Rahma Salum
Member
- Sep 7, 2020
- 30
- 59
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdallah ametoa Wiki moja kwa Taasisi za Ardhi, Mipango Miji pamoja na Wakala wa Ujenzi Zanzibar kukamilisha utaratibu utakaowezesha kuanza kwa ujenzi wa Majengo ya Taasisi za Serikali katika Mji Mpya wa Dodoma.
Amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo lililotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Ofisi ya uratibu wa shughuli za Serikali iliyopo Jijini Dar es Salaam ihamie Dodoma ndani ya kipindi kifupi.
Hemed Suleiman ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara Maalum ya kutembelea eneo lililokabidhiwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Kujenga Ofisi hizo katika eneo la Mji mpya Jijini Dodoma likiwa na ukubwa wa hekta 33.
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kuhamishia Makao Makuu ya shughuli za Serikali Jijini Dodoma katikati ya ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uamuzi uliokwenda sambamba na kuzingatia wazo la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alilolitoa mwanzoni mwa miaka ya 60.