataja maeneo yatakayonufaika kuwa ni kuzuia ujangili, kuboresha miundombinu kwenye makazi na jamii inayozunguka maeneo ya Hifadhi za Taifa, utakaogharimu Euro milioni 15.

Alisema kuwa Euro milioni 20 zitaelekezwa kuboresha huduma ya maji kwenye miji inayokua na kiasi kingine cha Euro milioni 3 kitatumika kuboresha usalama wa maji kwenye maeneo ya baadhi ya miji nchini.

Amina amesema kuwa kiasi kingine cha Euro milioni 3 kitatumika katika masuala ya kulinda haki za akina mama na wasichana wanaokabiliwa na changamoto ya ukatili wa kijinsia kwa kuwapatia msaada wa kisheria.

Balozi wa Ujerumani nchini, Regine Hess na Kiongozi wa Ujumbe wa Ujerumani ulioshiriki majadiliano yaliyofanikisha kupatikana kwa msaada huo Marcus Von Essen, walisema Ujerumani imeamua kufufua ushiriki wake katika kujenga maendeleo ya Tanzania ili kuunga mkono uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.

Walieleza kuwa chini ya makubaliano mapya, Ujerumani yatajikita zaidi kusaidia afya ya mama na mtoto, kusaidia masuala ya bima ya afya kupitia NHIF, maji na usafi wa mazingira, usimamizi wa fedha za umma, kuhifadhi maeneo ya urithi wa dunia kama vile hifadhi ya Selous na kuwalinda wanawake na wasichana dhidi ya vitendo vya kikatili.

Chanzo: Mwananchi
 
190bn sisi za nini sasa. Hii misaada misaada ndio inafanya hawa weupe watudharau sanaa.

Tumeshindwa kubuni mbinu humu ndani kupata hiyo 190bn mpaka weupe watupe msaada?
 
Misaaada teleeeeee lakini bado umasikini ni wa kutisha mno. Kuna umasikini mkubwa nchi hii kuliko tunavyodhani.Ngonjera za wanasiasa wetu na watawala wetu kwamba uchumi unakua,ni ishara ya mwenye shibe asiyejali mwenye njaa.
 
190bn sisi za nini sasa hii misaada misaada ndio inafanya hawa weupe watudharau sanaa..

tumeshindwa kubuni mbinu humu ndani kupata hiyo 190bn mpaka weupe watupe msaada?
OK noted nikuelimisha kidogo Principal za biashara,

Hizo pesa ni Fedha za kigeni Euros, Tukizipata hizo zinatusaidia kuimarisha thamani ya shilingi yetu pia

Hizo pesa za kigeni zinatuwezesha sisi wakinga tusipate Taabu pale tunapoagiza bidhaa toka nje ya Tanzania, Huko nje ya Tanzania hatuagizi bidhaa kwa kutumia pesa ya Tanzania

Kwa hali ya kawaida kiongozi na hii hali ya uviko 19,Ni bidhaa gani sisi Tanzania tuuze nje tuweze pata hizo pesa Ghafla hivyo

Uchumi unatawaliwa na kanuni mbili tu kiongozi yaani nguvu ya uuzaji na ununuaji au Forces of Demand and Supply

The lower the demand of your currency the lower the value of your currency in the market

The lower the demand of Forex in our country the stable the Shilling we have in our economy
 
190bn sisi za nini sasa hii misaada misaada ndio inafanya hawa weupe watudharau sanaa..

tumeshindwa kubuni mbinu humu ndani kupata hiyo 190bn mpaka weupe watupe msaada?...
Tozo ndio u ubunifu walionao
 
190bn sisi za nini sasa.....hii misaada misaada ndio inafanya hawa weupe watudharau sanaa..

tumeshindwa kubuni mbinu humu ndani kupata hiyo 190bn mpaka weupe watupe msaada?...
Tumebuni tozo mmelalamika
 
Ata kama ni wewe unaweza kukata pesa yakupewa. Tuwaache ccm tuu maana walishashindwa mwaka wa 50 hawawezi fanikiwa kwa miaka 5
 
OK noted nikuelimisha kidogo Principal za biashara, Mimi kama Mkinga

Hizo pesa ni Fedha za kigeni Euros, Tukizipata hizo zinatusaidia kuimarisha thamani ya shilingi yetu pia...
Kwanini waombe misaada kwa mabeberu wakati mimi niko mzalendo naweza kutoa kiasi hicho kidogo kama hicho cha euro 71?

Ifikie wakati hii serikali itushirikishe hata sisi mabilonea wazalendo wazawa kwenye ishu ndogo ndogo kama hizi za kutoa misaada isiyozidi euro million 100.
 
190bn sisi za nini sasa.....hii misaada misaada ndio inafanya hawa weupe watudharau sanaa..

tumeshindwa kubuni mbinu humu ndani kupata hiyo 190bn mpaka weupe watupe msaada?...
Waswahili bana.

Tozo hamtaki ma misaada mnachonga.

Hizo mbinu watakazo buni unadhani hizo kodi watalipa MBUZIII
 
Ujerumani imeipatia Tanzania msaada wa Euro milioni 71, sawa na takribani Sh190.5 bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi kadhaa ikiwemo maji, uendelezaji wa maliasili na utalii, afya ya mama na mtoto pamoja na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Fedha na Mipango Oktoba 26 2021 nyaraka za makubaliano ya msaada huo zimetiwa saini kati ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango anayesimamia masuala ya Fedha za Nje Amina Khamis Shaaban na Kiongozi wa ujumbe wa Serikali ya Ujerumani Marcus Von Essen.

Akizungumza baada ya kutiwa saini kwa nyaraka hizo, Naibu Katibu Mkuu Amina Khamis Shaaban aliyataja maeneo yatakayonufaika na msaada huo kuwa ni afya ya mama na mtoto iliyotengewa Euro milioni 24 na mradi wa kuzuia migogoro baina ya wanyamapori na binadamu, utakao tumia Euro milioni 6.

“Maeneo mengine yatakayonufaika na fedha hizi ni mpango wa kufidia upotevu wa makusanyo ya maduhuli katika sekta ya utalii kutokana na upungufu wa watalii walioingia nchini kwa sababu ya ugonjwa wa Uviko -19,”amesema.

Ameyataja maeneo yatakayonufaika kuwa ni kuzuia ujangili, kuboresha miundombinu kwenye makazi na jamii inayozunguka maeneo ya Hifadhi za Taifa, utakaogharimu Euro milioni 15.

Alisema kuwa Euro milioni 20 zitaelekezwa kuboresha huduma ya maji kwenye miji inayokua na kiasi kingine cha Euro milioni 3 kitatumika kuboresha usalama wa maji kwenye maeneo ya baadhi ya miji nchini.

Amina amesema kuwa kiasi kingine cha Euro milioni 3 kitatumika katika masuala ya kulinda haki za akina mama na wasichana wanaokabiliwa na changamoto ya ukatili wa kijinsia kwa kuwapatia msaada wa kisheria.

Balozi wa Ujerumani nchini, Regine Hess na Kiongozi wa Ujumbe wa Ujerumani ulioshiriki majadiliano yaliyofanikisha kupatikana kwa msaada huo Marcus Von Essen, walisema Ujerumani imeamua kufufua ushiriki wake katika kujenga maendeleo ya Tanzania ili kuunga mkono uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita.

Walieleza kuwa chini ya makubaliano mapya, Ujerumani yatajikita zaidi kusaidia afya ya mama na mtoto, kusaidia masuala ya bima ya afya kupitia NHIF, maji na usafi wa mazingira, usimamizi wa fedha za umma, kuhifadhi maeneo ya urithi wa dunia kama vile hifadhi ya Selous na kuwalinda wanawake na wasichana dhidi ya vitendo vya kikatili.

Chanzo: Mwananchi
Mhuuhh! Kasi inaendelea
 
Mahela yote hayo halafu fedha zikifika watu wanabonya tu hakuna usimamizi mzuri wala miradi ya maana siku zote hawa jamaa wanatoa fedha kwa mambo ambayo hayatusaidiii kujikwamua kiuchumi.

Ni katika matumizi ambayo ni ya kawaida kabisa ambapo tukitulia hizo fedha tunazipata wenyewe.
 
Back
Top Bottom