Ujenzi Wa Reli Ya Kimataifa Dar Es Salaam hadi Morogoro Washika Kasi

Habari Njema kwa watanzania wote wapenda maendeleo.
Zoezi la Reli la utandikaji wa reli ya Standard Gauge (SGR) Sasa imeingia rasmi jijini Dar es Salaam na kwa sasa zoezi hilo linafanyika eneo la Vingunguti jijini hapa.

Naibu Waziri wa fedha amelidhishwa na maendeleo ya mradi huo huku akisema mpaka sasa Serikali imeshatoa zaidi ya Trillion 2 kwenye mradi wa Reli ya SGR.

Kwa habari zaidi karibu katika youtube page ya TRC uone zaidi.

"Hongera sana Serikali"
 
JPM kiboko yao mgao wa umeme si hoha tena, tumesahau ya,maendeleo ya mgao wa umeme. Magazeti, redio na TVs walitajirika kwa malipo kutoka Tanesco ya matangazo ya ratiba za mgao wa umeme.

Kuliepusha hili shirika la umeme na kijirudia kwa na hasara na aibu liloloitia Taifa huko nyuma na pendekeza jina lovadilishwe na itasaidia Watanzania kusahau machungu lilllotuletea.

Vitu kama madawati sio ishu pasua kichwa, hatushangai CDM kubakia na agenda ya ulaghai na uongo na wana upepeta kwelikweli..
 
kwa taarifa nilizozipata mpaka Disemba mwaka huu ngoma itakua imekamilika mpaka morogoro.
 
kwa taarifa nilizozipata mpaka Disemba mwaka huu ngoma itakua imekamilika mpaka morogoro.

Wangeleta Engines na mabehewa machache ikaanza safari za DRT kwa abiria DSM mpaka pugu angalau. Chenji ianze rudi mdogomdogo. Pugu sitesheni 30 seconds. Chezea Magufuli wewe!!
 
Utekelezaji unaendelea. ..tunaahidi na kutekeleza..

Maendeleo ya Vitu na sio ya Watu yana maana gani Mkuu ,hebu tupatie Faida kadhaa kuwa na Miundombinu ambayo ita washinda Raia kuitumia kwa Sababu ya Hali zao za Uchumi ?
 
Yaani reli ya Dar-Moro ni ya kimataifa? Au unamaanisha kiwango cha kimataifa? Kwa vyovyote, naipongeza serikali.
 
Wakati JPM anatangaza mpango wake wa kujenga reli ya umeme kuna watu walimuita mwehu anaota ndoto za mchana.
 
Wengine wapo busy kuzungusha mabakuli ya msaada wa kulipia watoto wao ada
 
Wangeleta Engines na mabehewa machache ikaanza safari za DRT kwa abiria DSM mpaka pugu angalau. Chenji ianze rudi mdogomdogo. Pugu sitesheni 30 seconds. Chezea Magufuli wewe!!
mradi una phase nne kama sijakosea; ya kwanza ambayo ni toka Dar to Moro niliambiwa itakamilika Disemba kama kutakuwa na mabadiliko itakua ni changamoto za kiutendaji tu.
 


NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Serikali imedhamiria kwa dhati kukamilisha mradi mkubwa wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR), ambapo tayari kiasi cha zaidi ya shilingi trilioni 2 kimetolewa mpaka sasa kwa ajili ya ujenzi huo.

Dkt. Kijaji ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi eneo la Soga, umbali wa kilometa 53, na kujionea maendeleo makubwa ya ujenzi wa reli hiyo.

Ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wake na kumpongeza mkandarasi anaye jenga reli hiyo, Kampuni ya Yapi Merkezi, kwa kutekeleza ujenzi huo kwa viwango vya hali ya juu ambapo ameelezwa kuwa, treni ya kwanza kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro inatarajia kuanza safari zake Mwezi Novemba mwaka huu kama kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa.

"Ninampongeza sana Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake kubwa na kuamua kwa dhati kutekeleza mradi huu mkubwa na miradi mingine, ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme kwa njia ya maporomoko ya maji ya Mto Rufiji, ambayo kukamilika kwake kutachochea uchumi wa viwanda" alisema Dkt. Kijaji

"Tunakwenda kwenye Tanzania ya viwanda, tutakuwa na viwanda kila mahali, tumeanza ujenzi wa mradi wa umeme wa megawat 2,115, viwanda vitazalisha bidhaa ambazo zitahitaji miundombinu ya usafirishaji, reli hii itatumika na tunatarajia ifikapo mwaka 2025, Tanzania itakuwa ni nchi yenye kipato cha kati" aliongeza Dkt. Kijaji

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR), kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, Mhandisi Machibya Masanja, amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo umekamilika kwa asilimia 42.

"Mradi wetu unaenda vizuri na kwa wakati, zoezi la ujenzi na utandikaji reli tumeanza katika Jijini la Dar es Salaam umeanza na unaendelea vizuri ambapo ujenzi wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 55 na utandikaji wa reli katika Jiji hili utafikia kilometa 10 mwishoni mwa mwezi Februari" alifafanua Mhandisi Masanja.

na nguvu kubwa imeelekezwa katika ujenzi wa tuta na madaraja, zezi ambalo limefikia asilimia 55 hivi sasa" alifafanua Mhandisi Masanja

Ujenzi wa Reli kwa Kiwango cha Kimataifa kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma hadi Mwanza, na baadae kuunganisha mtandao wake na nchi jirani za Kongo, Uganda, Burundi na Rwanda, unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi trilioni 7.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezungumza na wakazi wa eneo la Guluka Kwalala, Gongo la Mboto, waliokuwa wakiendelea na taratibu zao za kulipwa fidia ambapo amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwaletea maendeleo.

Baadhi ya wakazi hao, pamoja na kuiomba Wizara ya Ardhi na Makazi iwasaidie kupata viwanja kwa ajili ya kujenga makazi yao baada ya kulipwa fidia kupisha ujenzi wa mradi huo wa Reli ya Kisasa, wamempongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kusimamia ustawi na maendeleo ya nchi na kuahidi kuendelea kumuunga mkono.
Hii ndio habari ifaayo kusikika kwa watanzania, sio habari za yule mjinga kuwadi wa mabeberu TAL, acha baridi imnyooshe kwa ufala wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom