Ujenzi wa Miradi hii Bagamoyo ni wa Lazima Kiasi Hiki?

....naomba kiongozi yoyote wa juu wa serikali atueleze master plan ya vitu kama hivi iko vipi...yaania if to build anew public university what is the place, if it is to construct a new port,what is the place? au ni kufikiria kuvuka daraja ukishafika hapo darajani? au ni kwa fikra za mkuu aliyepo madarakani? kwa mpango huu naona masuala ya Jamhuri ya Watu wa Tanzania Kusini na Kaskazini inanukia...People's Republic of Souther/Northern Tanzania.
 
On a positive note hapa, kinyume na wengi..nakubali kwamba huenda mipango ya hii miradi haikuwa thoroughly thought through, pengine(allegedly), lakini miradi mingine huenda yenyewe ikawa ni kitovu cha kuchochea maendeleo (stimulus) hivyo inaeza kuleta picha hasi kwa mtu anayeangalia ktk angle ya kiusababishiwa zaidi.

Mindhali Bagamoyo kuna hoteli za kitalii kule na nasikia watu wajenga kule kwa kasi ya ajabu, na mishemishe nyingine zikipamba moto huenda with time mambo yakatengemaa.

Next move ningependa ktk term yake ya pili ya JK ahamishie mishemishe kule Western zone napo kuchangamke. Huku south barabara nadhani kwa kiwango kikubwa imekamilika, no excuse tena kwa ndugu zangu wamakuwa na wamakonde plus wayao.
 
tatizo ninaloliona ni kuwa wale wenyeji watanufaika vipi na vitega uchumi hivi? waliowengi ni watu wa hali ya chini hasa kielimu. otherwise Bagamoyo ni eneo ambalo litawanufaisha wengi ni kama dar es salaam hainufaishi wazalamo pekee bali nchi nzima. hebu nenda pale uone profile za watu wanaofaza kazi/kufanya biashara pale utajua

Maeneo mengi ya Bagamoyo, waungwana wameshajigawia mapema wazawa wanasogezwa mbali sana na hizi sehemu miradi ilipo. Watakaofaidi kwa kiasi kikubwa sio Wakwere kama wengi tunavyodhani.
 
Hatma ya Mji Mkongwe katka yote haya ni nini? Bagamoyo si mahali tu alipotoka Mheshimiwa Rais wetu bali ina mchango mkubwa katika historia yetu. Tusiache mbachao kwa msala........

Amandla......
 
Mungu kwa nini hujapenda kutupa viongozi wenye kuona mbali? Kwa nini huturudishii Nyerere

Hapa ndipo tatizo letu lilipo, this sense of religiosity. Tunamuachia mungu mambo ambayo ni responsibility yetu.Hata hao wanaomuamini mungu wanasema mungu huwasaidia wanaojisaidia.

Huwezi kuwa na population isiyo critical, isiyosoma magazeti (indeed population isiyo na critical/ coherent /educated press) halafu ukamlaumu mungu. I understand to an extent kuilaumu population hii ni blaming the victim, lakini at the same time population hii hata bila ya western sophistication, haiko that naive.Kwa hiyo wakina Mkapa wanapotoa cooked up economic data kuna chance ya wasomi kudanganywa kuliko hawa wananchi wa kawaida.

Which begs the question, kwa nini hawa vote with their interest? Au ndiyo hizi habari za kusubiri kushushiwa kiongozi na mungu?

And all this obsession with Nyerere had better stop, the man is dead and dead men don't talk, let alone lead. Kumtaka Nyerere afufuke ili tuwe na kiongozi bora ni kuwatukana Watanzania wote walio hai. Tunachohitaji ni kubadili uongozi wa sasa na kuweka mpya ulio focused, si miujiza ya agano la kale isiyoyumkinika.
 
wakajenge mbeyaaaa ili kuwe na balance kwenye nchi hii. upendeleo utaendelea hadi lini?bandari sawa, ijengwe bagamoyo itafaidisha watu wote, lakini uwanja wa ndege, ujengwe mbeya au hata dodoma.
 
bara watujengee hapa bwagamoyo, maana maembe,mingonko,viazi,mapera, miwa, samaki nchanga, korosho na mabibo yote tutapeleka ulaya.
 
Fallacy ya argument yako inatokana na kujikita kwake katika averages.

Si kila mtanzania ni "lame", na hata kama wasio lame ni wachache, bado wana wajibu wa kutaka uongozi bora na kutoa ushawishi kwa wale wasiojua/ tegemea uongoi bora.

Kauli yako imekata tamaa. Concept nzima ya maendeleo inatokana na kuelewa limitations za the human condition, lakini kuelewa pia kwamba hata kama tuna limitations, tunaweza kufanya gradual advancement.

Kama si hivyo dunia nzima ingekuwa inalala na kuishi kijima tu.

Ndugu truth hurts,i get it,you are one of the brave ones,YOU are just not enough to CHANGE anything,although you can just be a catalyst for more changes,and this process my friend takes YEARS.SIO KUKURUPUKA,just like you jumped on what i wrote.
 
Ndugu truth hurts,i get it,you are one of the brave ones,YOU are just not enough to CHANGE anything,although you can just be a catalyst for more changes,and this process my friend takes YEARS.SIO KUKURUPUKA,just like you jumped on what i wrote.

Usichoelewa (au kama unaelewa hujaacknowledge fully) ni kwamba a journey of a thousand miles begin with one step. Mimi pia sina matumaini ya chochote muhimu ku change in the immediate future Tanzania, lakini hili halimaanishi nikae kimya nikiona mambo hayaendi sawa.

Na hata kama hatuwezi kuleta "change" in the immediate future, hata kuwapa future historians access ya jinsi watanzania wengine tulivyofikiri tu ni kitu muhimu.Ndiyo maana nakwambia hata kama change is out of hand, ni muhimu tutoe views zetu.

Kuna generation inakua sasa hivi inajifunza mengi hapa.
 
Mimi kwa maoni yangu pesa hizo zingetumika katika kuboresha miundo mbinu ya jiji la Dar. Jiji la Dar sasa hivi lina matatizo makubwa ya uchafu uliokithitiri hadi kushika namba ya tatu katika Afrika na namba nane katika majiji ya dunia yaliyokithiri kwa uchafu.

Dar sasa hivi ikinyesha mvua kubwa kwa dakika chache tu basi bahari ya hindi yote huhamia jijini na mitaa mingi kufurika maji machafu na hata kutishia usalama wa mali na raia wa jiji. Jiji la Dar halina vitendea kazi muhimu katika kusafisha jiji ikiwemo magari ya kubebea takataka.

Magari yanayotumika katika ubebaji taka Dar yanatia aibu sana maana hayana sifa yoyote ya kufanya kazi hiyo. Jiji la Dar halina taa sehemu nyingi sana, hata ile mitaa ambayo miaka ya nyuma ilikuwa na ahueni ya kuwa na taa hapa na pale mingi ya mitaa hiyo sasa hivi ni giza la kutisha.

Kwa hiyo hizi shilingi bilioni 400 kama zingemwaga katika jiji la Dar basi matatizo mengi niliyoyataja hapo juu yangeweza kumalizwa kabisa au kupunguzwa kwa kiasi kikubwa sana.

Sasa leo Kikwete anataka naye aache legacy ya kujenga kwao wakati jiji la Dar likizidi kudidimia. Mwaka 2015 ataingia mwingine naye atataka aache amejenga huko atokako. Hali hii ya kila mvuta kamba kuvutia kwake bila kujali vipaumbele vya nchi kama isipokemewa basi jiji la Dar linaweza kabisa katika miaka michache ijayo likawa ni shida sana kuishi maana miundo mbinu itakuwa katika hali ya kutisha na nchi haitaweza tena kufanya lolote ili kurekebisha hali hiyo kutokkana na gharama kubwa sana ambazo nchi haitaweza kuzimudu.

Jiji la Dar sasa hivi liko kwenye hatarini kama hatua muhimu za kuboresha miundo mbinu ya jiji na mambo mengine mbali mbali jijini basi hakuna wa kulaumiwa ila Viongozi ambao hawajui kabisa kuamua ni vipi ni vipaumbele vya nchi. Sasa hivi kujenga Bagamoyo hakuna umuhimu wowote kwa Watanzania ukilinganisha na kuboresha miundo mbinu ya jiji la Dar ambayo iko katika hali mbaya sana.

Pamoja na Viongozi wa Serikali kudai kwamba Dodoma ndiyo mji mkuu wa Tanzania lakini ukweli ni kwamba mji mkuu wa Tanzania bado ni Dar na jiji linastahili kabisa kupewa kipaumbele ili kuboresha mambo mbali mbali jijini likiwemo la miundo mbinu.
 
Wadau, hii habari si njema hata kidogo na ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu Tanzania. Nachokiona JK anatuachia mfano mbaya sana na ambao unaweza ku;lipeleka Taifa pabaya.

Tujiulize; Je ikiwa miradi hiyo ya Bagamoyo haitakamilika hata anaondoka madarakani ana uhakika gani kama mrtithi wake ataendleza na kukamilisha miradi hiyo? Maana haina tija kwa Taifa zaidi ya ubinafsi tu. Hapa naona fedha nyingi zikipotea (iwapo mirdai hiyo haitakamilika) na kwa kuwa Miradi hiyo haina umuhimu wala tija, ni wazi kuwa Rais ajaye ataitekeleza.

MIRADI HII NI HATARI KWA UMOJA WA TAIFA
Upendeleo huu kwa eneo ambalo tayari kilometa 60 tu pembeni (Yaani Dar) pameendelea vya kutosha (kwa maono ya Kitanzania) ni wazi kuwa itakuwa vigumu sana kwa shuguli za kiuchumi kuhamia Bagamoyo maana imechukua miaka 40 kuifanya Dar iwe jinsi ilivyo sasa, hii miaka 10 ya JK inawezaje kuiweka kando Dar na kuifanya Bagamoyo kuchukua nafasi ya Dar? Kwa nini miradi hii isingepelekwa Dodoma na kuufanya Dodoma kuwa mji Mkuu kikweli?

Nionavyo mimi, kuna hatari huko mbele kila Rais atakayekuja kuiga mfano huo mbya wa JK wa kurundika miradi mikubwa mkoani/WIlayani kwake. Athari yake ni kuwa itafikia mahali Watanzania watataka kila mkoa utoe Rais kwa zamu kitu ambacho ni cha hatari mno maana ni Mkoa gani utakubali kuwa wa mwisho kwenye utaratibu huo wa zamu?

Ee MUNGU, TUKUMBUKE WATU WAKO, TUEPUSHE NA WATAWALA WOTE, WA SASA NA WAJAO WENYE TAMAA YA KULIMBIKIZA KILA KIZURI KWAO NA KUWAACHA WATANZANIA WENGINE NYUMA. AMEN!
 
Maeneo mengi ya Bagamoyo, waungwana wameshajigawia mapema wazawa wanasogezwa mbali sana na hizi sehemu miradi ilipo. Watakaofaidi kwa kiasi kikubwa sio Wakwere kama wengi tunavyodhani.

Mkuu Bob, hivi kama wewe ni Mkwere hivi kweli unataka ushikwe mkono mara ngapi? yaani hii yote haitoshi kukufanya upate mwamko wa kimaendeleo kweli?. Uwekezaji huu ukienda Mbeya au Arusha utalalamika tena?
 
Hivi nyini mlitegemea nini kutoka kwa Jakaya Kikwete mlipomchagua? Yeye anakwenda kupima akili kila mwaka, na akili zake zimefikia kikomo. Mnastaajabu ya Kikwete subirini Kikwete raundi ya pili hapo ndipo mtakapojuta na kukuta mjukuu.
 
Karibu kila jioni utashuhudia msafara wa mkulu ukimpeleka kwao bagamoyo, hivi raisi wa awamu ya nne anafanyia kazi Magogoni na kulala Bagamoyo? Na je hiyo bajeti ya kugharimia huo msafara wa kudumu kwenda bagamoyo imetengwa? Kweli miradi ya marlendeleo ni mizuri ila kama itabuniwa na kuchipushwa kwa mda mfupi kwa ushawishi wa kisiasa nje ya dira ya maendeleo ya taifa ya mda mfupi na mrefu, hayo yanageuka kuwa maangamizi. Mkulu anachofanya hapa ni kudumisha mila ili wakwere wasijesahau kuwa walishamtoa rais wa nchi.
 
Lakini wiki hii nimesoma JK amesema chuo kikuu kingine kama cha UDoM kitajengwa Mara (sina hakika kama ni kupunguza mapanga ya tarime). Sasa ubaya upo wapi kujenga upya bagamoyo ambayo inaonekana kuwa nyuma kimaendeleo lakini ina "potential"?. Si kweli bagamoyo watu wakubwa tu ndio wamejichukulia viwanja. Nakumbuka Halmashauri ya Bagamoyo ilitangaza na watu wakanunua viwanja kwa bei ya kawaida-Low density ilikuwa shs 300,000/=.
 
Mi naona ajenge tu. Kama kuna watu wenye kumbukumbu wacheki uwiano wa Bagamoyo na wakazi wengine maeneo hayo, na uwiano wa wanaomiliki huko. Kisha waje wacheki takwimu hizo hizo baada ya hiyo miradi kukamilika. La kuvunda halina ubani, kama ni wa kuvaa msuli na kuchez bao, hata upewe mbingu utabaki na msuli tu...
 
Watu wanasema oooooh, wachaga wakipewa nchi watapendelea kwao. Kikwete naye mchaga, sio?
 
Naona kwa sera hizi kila mkoa utoe mgombea uraisi maana sera , za cha chetu tawala (kitukufuu) ndio zinatuelekeza huko au mwishowe yue kama Yugoslavia tuna maraisi 26 wanaoongoza alternatively kila baada ya miaka miwili tunabadili, yakitushinda hayo tugawanyike.
 
hey hiyo nayo kali kichuguu naona kama bongo vile.labda tufikirie kila wilaya kuwa na raisi wake badala ya kusubiri zamu ya uraisi maana miaka kumi mingi sana eti.
 
Back
Top Bottom