#COVID19 Ujerumani: Bunge lapitisha Sheria mpya kupambana na Maambukizi ya CoronaVirus

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Bunge la Ujerumani limeidhinisha sheria mpya za kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona. Hatua hiyo imechukuliwa leo wakati Kansela Angela Merkel anayekaimu serikali, akijiandaa kukutana na viongozi wakuu wa majimbo 16 ya Ujerumani kujadili hatua zaidi za kukabiliana na janga la virusi hivyo.

Miongoni mwa yaliyopitishwa ni kutorefushwa kwa hali ya janga la kitaifa baada ya kipindi cha hali ya dharura ya kukabiliana na janga hilo kufikia mwisho wake hapo Novemba 25.

Kipindi hicho cha hali ya dharura cha kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani kilianzishwa mwezi March 2020 ambapo miongoni mwa mambo mengine kulikuweko na sheria kali za usafiri. Hata hivyo sheria zilizopitishwa na bunge sasa zitahitaji kuidhinishwa pia na Bundesrat ambalo ni baraza la juu la maamuzi ya mwisho Ujerumani.

Aidha mpango wa kukabiliana na ongezeko la maambukizi unajumuisha sheria ya kuwalazimisha wafanyakazi wa vituo vya kuhudumia wazee pamoja na wageni wanaotembelea vituo hivyo kupima kila siku, haijalishi ikiwa mtu amechanja au hajachanja.

Kadhalika mtu atalazimika kuonesha uthibitisho wa ikiwa amechanjwa, amewahi kuugua Covid na kupona au kupima katika maeneo ya kazi na katika usafiri wa umma. Shule zitaendelea kuwa wazi na pia hakuna vizingiti vya kusafiri au watu kulazimishwa kuchanja.

Lakini sheria kali imewekwa kwa wale watakaofanya udanganyifu wa vyeti vya chanjo ambapo adhabu ya hadi miaka mitano jela imewekwa. Kwa mujibu wa polisi ya Ujerumani suala la watu kughushi vyeti vya chanjo ni kubwa sana nchini Ujerumani ambapo kuna wanaouza vyeti hivyo vya bandia hadi yuro 400.

Nchini Uingereza shirika linalosimamia masuala ya usalama wa afya limesema watoto kati ya umri wa miaka 12 na 15 wanapaswa kucheleweshwa kuchanjwa endapo waliwahi kuugua Covid alau wiki 12 baada ya kuambukizwa.

Uhispania nayo imetangaza kutoa chanjo ya ziada kwa wazee wa kuanzia umri wa miaka 60 na zaidi wakati Uholanzi ikisema inakabiliwa na upungufu wa vifaa vya upimaji virusi vya Corona.
 
Kugushi vyeti vya chanjo kumbe ni mpaka ulaya mi nilifikiri ni bongo Tu
 
Ni mangapi yanafanyika katika maisha ila matokeo yanakuwa kinyume? Ni mangapi yanafanyika katika maisha matokeo yanakuwa positive? Think positively!
Ndio maana nakushangaa unapolazimisha kuwa Magufuli kafa kwa corona na sababu et alikuwa kiBuri, kila mtu lazima uwe kiburi au usiwe kiburi.
 
Back
Top Bottom