Ujenzi wa SGR unaendelea vizuri kama ulivyopangwa

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
296
681
Waziri Fedha na Mipango Dr Philip Mpango amesema Ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Standard Gauge: Ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (km 300) unaendelea vizuri kama ilivyopangwa, ambapo shughuli zinazoendelea ni ujenzi wa madaraja, makalavati, daraja lenye urefu wa km 2.54 katikati ya jiji la Dar es Salaam, ukataji wa miinuko, ujazaji wa mabonde na utandikaji wa reli.

Aidha amesema katika kipande cha Morogoro – Makutupora (km 422), kazi zinazoendelea ni pamoja na ukataji wa miinuko na ujazaji wa mabonde, usanifu wa njia na ujenzi wa kambi za Kilosa na Ihumwa. Kwa upande wa kipande cha Isaka – Rusumo (km 371), hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa njia ya reli.

Aidha, taratibu za ununuzi wa mabehewa, injini na mitambo itakayotumika kutoa huduma ya usafiri kwenye reli ya Standard Gauge zipo katika hatua za mwisho.Katika miradi inayogharamiwa na mfuko wa reli, shughuli zilizofanyika ni: kununua vichwa 11 vya treni kwa ajili reli ya kati; kuendelea na ukarabati wa reli ya Tanga – Arusha (km 439) ambapo kipande cha Tanga – Mombo (km 129) kimeanza kufanya kazi ya kusafirisha mizigo na ukarabati wa vipande vya Mombo – Same (km124) na Same – Arusha (km 186) unaendelea. Aidha, kazi ya ukarabati wa mabehewa inaendelea ambapo hatua iliyofikiwa ni kukamilika kwa ukarabati wa mabehewa 15.
 
Kusimamia na kuendesha mwendo kasi kutoka kutoka Kimara kwenda mjini kizungumkuti.Sijui hizo treni za umeme tutaweza!!
 
Kusimamia na kuendesha mwendo kasi kutoka kutoka Kimara kwenda mjini kizungumkuti.Sijui hizo treni za umeme tutaweza!!
Mwendokasi upo incorporated kati ya serikali na watu binfasi, haifananishwi na SGR mkuu,
 
Hongera kadogosa, huyu baba Baclays UK wanamlilia sana ni jembe.
 
Hesabu ni Rahisi Sana.
Na-Assume
Watanzania Wanaomsupport Lissu tuko= 5000000(5 million).

Kila Mmoja Atadeposit 2,000/= kila Mwezi karibia na Tarehe 15.

Total itakuwa 10,000,000,000(10 Billion).

Hii ni zaidi ya Mshahara,posho,pension na Marupurupu ya Mbunge Kwa Miaka 5.

Watanzania Tukiamua Tunaweza.

TUMCHANGIE TUNDU LISSU SASA.

TUNDU LISSU RAIS 2020.

"Mopao Mokonzi"
 
Mchango kwan amefiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom