Ujenzi Wa Reli Ya Kimataifa Dar Es Salaam hadi Morogoro Washika Kasi

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019


NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Serikali imedhamiria kwa dhati kukamilisha mradi mkubwa wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), ambapo tayari kiasi cha zaidi ya shilingi trilioni 2 kimetolewa mpaka sasa kwa ajili ya ujenzi huo.

Dkt. Kijaji ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi eneo la Soga, umbali wa kilometa 53, na kujionea maendeleo makubwa ya ujenzi wa reli hiyo.

Ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wake na kumpongeza mkandarasi anaye jenga reli hiyo, Kampuni ya Yapi Merkezi, kwa kutekeleza ujenzi huo kwa viwango vya hali ya juu ambapo ameelezwa kuwa, treni ya kwanza kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro inatarajia kuanza safari zake Mwezi Novemba mwaka huu kama kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.

"Ninampongeza sana Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake kubwa na kuamua kwa dhati kutekeleza mradi huu mkubwa na miradi mingine, ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya maporomoko ya maji ya Mto Rufiji, ambayo kukamilika kwake kutachochea uchumi wa viwanda" alisema Dkt. Kijaji

"Tunakwenda kwenye Tanzania ya viwanda, tutakuwa na viwanda kila mahali, tumeanza ujenzi wa mradi wa umeme wa megawat 2,115, viwanda vitazalisha bidhaa ambazo zitahitaji miundombinu ya usafirishaji, reli hii itatumika na tunatarajia ifikapo mwaka 2025, Tanzania itakuwa ni nchi yenye kipato cha kati" aliongeza Dkt. Kijaji

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, Mhandisi Machibya Masanja, amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo umekamilika kwa asilimia 42.

"Mradi wetu unaenda vizuri na kwa wakati, zoezi la ujenzi na utandikaji reli tumeanza katika Jijini la Dar es Salaam umeanza na unaendelea vizuri ambapo ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 55 na utandikaji wa reli katika Jiji hili utafikia kilometa 10 mwishoni mwa mwezi Februari" alifafanua Mhandisi Masanja.

na nguvu kubwa imeelekezwa katika ujenzi wa tuta na madaraja, zezi ambalo limefikia asilimia 55 hivi sasa" alifafanua Mhandisi Masanja

Ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma hadi Mwanza, na baadae kuunganisha mtandao wake na nchi jirani za Kongo, Uganda, Burundi na Rwanda, unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi trilioni 7.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezungumza na wakazi wa eneo la Guluka Kwalala, Gongo la Mboto, waliokuwa wakiendelea na taratibu zao za kulipwa fidia ambapo amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwaletea maendeleo.

Baadhi ya wakazi hao, pamoja na kuiomba Wizara ya Ardhi na Makazi iwasaidie kupata viwanja kwa ajili ya kujenga makazi yao baada ya kulipwa fidia kupisha ujenzi wa mradi huo wa Reli ya Kisasa, wamempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kusimamia ustawi na maendeleo ya nchi na kuahidi kuendelea kumuunga mkono.
 
Habari Njema kwa watanzania wote wapenda maendeleo.
Zoezi la Reli la utandikaji wa reli ya Standard Gauge (SGR) Sasa imeingia rasmi jijini Dar es Salaam na kwa sasa zoezi hilo linafanyika eneo la Vingunguti jijini hapa.

Naibu Waziri wa fedha amelidhishwa na maendeleo ya mradi huo huku akisema mpaka sasa Serikali imeshatoa zaidi ya Trillion 2 kwenye mradi wa Reli ya SGR.

Kwa habari zaidi karibu katika youtube page ya TRC uone zaidi.
 
Kazi nzuri
Ili eneo la Vingunguti napitaga kila siku hapa sina ata lisaa limoja toka nipite kazi ni usiku na mchana kwakweli! Kama utakuwa mpitaji wa nyerere road kama unatokea Tazara unaenda Airport ukafika Vingunguti mataa ukaingia barabara inayoshuka machinjioni hapo ndipo kuna shughuli tokea hapo kwenye kiwanda cha Bakharesa Ice-cream kuitafuta kipawa ni full kazi aisee.
 
Ni vyema watanzania tukaanzisha utamadini wa kuchangia majimbo yaliyo nyuma kimaendekeo, ifike siku bweni, shule au hospitali ikijengwa Singida mashariki au Simanjiro tusikie imejengwa kwa msaada wa wanajimbo wa Ukonga, Kibamba, Arusha, Ilala, Hai, Vunjo nk. Hii itakuwa tamaduni nzuri sana watanzania wenzangu.
 
Kodi zetu wala haku a haj ya kumsifu sn tena amefanya bil makubaliano ....kiongozi anapaswa kutuambia na kufanya kitu kipya kabisa mabwawa ns reli yalikuwa lwenye mipango...... ccm ingekuaa na uthubutu ingeketa katiba mpyA
 
Habari Njema kwa watanzania wote wapenda maendeleo.
Zoezi la Reli la utandikaji wa reli ya Standard Gauge (SGR) Sasa imeingia rasmi jijini Dar es Salaam na kwa sasa zoezi hilo linafanyika eneo la Vingunguti jijini hapa.

Naibu Waziri wa fedha amelidhishwa na maendeleo ya mradi huo huku akisema mpaka sasa Serikali imeshatoa zaidi ya Trillion 2 kwenye mradi wa Reli ya SGR.

Kwa habari zaidi karibu katika youtube page ya TRC uone zaidi.

Hapakazitu Kuleni mbuzi kwa sana kwa order yangu ...wakandarasi na wafanyakazi wa TRC ..
 
Mkoloni pia alikuwa na uwezo wa kujenga leli bora kuzidi hii lakini Mwalimu Nyerere alimfukuza mkoloni kwa sababu Tanzania inahitaji _________________________nawala haitaki_______________________ikiwa nchi haitakuwa na hiyo_____________________hiyo_______sisi haitotusaidia kitu.
Mwenye akili ajaze nafasi wazi nimpe ka vocha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkoloni pia alikuwa na uwezo wa kujenga leli bora kuzidi hii lakini Mwalimu Nyerere alimfukuza mkoloni kwa sababu Tanzania inahitaji _________________________nawala haitaki_______________________ikiwa nchi haitakuwa na hiyo_____________________hiyo_______sisi haitotusaidia kitu.
Mwenye akili ajaze nafasi wazi nimpe ka vocha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatuitaji maneno ya kusadikika acha tufanye vitu ambavyo ni touchable and visible
 
Hongera Tanzania sasa nasi tunaingia kwenye maendeleo(kwa tafsiri ya sisi wanadamu).

Huwa nawaza ni kwa nini binadamu tukaamua kuwa maendeleo yahusishe kubadilisha taswira ya Dunia kwa constructions, na si kuboresha mali asili tuliyorithi, nawaza pale ambapo miji yote na vijiji vitakapokuwa vimeendelea sana na kufanana na new York city dunia itafananaje? Hapa namaanisha vijiji vyote ndani ya kigoma, singida, huko umasaini na dunia nzima vina matreni ya umeme, magorofa, magari ya kisasa n.k

Mji niliopo una joto kweli tofauti na miaka 30 iliyopita, kwa sababu ya maendeleo tumekata miti kweli, na ni kweli tuna maendeleo, magorofa, maji ya bomba, lami, nguzo za umeme.

zamani ilikuwa ukitembea unakutana na miti mikubwa ya asili,ndege wa aina mbalimbali, hewa nzuri na baridi. Sasa tuna lami, tunaendesha magari kwa raha, magorofa yenye lift na AC Ila Ile miti haipo tena, kuna aina flani ya ndege hawaonekani tena, hewa ina utofauti na hali ya hewa haitabiriki, kunaweza kukawa na joto na jua kali kupitiliza kitu ambacho hakikuwepo kabla.

Anyway sababu hii ndo tafsiri binadamu wote duniani tuliyoichagua ya maendeleo, tujipongeze kwa hatua tuliyopiga.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom