Ujenzi wa Taasisi za Serikali ya Zanzibar Jijini Dodoma kuanza ndani ya wiki moja

WAKUDAMSH

JF-Expert Member
Sep 17, 2018
618
1,000
Wizara zenye kushugulika na Muungano ofisi zake zote zipo Tanganyika. Wizara za Mambo ya Ndani, Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Mambo ya Nje ambazo ndiyo mhimili wa dola.
Katika Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar hakuna kuzungumzia ukubwa bali ni wadau wawili sawa wanaounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( Tan + Zan + ia).
Usawa wa wadau hawa ktk Muungano bila kujali 'ukubwa' , ingependeza mhimili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuweka makao yake Zanzibar ili sehemu hii nyengine ya Muungano kufaidi uwepo wa Taasisi kubwa ya Muungano visiwani na kuchuma manufaa yake kiuchumi, kisiasa na kijamii na kuuimarisha muungano huu kivitendo.
Dodoma iwe ni Bunge la Tanganyika . Mfano Jamhuri ya Afrika ya Kusini inaundwa na muungano wa state 4 ambazo ni za Cape Province, Transvaal Province, Natal Province and Orange Free State Province.
Hizo state 4 zinazounda nchi ya Republic of South Africa ((RSA) kufaidi muungano huo na majimbo 9 ambayo ni Western Cape, Eastern Cape, Northern Cape, North West, Free State, Kwazulu Natal, Gauteng, Limpopo and Mpumalanga.
Mhimili wa dola makao yake makuu yapo Pretoria jimbo la Gauteng , huku mhimili wa Bunge la Jamhuri / Legislative lipo Cape Town ktk jimbo laWestern Cape na mhimili wa Mahakama Kuu makao yake yapo Bloemfontein jimbo la Free Orange. Mgawanyiko huu ni kusambaza faida za 'muungano' .
Sawa Zanzibar tayari wanalo bunge lao linalojadili mustakabathi wa Zanzibar na watu wake we huoni kupeleka bunge kule kutalimeza hili na kuondoa maana kbs,kwa mtazamo wangu mimi naona waendelee kushughulikia kero za muungano,pia iangaliwe namna bora ni kwa namna gani Zanzibar itajitegemea yenyewe pasipo kuidekea dekea bara,kama kuna madeni ilipe na pia Zanzibar iachwe ifanye maamuzi yenyewe kwnye kusimamia na kunufaika na rasilimali zake yenyewe.Shida baadhi ya wa Zanzibar wanatamani mwarabu arudi tena awatawale wakafanye kazi za uyaya na kusoma juzuu upenuni.Sisi wenyewe tunaweza amini nchi hizi mbili ndani ya jamuhuri moja zitastawi sana ndani ya miaka kumi ijayo kukata mzizi wa fitna 2035 linatandikwa daraja kuunganisha nchi hizi mbili, InshAllah,Zanzibar itainjoi sana,huna haja ya kuweka bunge watu watakuwa wanaflow tu,bata Zanzibar muda wowote tena ndani ya muda mfupi,swala la ardhi Zanzibar haitakuwa inshu tena unaweza ukalala bara kazi zako visiwani,safi kbs.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,605
2,000
Shida baadhi ya wa Zanzibar wanatamani mwarabu arudi tena awatawale wakafanye kazi za uyaya na kusoma juzuu upenuni
Ndiyo tatizo la wanasiasa wa CCM Mpya kuwa na visheni duni kusingizia mabebebe-ruhani au Mwarabu-ruhani ambao Hawapo kiuhalisia wala kuonekana, Zanzibar inaweza kuwa kama Hongkong au Dubai kama serikali ya Muungano itaacha kufanya maamuzi mabaya kuwekeza Dodoma badala ya Zanzibar.
 

chilubi

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
8,028
2,000
ofisi za Taasisi za SMZ zinafanya nini bara? Mrudisheni Ally Kessy Bungeni kiboko yao CCM Zanzibar/SMZ
 

conservative3

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
1,070
2,000
Ndiyo tatizo la wanasiasa wa CCM Mpya kuwa na visheni duni kusingizia mabebebe-ruhani au Mwarabu-ruhani ambao Hawapo kiuhalisia wala kuonekana, Zanzibar inaweza kuwa kama Hongkong au Dubai kama serikali ya Muungano itaacha kufanya maamuzi mabaya kuwekeza Dodoma badala ya Zanzibar.
Znz kuna majengo yao znz na bara wakiwa wanataka kufanya shughuli zao za kiznz wanatumia majengo yapi wakati serikali iko dom?km rais yuko dom then wazir kiongoz dar itamuitaji kusafiri mara kwa mara kutoka dar kwenda dom .je gharama haitakuwa kubwa?
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,605
2,000
Znz kuna majengo yao znz na bara wakiwa wanataka kufanya shughuli zao za kiznz wanatumia majengo yapi wakati serikali iko dom?km rais yuko dom then wazir kiongoz dar itamuitaji kusafiri mara kwa mara kutoka dar kwenda dom .je gharama haitakuwa kubwa?
Hapo tunaangali mtu badala ya Maendeleo ya Watu.

Ikiwa Bunge la Muungano na mhimili wa Bunge la Muungano likawa na makao yake Zanzibar ndiyo kuimarishwa kwa Muungano kwani itachochea pia Zanzibar kukua kiuchumi na kibiashara huku ikipelekea kuwa kitovu cha biashara kanda hii ya Afrika Mashariki na Kati.

Dodoma haina uwezo huo kijiografia, tuuimarishe muungano huu kwa vitendo sahihi kwa Zanzibar na Tanganyika.
 

conservative3

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
1,070
2,000
Hapo tunaangali mtu badala ya Maendeleo ya Watu.

Ikiwa Bunge la Muungano na mhimili wa Bunge la Muungano likawa na makao yake Zanzibar ndiyo kuimarishwa kwa Muungano kwani itachochea pia Zanzibar kukua kiuchumi na kibiashara huku ikipelekea kuwa kitovu cha biashara kanda hii ya Afrika Mashariki na Kati.

Dodoma haina uwezo huo kijiografia, tuuimarishe muungano huu kwa vitendo sahihi kwa Zanzibar na Tanganyika.
Sababu ya bunge kuwa znz ni zipi?ambazo dodoma haistahili?
Tayari znz kuna maeneo ya ofisi za kimuungano k.m ulinzi mambo ya ndani nk.
Bado wa znz wanalalaimika kuwa aedhi yao ni ndogo hivyo ndo maana wanaweka mashart kununua kwa watu wa bara je kuendelea kuchukua ardhi si kuongeza kero..maana ukijenga maofisi kuke pia usisahau wapo watakaotaka ndani ya mwaka mmoja ajenge nyumba asikae kota au vinginevyo..km kufungua bar na biashara zingine.
Kati ya bara na znz nani ni rahisi kumu accomodate mwenzake?
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,605
2,000
Sababu ya bunge kuwa znz ni zipi?ambazo dodoma haistahili?
Kuimarisha muungano, mhimili wa dola na mhimili wa Mahakama vipo Tanganyika kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhimili uliobaki wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ungepeleka makao yake Zanzibar .

Hii ya Bunge la Muungano kuwa na kukutana Zanzibar mbali ya kuimarisha Muungano kisiasa pia utachochea uchumi maana wabunge 300 wasaidizi wao, wafanyakazi wa sekretariati ya Bunge la Muungano , wageni walikwa n.k wote kuwepo Zanzibar ni pia kuimarisha uchumi wa upande mwingine ambao ni mdau wa Muungano. Hivyo faida ni kubwa na kuweza kuigeuza Zanzibar kuwa Dubai kibiashara, kimajengo, kiburudani, kiajira mtambuka n.k

Mihimili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Dola, Mahakama na Bunge yote kuwapo Tanganyika wakati imevaa joho la Muungano ni choyo kubwa kwa mdau mmoja kujinufaisha pekee yake kiuchumi, kibiashara na kimapato mbali ya kisiasa.
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
7,231
2,000
Huko ni kujipendekeza.
Yaani unachukuaje pesa za wazanzibar na kuzipeleka Dodoma kujenga majengo ya watanganyika?
Huo ni zaidi ya upumbavu.
 

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,404
2,000
Na uhakika mzee Abeid Karume asingekubali maamuzi ya serikali awamu ya Mwinyi Junior ya SMZ kwenda kujenga Dodoma masuala ya muungano. Tayari Tanganyika imefaidi vya kutosha.

Na Mzee Abeid Karume baharia mstaafu aliyesafiri sehemu nyingi ugaibuni angepigania baadhi ya shughuli na majengo ya taasisi za Muungano kuwa na makao yake Zanzibar ili kuchochea uchumi na biashara upande wa Zanzibar badala ya kuwekeza Dodoma kusipo na faida yoyote zaidi ya asilimia 4% ya mgao wa fedha toka kwa waziri wa fedha wa Tanganyika chini ya mwamvuli wa muungano.

Nipo sawa na wewe
 

wagagagigi

JF-Expert Member
Dec 9, 2014
883
1,000
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdallah ametoa Wiki moja kwa Taasisi za Ardhi, Mipango Miji pamoja na Wakala wa Ujenzi Zanzibar kukamilisha utaratibu utakaowezesha kuanza kwa ujenzi wa Majengo ya Taasisi za Serikali katika Mji Mpya wa Dodoma.

Amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Ofisi ya uratibu wa shughuli za Serikali iliyopo Jijini Dar es Salaam ihamie Dodoma ndani ya kipindi kifupi.

Hemed Suleiman ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara Maalum ya kutembelea eneo lililokabidhiwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Kujenga Ofisi hizo katika eneo la Mji mpya Jijini Dodoma likiwa na ukubwa wa hekta 33.

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kuhamishia Makao Makuu ya shughuli za Serikali Jijini Dodoma katikati ya ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uamuzi uliokwenda sambamba na kuzingatia wazo la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alilolitoa mwanzoni mwa miaka ya 60. View attachment 1625922
Sisi wazanzibari hatuna haja ya majengo ya serikali Dodoma!
 

Rogojin The Idiot

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
1,899
2,000
Makao makuu ya nchi ya Tanganyika yapo wapi? Maana nchi ya Zanzibar mji mkuu wake ni Unguja /Zanzibar.

Hii ni mojawapo ya kero za Muungano kulazimisha nchi ya Zanzibar kuhamishia Ofisi zake katika mji ambao ni makao makuu ya Tanganyika iliyofichwa ktk joho la Muungano.

Dodoma ni makao makuu ya nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ningeshauri Bunge la Muungano wa Tanzania wapeleke makao yake makuu Unguja ili Zanzibar nayo ifaidike kiuchumi kwa shuguli za kimuungano za kufanya vikao vyake vyote Zanzibar na siyo Tanganyika ifaidi kila kitu huku Zanzibar ikisubiri 4% ya mgao wa fedha ambayo ni ndogo kama baadhi ya taasisi taasisi za Muungano zingepeleka makao yake Zanzibar.

Mifano ya faida za kiuchumi kwa Zanzibar ni Nyumba za wabunge wa Muungano zingejengwa Unguja, Ukumbi wa Bunge na sekretariati yake Unguja, boti na ndege kibao zingeenda Unguja, magari ya kukodisha na mafuta n.k yangetumika Zanzibar , wageni wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wangejazana Unguja na kuongeza idadi ya wageni badala ya kutegemea wageni watalii, kazi za udobi, starehe, burudani kuhudumia mamia ya watu wanaoenda Bunge la Muungano likiwa Zanzibar hii ni mifano kiduchu tu Wazanzibari wangefaudu matunda ya Muungano na kelele kupungua

Kuna nchi inaitwa tanganyika? Muulizieni Mtikila huko alipo kama kuna nchi inaitwa Tanganyika
 

for life

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
2,670
2,000
Zanzibar nikikumbka walivyopiga pesa za tanesco wakatutishia watawasha vibatari magu akawasamehe hizo hela tutazirudisha wakianza kuchimba mafuta
 

conservative3

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
1,070
2,000
Kuimarisha muungano, mhimili wa dola na mhimili wa Mahakama vipo Tanganyika kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhimili uliobaki wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ungepeleka makao yake Zanzibar .

Hii ya Bunge la Muungano kuwa na kukutana Zanzibar mbali ya kuimarisha Muungano kisiasa pia utachochea uchumi maana wabunge 300 wasaidizi wao, wafanyakazi wa sekretariati ya Bunge la Muungano , wageni walikwa n.k wote kuwepo Zanzibar ni pia kuimarisha uchumi wa upande mwingine ambao ni mdau wa Muungano. Hivyo faida ni kubwa na kuweza kuigeuza Zanzibar kuwa Dubai kibiashara, kimajengo, kiburudani, kiajira mtambuka n.k

Mihimili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Dola, Mahakama na Bunge yote kuwapo Tanganyika wakati imevaa joho la Muungano ni choyo kubwa kwa mdau mmoja kujinufaisha pekee yake kiuchumi, kibiashara na kimapato mbali ya kisiasa.
Unasahau kuwa maeneo yaliyo chini ya wizara za kimuungano km jwtz waznz wanaona ni maeneo makubwa..yanapaswa kupunguzwa leo ukamege eneo tena uanze kujenga any way kupanga ni kuchagua..
Bunge halikujengwa zama hizi na pia hata mahakama haikujengwa zama hizi kwa nn useme bunge lihame usiseme mahakama...niambie impact ya mahakama kujengwa znz au mwanza ?kwa kuwa hiyo mahakama inaketi hata znz kusikiliza mashauri haibase dar pekee. Na watumishi wangapi wa mahakama.
Rais wa muungano automatic anakuwa rais wa tanganyika hilo ndio lilofanya awe na makazi bara. Kwa kuwa znz ana msaidizi ambaye ni rais wa znz.
Znz kimsingi hawapendi ardhi yao.iguswe na bara ndo maana hata mtu wa bara kwenda kununua ardhi kana kwamba mtu anatoka kenya...ila linapokuja suala la serikali ya bara kujenga miundo mbinu bara na kuwakaribisha wazanzibar inaonekana upendeleo....
Dodoma hata leo nenda kwa mgogo kununua ardhi km utakutana na mashart lukuki km znz..
Unawapeleka wabunge znz wataanza kulalamikiwa mara fujo mara maadili mara wamechukua eneo kubwa nk...
Ofisi inayojengwa dodoma ni ya wazazibar kwa ajili ya mqmbo ya muungano kwa wazanzibar ila bara wana ofisi yao ya mambo yq muungano.
Serikali ya znz imetenga hekta ngapi kwa ajili ya ofisi za muungano?
Unaamin znz hakuna ofisi ya muungano kwa ajili ya mambo ya muungano?.
 

Rogojin The Idiot

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
1,899
2,000
Hata sukari ya Zanzibar hawaitaki vipi hayo majengo ya Zanzibar yatawasaidia wazanzibari? Ni kupoteza fedha za walipa kodi tu Wallah

Nani kaikataa sukari ya Zanzibar? Na magari je? Tunakuza sana mambo wakati mwingine. Mbele ya safari, Tanzania bara ndio itakuwa salama ya Zanzibar kwenye ardhi. Population growth ya Zanzibar inatisha na naona mnajisahau sana kuwa wengi wako bara wanafanya shughuli zao za kimaisha
 

conservative3

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
1,070
2,000
Hata sukari ya Zanzibar hawaitaki vipi hayo majengo ya Zanzibar yatawasaidia wazanzibari? Ni kupoteza fedha za walipa kodi tu Wallah
Zanzibar ukiangalia mahitaji yao kwa mwaka na uzalishaji ni kwamba uzalishaji ni mdogo kuliko mahitaji hivyo imewalazimu kuqgiza nje sukari kukidhi mahitaji yao ya ndani.
K. Suala la kuagiza nje mfanyq biashara yyte anaweza kuagiza nje la msingi unalindaje walipakodi wako?
Kwa kuwa gharama ya uzalishaji kwa nje iko chini kuliko bara..znz hawqkukatazwa ila wameambiwa walipe kodi km mtibwa na kilombero na kagera..hilo hawataki
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,605
2,000
Hata sukari ya Zanzibar hawaitaki vipi hayo majengo ya Zanzibar yatawasaidia wazanzibari? Ni kupoteza fedha za walipa kodi tu Wallah
Zanzibar inatakiwa iwe kitovu kikuu cha biashara kwa Tanzania ili biashara ya sukari n.k ifike Burundi, Rwanda, DR Congo, Zambia , Malawi. Lakini Tanganyika maono yao kibiashara ni mafupi hawaoni fursa kubwa Zanzibar ikipewa nafasi kujinafasi kama enzi za biashara za dola kubwa ya Zanzibar empire kote Afrika Mashariki mpaka ndanindani kwa Wangwana Congo. Ubelgiji iliona choyo ikawepo vita katika ya Dola-Kubwa ya Hiyama ya Zanzibar na Ubelgiji The Belgian-Arab War , kimsingi ilikuwa vita vya kibiashara.

Tanganyika pia inataka kuzuiwa maendeleo ya kibiashara ya mshirika wake ktk Muungano yaani Zanzibar. Zama hizi za biashara kubwa kubwa za kimataifa kuifanya Zanzibar iwe "Kariakoo" kuu (Dubai) ya biashara kanda hii ya Afrika bado Tanganyika haijaielewa dhana hii au inafanya kusudi kuididimiza Zanzibar kimaendeleo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom