Financial Analyst
JF-Expert Member
- Nov 27, 2017
- 1,605
- 2,743
- Thread starter
- #21
Hongera mkuu, pia umenipa fundisho pia..Inaweza ikatosha au isitoshe, tafuta fundi akupe makadirio yake kwanza, ikiwa fundi ni mtu wako wa karibu itakuwa poa zaidi bei itapoa, ukiwa na muda uwepo site, material jitahidi kununua kwa jumla au lah km una idea ya ufundi usipattane na fundi boma zima, waje mafumdi wajenge uwalipe kwa tofali.
Kuna kibanda cha vyumba vi4, kimoja master na ukumbi wake, choo cha public, sebule, jiko, stoo na dinning, nimetumia kama milioni 20 hv bado finishing kidoogo hapo nishaipaua, madirisha, chini niliweka zzege, plasta, mabomba ya umeme tayari gypsum board.
Kilichonisaidia mimi ni kujuana na watu, kasoro boma tu ndio nilikubaliana na fundi akataka 1.8 huyu ni fundi wa huko huko ninakojengea(nimejenga kijijini, hivyo kuweka ukaribu na watu nikaona si vema kuchukua mafundi mbali, huyu aliwahi nitengenezea kisima) alipomaliza boma, kupaua akaleta michongo ya tamaa akataka milioni 2, nikapiiga chini, kuna shemeji yangu ni mtaalam wa kupaua nikamfata nikampa mikabala, akaniambiia ninunue vifaa vyoote aje apige kazi siku 2 tu nimuandalie laki 6, wiring nikamchek broo wangu mmoja akaniambia ninunue vifaa vyote aje apige kazi kwa siku mbili yeye hakutaka tsh 10 zaidi nikawapoza vibarua tu.
Plasta, zege la chini, shimo la choo na kukiset choo cha public, na gypsum nikampata mwanangu akanifanyia kazi kwa bei chee tu.
Madirisha nikanunua vifaa kuna kijana tunafanya nae mazoezi ya mpira sehemu akaja kunifanyia home, kila dirisha nilimpa elfu 15 kama sijakosea.
Hapo unaweza kupata picha kamili.
●Vitu kwa jumla
●Mafundi wenye ukaribu na mimi kama wapo..