Ujenzi wa Uwanja Mpya wasimama

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,082
Ujenzi wa Uwanja Mpya wasimama

2007-11-23 19:18:21
By Somoe Ng'itu

Ujenzi wa Uwanja Mpya wa Taifa umesimama kufuatia wakandarasi wa uwanja huo, kampuni ya Beijing Construction kuidai serikali.

Chanzo kimoja kiliiambia Nipashe kuwa baadhi ya mafundi waliokuwa wanajenga uwanja huo wamerejea kwao China.

Zoezi la ujenzi inasemekana lilianza kusuasua kabla ya mechi mbili za timu ya taifa, Taifa Stars zilizofanyika hapo na baada ya kuchezwa michezo hiyo wakandarasi walikuwa wakilipwa fedha zao kwa siku.

Habari za kuaminika kutoka katika duru za serikali zinasema kuwa matatizo hayo yalitokana na fungu la Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kutoka Hazina kuchelewa kuwafikia.

``Hali ilianza kuwa ngumu baada ya mechi mbili za Stars zilizofanyika pale na hii yote imetokana na fedha za awamu ya pili za mradi huo kuchelewa kutolewa,`` kilisema chanzo hicho.

Juzi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Muhammed Seif Khatib alisema kuwa imeamua kutoutoa uwanja huo kutumika katika mashindano yoyote mpaka ujenzi wake utakapokamilika rasmi na kukabidhiwa kwao.

Khatib alisema kuwa kuna sababu kuu tano ambazo zimefanya wafikie maamuzi hayo licha ya kufahamu kuwa mashindano hayo yanamsisimko mkubwa na kuongeza kuwa maamuzi waliyotoa yametokana na kuthamini fedha za walipa kodi waliotoa kufanikisha ujenzi huo.

Waziri alisema kuwa si vyema kuruhusu uwanja kutumika hali ya kuwa sehemu ya kukimbilia imechimbuliwa tayari kutengenezwa upya kwa kufuata maelekezo ya Chama cha kimataifa cha riadha (IAAF) ambapo mashabiki wanaweza kuharibu na kuleta usumbufu.

Hiyo ni moja ya sababu nyingine iliyopelekea kutotoa ruhusa ya kuutumia kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji ya Afrika Mashariki na Kati yanayotarajiwa kuanza Desemba 8 hadi 22.

Wakati huo huo, TFF imesema mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Bara, Kilimanjaro Stars na Zambia, Chipolopolo iliyofanyika juzi iliingiza sh. Milioni 24.8.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom