bandari ya mtwara ndio yenye kina kirefu tz nadhani hulijui hilo
Ndugu yangu usiligeuza suala hili muhimu la kiuchumi kuwa la kisiasa. Umuhimu wa bandari kwa uchumi wa Tanzania hauna ubishi. Yapo mambo ya msingi muhimu kufahamika:
Bandari ya Dar imeelemewa kwasababu ya wingi wa mizigo inayopitia katika bandari hiyo ndio maana kuna foleni za meli kuingia hapo Bandarini. Kuelemewa huko, kunasabasha jiji kuzidiwa na wingi wa magari ya mizigo na abiria (traffic congestion) yanayoingia na kutoka Bandarini. Zipo jitihada za kufanya upanuzi wa bandari hiyo kwa kujenga gati mpya no 13 na 14. Upanuzi huo ni suluhu ya muda mfupi katika handling ya mizigo, lakini hakutoa suluhu ya tatizo la congestion jijini....sana sana utaongeza congestion. Ni kwa msingi huo ujenzi wa bandari mpya ni jambo la muhimu.
Kwanini Bagamoyo?
Eneo la ujenzi wa bandari la Bagamoyo, lina kina kirefu na mlango mpana wa kuingizia meli zitakazohitaji kutia nanga. Hizo ni sifa kubwa zinazopelekea interest ya Wawekezaji wa sekta ya bandari kupendelea kuwekeza kule. Miaka 20 ijayo, meli zitakazojengwa zitakuwa ni 4th Generation zenye size kubwa kwa ajili ya kubeba mizigo mingi. Meli hizo hazitoweza kuingia kwenye lango la bandari ya Dar es salaam unless lifanyike zoezi la kupanua mlango wa bandari na kuchimba zaidi kuongeza kina....jambo ambalo itabidi kuchimba eneo kubwa mpaka ilipo Ikulu. Bandari ya Tanga na ile ya Mtwara vilevile zina disadvantage ya kutokuwa na Kina kikubwa kinachotakiwa kwa ajili ya hizo 4th generation ships. Sisemi kwamba haziwezi kutengenezwa zika accomodate meli za aina hiyo, la hasha. Inawezekana, lakini kwa gharama kubwa. Hivyo mtu anayetaka kuwekeza kwenye bandari ni rahisi zaidi kuwekeza Bagamoyo kule eneo lingine.
Lakini pia,duniani kote, bandari huwa zinafanya vizuri panapokuwa na eneo la Export Processing Zone na miundombinu mingine. Kule Bagamoyo next to eneo la BandAri, kuna eneo kubwa la mamlaka ya EPZA kwa ajili ya viwanda vya uzalishaji kwa ajili ya mauzo ya nje. Hivyo, muwekezaji yoyote mwenye kutaka kuwekeza kwenye bandari, atavutiwa kuwekeza kwenye bandari iliyo karibu na EPZ.
Tatu biashara ya bandari inahitaji kuwa karibu na eneo la biashAra (Business/commerical district) kwa ajili ya kuwezesha transactions mbalimbali. Kwa TZ commercial district ipo Dar es salaam. Hivyo muwekezaji wa bandari ata prefer kwenda bagamoyo iliyopo karibu na Dar kuliko mahala pengine. Lakini pia, Bagamoyo ina potential ya kutengeneza new business district.
Mtwara
Bandari ya Mtwara ipo sorted. Wale investors wa kuchimba gesi wameshaelezea nia yao ya kuitumia bandari ile kama sehemu ya usafirishaji wa gesi. Pia tayari eneo la uzalishaji wa viwanda karibu na bandari limechukuliwa na makampuni yatakayowekeza kwenye viwanda vya kuzalisha mbolea kwa kutumia gesi, na makampuni mengine ya uzalishaji wa cement kama lile la Dangote......hivyo, investor mpya anayekuja sasa, hawezi kuwa na interest na Mtwara kwani tayari kuna strategic investors wa bandari ile.
TANGA
Tanga itaendelezwa soon kwa hesabu za kuitumia ku serve eneo la kaskazini, na pia ni altenative ya Mombassa na pia inahitajika na waganda. Mipango yake ipo. Soon utaona nayo inashughulikiwa.