X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,810
Ujenzi wa nyumba kwa siku moja wazinduliwa.
Na Peter Mwenda: Majira
TATIZO sugu la ukosefu wa makazi nchini limepata ufumbuzi baada ya kampuni ya Moladi Framework ya Afrika Kusini kuzindua teklonojia mpya ya ujenzi wa nyumba za
gharama nafuu na muda mfupi.
Mgunduzi wa teknolojia hiyo, Bw. Henrick Botes alisema Dar es Salaam jana kuwa ujenzi huo ambao aliugundua mwaka 1986 nchini Afrika Kusini, unatumia gharama ndogo na muda wa siku moja kumalizika.
Akionesha ujenzi huo katika nyumba iliyojengwa eneo la Wazo Hill Dar es Salaam jana, Bw. Botes alisema wanajenga ukuta kwa kutumia saruji na mchanganyiko ya vitu vingine ambayo ukuta wake unakauka baada ya saa nne.
Bw. Botes alisema kabla ya kumimina saruji hiyo njia za umeme, mabomba ya maji, fremu za majidisha, milango zinakuwa zinawekwa na baadaye siku ya pili makasha yanayosimamia ukuta yanaondolewa na kupachika madirisha, kupiga bati na kumalizia marumaru.
Alisema ujenzi wa nyumba yenye vyumba vitatu, sebule, choo na jiko hugharimu sh. mil. 20 bila kuingiza gharama za marumaru, madirisha ya kisasa na mabati ya thamani kubwa.
Bw. Botes alisema nyumba ambayo imewekwa marumaru na vitu vingine vya kisasa inagharimu sh. mil. 40 hadi mteja kukabidhiwa nyumba yake kuishi.
Alisema Kampuni ya Moladi Framework imefanikiwa ujenzi huo katika nchi za Zambia, Ghana, Zimbabwe, Angola, Botswana, Msumbiji, Nigeria na Afrika Kusini.
Alisema kampuni yake ya Moladi imefungua tawi nchini na mkandarasi aliyeteuliwa kwa sasa ni kampuni ya Holtan ya jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Moladi Framework nchini, Bw. Abeid Abdallah alisema kampuni yake ambao ni wakala pekee imedhamiria kutoa ufumbuzi wa uhaba wa makazi kwa kutengeneza nyumba kwa kutumia muda mfupi.