Ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” wapiga hatua kubwa barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,003
1,024
9500049_1_1_21c5390f-b671-4c8d-8f92-c9b2ee1d7558.jpg

Barabara ya mwendo kasi ya Nairobi Expressway, iliyowekezwa na kujengwa na kampuni ya China, imeanza kufanya kazi kwa majaribio. Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 27.1 itapunguza muda wa safari kutoka jijini Nairobi hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kutoka saa 2 hadi dakika 15. Barabara hiyo ni mradi mwingine muhimu wa ushirikiano kati ya China na Kenya kufuatia pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Kabla ya hapo, pande hizo mbili zimeshirikiana katika ujenzi wa miradi mingi mikubwa ya ushirikiano nchini Kenya, zikiwemo reli inayounganisha Naibori na Mombasa, bandari ya Lamu, na bandari ya Mafuta mjini Mombasa.

Kenya ni moja ya nchi zilizoshudhudia maendeleo makubwa ya ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” barani Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, kupitia pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, miradi mingi ya ushirikiano kati ya China na Afrika katika nyanja mbalimbali imetekelezwa, na kupata mafanikio makubwa. Zaidi ya miaka 600 iliyopita, msafara wa Zheng He ulifika maeneo ya pwani ya Afrika Mashariki. Historia ndefu ya mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika imeweka msingi imara kwa pande hizo mbili kukuza uhusiano. Mwezi Desemba 2015, Afrika Kusini ilikuwa nchi ya kwanza ya Afrika kusaini ushirikiano wa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na China. Hadi sasa, karibu nchi zote za Afrika ambazo zina uhusiano wa kidiplomasia na China zimejiunga na pendekezo hilo. Kamati ya Umoja wa Afrika pia imekuwa shirika la kwanza la kikanda lililosaini ushirikiano wa ujenzi wa pamoja wa pendekezo hilo.

Ujenzi wa miundombinu ni sekta ya kijadi ya ushirikiano kati ya China na Afrika. Maendeleo ya kasi katika miongo iliyopita yameipatia China uzoefu na uwezo mkubwa katika ujenzi wa miundombinu, na kampuni zake zinahitaji kwenda nje ya nchi ili kupata maendeleo zaidi. Wakati huo huo, hali duni ya miundombinu barani Afrika imekuwa kizuizi kikubwa cha maendeleo ya bara hilo. Ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umeleta fursa kubwa kwa pande hizo mbili kuzidisha ushirikiano. Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi, Kampuni za China zimejenga zaidi ya kilomita 6,000 za reli na kilomita 6,000 za barabara, kujenga au kukarabati takriban bandari 20 na zaidi ya vituo vikubwa 80 vya umeme barani Afrika.

Pendelezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” pia limeleta uwekezaji kwa nchi za Afrika. Afrika ndilo bara linalohitaji uwekezaji wa nje zaidi duniani, na pengo lake la uwekezaji katika miundombinu limefikia dola bilioni 100 za Kimarekani kwa mwaka. Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi, uwekezaji wa China barani Afrika umezidi dola bilioni 43 za kimarekani, na zaidi ya kampuni 3,500 za China zimeanzisha matawi yake na kuwekeza barani Afrika.

Ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” pia umestawisha biashara kati ya China na Afrika. China imeendelea kuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika tangu mwaka 2009. Katika miaka ya hivi karibuni, ili kuboresha muundo wa biashara kati ya pande hizo mbili, China imechukua hatua mbalimbali ili kuongeza maagizo ya bidhaa zisizo za maliasili kutoka Afrika, na kusamehe asilimia 97 ya bidhaa kutoka nchi 33 barani Afrika. Sasa Chini imekuwa soko la pili la bidhaa za kilimo za Afrika. Pia, tangu mwaka 2017, maagizo ya huduma ya China kutoka Afrika yameongezeka kwa wastani wa asilimia 20 kila mwaka.

Aidha, pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” pia limetoa jukwaa kubwa na fursa zaidi kwa ushirikiano kati ya China na Afrika katika nyanja za uchumi wa kidijitali, maendeleo ya kijani, afya ya umma, elimu, na utamaduni.
 
Back
Top Bottom