Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,272
Biashara hii ni sawa na duka la reja reja, inategemea sehemu ulipo, chumba chenye gypsum umeme, maji, madirisha ya aluminium hufika 70,000 - 80,000 kama nyumba iko karibu na mjini, au usafiri wa kwenda mjini si shida. Kwa sehemu za uchochoroni chumba huwa 30,000- 40,000.
Uzuri wa biashara hii ni kwa mwisho wa mwezi ni lazima utakusanya kodi. Changamoto inakuja kwa wapangaji wa muda mrefu mnakua mmezoeana na anapokosa hela ya kodiwkumfuka unashindwa. Wengine wanakueleza wanauguliwa, ada za watoto au wamefukuzwa kazi.
Changamoto nyingine ni idadi ya watu wanaokaa na kutumia miundo mbinu. Wengi wanaopanga nyumba hizi ni wa kipato cha chini. Unakuta mpangaji anauguliwa na mjomba wake na ukoo wao wote wako pale kuuguza. Hawafikiri maji, choo hasa kama ni choo cha shimo. Nyumba ya jirani choo kikijaa, mwenye nyumba anaweza kuomba watumie chako mpaka atakaporekebisha mambo kwake. Uswahilini maisha ni kusaidiana.
Ujenzi wa chumba na sebule ni advance na unatishia soko la wenye vyumba sita. Wakijiongeza watakao jenga simple one bedroom self contained nao watatishia soko la chumba na sebule.