Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,264
- 105,428
Lakini jamani tutazame upande mwingine wa Shilingi. Hii miradi yote imefanyiwa feasibility study na kuonekanaa inafaa na italeta tija. Sasa ni sawa kusema hao wataalam hawana uwezo wa kutosha?
Sidhani kama Rais akishauriwa na wataalam kwamba mradi haufai yeye akaendelea nao kwa sababu za kisiasa ama sivyo itakuwa yale ya "Alex stewwart" ya viongozi waliopita.
Mbona barabara na kiwanja cha ndege kitajengwa Serengeti?
Tujaribu kwenda ndani zaidi katika uchambuzi kabla ya kutoa hoja.
Feasibility study gani? Imefanywa na kampuni gani? Imeonyeshaje kwamba Bagamoyo ndiyo sehemu nzuri kabisa ya kutumia fedha zetu chache za kigeni? Utatuhakikishiaje kwamba hizi projects hazijapita kwa pressure ya top down? Kwamba mkulu anaagiza kiwanja cha ndege na bandari vijengwe kwanza, halafu feasibility study hata kama inakuja inachongwa ku fit matakwa ya mkulu?
Tumetumia hela kibao kuhamiha "mji mkuu" kwenda Dodoma, miaka kibao baadaye wizara zote, mabalozi wote na serikali yote kwa ujumla iko Dar bado.Hata hilo bunge lililohamia Dodoma wabunge wake kibao bado wako Dar. Hili halijatufundisha?
Katika wakati huu wa global economic crises, tunapata wapi confidence ya kuweka mihela kibao katika projects kubwa hizi? Historia ya kukuza miji kwa kumwaga fedha imejaa matokeo ya kushindwa, kuanzia Brasilia, Canberra mpaka Dodoma. Binafsi napenda zaidi mipango ya miji inayoipa miji organic growth, from bottom to top. Hizi habari za top down zimewashinda Waarabu na hela zao, zimewashinda Wa South Korea na teknolojia yao, other than a bottomless pit for our money, hizi pprojects hazina kazi nyingine.
While one can make a coherent case that the Dar business hub needs to be decentralized, and Bagamoyo may be the place to start, I feel that not enough justification is given.In addition tayari tuna bandari na viwanja vya ndege vinavyohitaji kuboreshwa. Tunakuwa sawa na yule mtu maskini lakini asiyetaka kufua nguo, nguo ikichafuka yeye anataka kununua nguo mpya tu. Hii si akili.
To make matters worse, projects zinaonekana kutolewa kwa sababu ya nasaba ya Kikwete kuwa Bagamoyo