Tetesi: Ujenzi wa miradi hii na vyanzo vyake vya mapato [funding]

Mzalendo JR

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,193
515
Kwanza nianze na pongezi kwa serikali ya jamhuri kwa kuchukua hatua katika kutekeleza mipango endelevu ya kiuchumi. Pia nimpe kongole alietamka kwa ukakamavu kua miradi hii ya Reli ya kati itakayofungua Dar Es Salaam Port kwa nchi nyingi ambazo hazina bahari (Landlocked countries), kua itajengwa kwa PESA ZETU WENYEWE. Kabla ya kuendelea naomba nitoe kipande cha hotuba ya Prof. Makame Mnyaa Mbarawa alioitoa bungeni kwenye bajeti ya 2016/17...

"....Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa kutumia Mfuko huu wa Reli, itachukua muda mrefu si chini ya miaka 300 kwa shilingi bilioni 50 ndiyo tuweze kupata trilioni 15. Kwa hivyo, Serikali sasa inaweka kipaumbele chake cha kwanza katika kujenga reli ya kati kupitia utaratibu wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu mwingine utakaoweza kutumika ni utaratibu wa ushirikiano baina ya nchi na nchi yaani Bilateral agreement ili kupata mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu. Serikali imeona mradi huu ni muhimu na tutasimamia kwa nguvu zetu zote ili tuhakikishe kwamba reli hiyo ambayo ina manufaa makubwa sana kwa nchi yetu hasa upande wa Congo kule na upande wa Burundi iweze kujengwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana ..."

Kwa undani wa hili jambo, Tanzania iko katika mazungumzo na Investiment banks za ulaya ili kupata mkopo wa dolla za kimarekani millioni 200. Mtu anaweza jiuliza nini kinatafutwa kwa kauli za viongozi kudai kua miradi hii inajengwa kwa fedha za ndani? Hapa wakimanisha ni makusanyo ya kodi zetu. Ukweli ni mzuri daima. Ikumbukwe Zambia ina skendo maarufu yani serikali ilikopa kimya kimya, baada ya uongozi kutoka madarakani ndio deni lisilojulikana la dolla Bilioni 2 likajulikana.

Tanzania ilijitoa kwenye mpango wa uendeshaji serikali kwa uwazi ambao awamu iliyopita iliridhia, sasa ni muda muafaka mipango kama hii kupita bungeni ili wabunge ambao ni wawakilishi wa watanzania waridhie kwa kua haya maamuzi yana athari kwao watanzania wa kawaida. Nia ni njema, lakini ni vema kutafula legitimacy ya watannzania kupitia Bunge. Kwa maelezo ya Makame hapo juu hakuna kilichotajwa kama mikopo toka Investment Banks, bali alisisitiza Bilateral treaties baina ya Tanzania na Nchi washirika wa maendeleo. Kigezo ni kupata unafuu wa riba. Did someone do a cost/Benefit analysis after his presentation in the parliament and decide to do otherwise? Nadhani kwenye hili andiko la serikali kuna ATCL revivig (Ununuzi ndege), Stiegler's Gorge Hydroelectric na SGR.

Pia ile kauli maarufu ya ....KWA PESA ZETU ZA NDANI igeuke na kua .....KWA PESA ZETU ZA KODI ZA BAADAE. Hii ni kwa sababu hii mikopo italipwa kwa kodi za watanzania hapo baadae, the maturity of which yawezekana serikali iliyoko madarakani inaweza kua imemaliza muda wake kikatiba. Maana baadae serikali ikianza kulipa hili deni, when a rational person asks when did we borrow such an amount while we built with our taxes ? Msipate kigugumizi cha unajua...unajua.


Mozambique Sues Credit Suisse in U.K. Over Debt Deals
Bunge Polis
Bloomberg - Are you a robot?
 
Baada ya utawala huu wa awamu ya 5 tutashuhudia matumizi mabaya mengi sana ya madaraka yalifanyika
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom