Ujenzi wa Miradi hii Bagamoyo ni wa Lazima Kiasi Hiki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujenzi wa Miradi hii Bagamoyo ni wa Lazima Kiasi Hiki?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kichuguu, Jul 5, 2010.

 1. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #1
  Jul 5, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  HATUA ya serikali kuelekeza miradi mikubwa zaidi ya sita ikiwemo ujenzi wa bandari na uwanja wa ndege wa kimatiafa wilayani Bagamoyo, alikozaliwa Rais Jakaya Kikwete imepingwa na wapinzani wakisema uamuzi huo ni ufujaji wa fedha za walipa kodi.

  Mjadala huo umeibuka wakati serikali imeshaanza mkakati wa kutekeleza azma ya kuigeuza
  Bagamoyo kuwa kitovu kikuu cha biashara na uchumi nchini kwa kujenga miradi mikubwa mbalimbali wilayani humo ikiwemo bandari, uwanja wa ndege, Chuo Kikuu, Soko la Kimataifa, barabara kuu kwenda mikoa ya Kanda ya Kaskazini, kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na viwanda mbalimbali.

  Juni 25, mwaka huu Rais Kikwete, alizindua eneo la uwekezaji lenye ukubwa wa ekari 300 ambapo wawekezaji wa Kampuni ya Kamal kutoka nchini India wameanza kutekeleza mradi wa kujenga viwanda na maduka wenye thamani ya Sh400 bilioni katika eneo Zinga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.


  Kufuatia utekelezaji huo kwa nyakati tofauti wapinzani walisema mpango huo umeibuka bila kuainishwa popote ikiwemo katika Dira ya Taifa ya Maendeleo (Visioni 2020/25).


  Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed alikosoa mradi huo akisema: "Ni jambo baya zaidi kuanzisha miradi mipya huku ya zamani ikifa. Mpango huo wa serikali ni mbaya, 'ni missallocation' (mgawanyo mbaya) ya miradi. Huwezi kuacha uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam ukiwa haina ufanisi kwa kutosha, ukajenga uwanja mwingine mkubwa Bagamoyo".

  Hamad aliongeza: "Tunachojua miradi kama hiyo ilitakiwa kuonyeshwa katika Dira ya Maendeleo ya 2020/25 na Mkakati wa Mkukuta, lakini hiyo haimo humo. Kibaya zaidi bajeti yetu inategemea wafadhili".


  Hamad Rashid alidai kuwa serikali imeshindwa kutumia msaada wa fedha zilizotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya kuboresha utawala bora na mfumo wa mahakama badala yake ikatumia asilimia 25 tu wakati miundombimu ya Idara ya Mahakama inahitaji kuboreshwa.


  "Serikali ingeweka mkazo kwa miradi iliyopo, huwezi kujenga bandari Bagamoyo wakati ya Dar utendaji wake ni mbovu na bandari za Tanga, Mtwara zinakufa. Huwezi kujenga chuo kikuu kama cha UDOM Bagamoyo na kuacha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinakufa, hili ni tatizo", alisema Hamad.


  Kauli hiyo ya Hamad inakuja wakati kuna taarifa kwamba, mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege unatarajiwa kuanza wiki ijayo huku ule wa bandari ukitarajiwa kuanza mwezi mmoja ujao.

  Akizungumza na Mwananchi Jumapili, kuhusu miradi hiyo jumamosi iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Magessa Mulongo alisema ujenzi wa uwanja wa ndege ulitarajiwa kuanza wiki hii na bandari mwezi Julai.

  "Vipo vinafanyika, kwa ujumla mambo yanakwenda vizuri. Hatua za awali za uwanja wa ndege wa kimataifa tunatarajia kuanza wiki ijayo (wiki hii), bandari mwezi ujao (Julai)," alisema Magessa.

  Alisema kuwa tayari kiwanja cha kujenga Chuo Kikuu kimepatikana eneo la Msakese na kwamba ujenzi wa barabara kati ya Saadani na Tanga upo mbioni.

  Naye Mwenyekiti wa NCRR-Mageuzi James Mbatia, alikosoa miradi hiyo akisema ni kupoteza fedha za walipa kodi na kuonya kuwa Watanzania wasifanywe wajinga ndani ya nchi yao.

  Mbatia alifafanua kuwa kujengwa uwanja wa ndege na bandari nyingine Bagamoyo umbali wa kilometa 65 kutoka Dar es Salaam ni kuchezea akili za Watanzania na kwamba, miradi hiyo inakofanywa kwa malengo ya kisiasa ya muda mfupi bila kuangalia mbali kwa manufaa ya taifa.

  "Hii ni 'wastage' (matumizi mabaya) ya fedha za walipa kodi. Hapa serikali inachezea akili za Watanzania. Kujenga bandari Bagamoyo kilometa 65 toka Dar ni akili ya wapi?" Alihoji Mbatia.

  Mbatia ambaye alihitimu hivi karibuni taaluma ya bandari nchini Ujerumani, alisema serikali imepanga kufanya hayo huku ikishindwa kutumia ukanda wa bahari wenye eneo la kilometa 1,424 na kwamba, bandari ya Dar es Salaam haimo hata miongoni mwa bandari 100 bora duniani.

  "Tufikiri chanya, tusifanye kienyeji na tusifanye mambo ya kitaalam kwa malengo ya kisiasa, tuache ubabaishaji," alisema.

  Mwenyekiti huyo wa NCCR alisisitiza kuwa jambo muhimu kwa serikali ni kuimarisha na kuboresha utendaji wa viwanja vya ndege na bandari zilizopo, pamoja na kujenga bandari kavu eneo la Kibaha ili kusaidia ufanisi kwenye badari ya Dar es Salaam.


  Uamuzi wa Rais Kikwete kujenga miraadi hiyo mikubwa katika mkoa na wilaya aliyotoka ni tofauti na ilivyokuwa kwa marais wa Tanzania waliomtangulia.

  Katika uongozi wake wa awamu ya kwanza mbali na kutawala kwa miaka 25, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hakuwahi kujenga hata barabara ya lami katika wilaya aliyotoka (Musoma Vijijini).

  Hata rais awamu ya tatu Benjamin Mkapa kwa miaka kumi ya madaraka yake, hakuweka mradi wowote mkubwa mkoa au katika wilaya aliyotoka.

   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hiyo miundombinu ingekuwa inajengwa kaskazini watu wangepiga kelele????????

  Ni swali tu wadau, nothing personal.
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  mwacheni ajenge kwao.
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Ubongo mgando.
   
 5. B

  Bobby JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Lumbe nahisi hujauntendea haki huu ubongo, nadhani tunapaswa tuuite ubongo mgandomgando. Yaani hivi vituko vingine jamani mbona soni? Kwanini tusiborehe hii air strip ya Dar? Hili linanikumbusha zile nyumba za NHC Chalinze, nimepita juzi zimeanza kuwa magofu. Hivi ili hii nchi inendelee yote inabidi kila mtu awe rais ili aendeleze kwake? That means tunahitaji miaka milioni 40 ili tuendeleee wandugu hii mbona noma?
   
 6. mujusi

  mujusi JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 237
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Lakini jamani tutazame upande mwingine wa Shilingi. Hii miradi yote imefanyiwa feasibility study na kuonekanaa inafaa na italeta tija. Sasa ni sawa kusema hao wataalam hawana uwezo wa kutosha?
  Sidhani kama Rais akishauriwa na wataalam kwamba mradi haufai yeye akaendelea nao kwa sababu za kisiasa ama sivyo itakuwa yale ya "Alex stewwart" ya viongozi waliopita.
  Mbona barabara na kiwanja cha ndege kitajengwa Serengeti?
  Tujaribu kwenda ndani zaidi katika uchambuzi kabla ya kutoa hoja.
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kuna mada fulani tulikuwa tukijadili kipindi fulani hapa jamvini, nikajaribu kuhoji ni criteria gani zinatumika kuamua miradi ya maendeleo, hususan ile inayokula ela nyingi? Je kuna masterplan?? Kwa sababu inaonekana kama mwanasiasa mwenye nguvu ndiye anaallocate miradi na si vinginevo, (lobbying), wengi kwene mada ile (akiwemo mbunge kijana 'machachari') wakasema ohh lobbying ipo hata US na Europe, mie nikakaa kimya huku nikisema kimoyomoyo 'Eeh Kumbe TWAFWA !! '.

  Walakini punde si punde kwene thread hiihii watu walewale akina Sikonge watakuja hapa kupinga huu mradi wa JK...
   
 8. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  La uwanja wa ndege halina shida.
  Bandari hapa ndo penye utata mkubwa,kwani katika best ports in the world Mtwara is among them,ila tunatumia theluthi moja tu ya eneo katika bandari hiyo.
  Hiivyo ningeona wamefanza la maana kama wangeenda kuiboresha ili tule vichwa kwa Malawi Zambia na hat Congo pia.
   
 9. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mi sitoki huko Bwagamoyo lakini nadhani hii miradi ni mizuri na inastahili kujengwa. Bandari ya Mtwara imeshaanza kukua kutokana na uchimbaji wa mafuta na gesi. Bandari ya Dar iko eneo baya na sidhani kama inaweza kupanuliwa zaidi. Uwanja wa ndege wa Dar uko eneo baya sidhani kama unaweza kupanuliwa sana. Naungana na mkuu mmoja aliesema kwamba hii miradi ingejengwa kaskazini watu wengeona ni sawa...
   
 10. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Uwanja wa ndege mpya ulishatafutiwa eneo zamani kabla muungwana hajaingia madarakani. Eneo lilishatengwa wilaya ya Mkuranga, inakuwaje ahamishie Bagamoyo? kwao for that matter! sasa huu ni ulimbukeni. Jamani Nyerere angetaka kupeleka vyote Musoma nchi ingekuwaje? Muraaa, ri uwanja riko kwetu muraa... Maslahi ya taifa yaangaliwe, huo sasa ni ubinafsi...watu wataanza kuchagua kiongozi kikanda ili miradi iletwe nyumbani. Hata huo Bwagamoyo internattional Airport itahamishwa na kupelekwa BK...oooh...mmh Kamachumu International Airport.....awamu nyingine kuleee Tuykuyu.....awamu nyingine kuleee Zenj...Kibandamaiti International Airport. Watanzania tuige mwalimu alivyo allocate rersources.
   
 11. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu hivi Muranga na Bwagamoyo viko ktk mkoa gani??
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Mmoja lakini si kwao na mkuu.....ni kama Upareni na Uchagani....Mramba hajawaki kupeleka lami upareni
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Niliwahi kuongelea suala la Bagamoyo kupendelewa kipindi cha Muungwana baadhi ya wanajamvi walinipinga sana lakini leo wamebaini nilikuwa sahihi.

  kuendeleza eneo analotoka rais au mkuu wa nchi imekuwa ni sehemu ya tabia ya watawala wengi wa nchi za Afrika.Rais wa zamani wa Zaire [Congo Kinshasa] hakubaki nyuma kufanya upuuzi wa kujenga mji alikozaliwa Gbadolite uwanja wa ndege wa kimataifa,ikulu na mambo mengi yaliyotafuana hazina ya nchi ya Zaire wakati huo,Rais wa zamani wa kenya mzee D Arap Moi alitenda dhambi ile ile ya kutumia vibaya hazina ya kenya kujenga alikozaliwa.Kufuru nyingine ilifanywa na Rais wa zamani wa Ivory Coast Bwana Felex H Boigny alitumia vibaya hazina ya taifa lake kujenge kanisa kubwa la Yamoussoukro,uwanja wa ndege,Reli,Barabara za kisasa na nk.

  Inashangaza kidogo kuona Tanzania iliyopata uhuru wake mwaka 1961 bado inaongozwa na kiongozi mwenye mawazo ya akina Felex Boigny,Daniel A Moi,Omari Bongo na Mobutu Seseseko.Mbaya zaidi ni kuona mfumo wetu wa siasa unaruhusu haya kutokea.Miradi yote inayokimbizwa Bwagamoyo ina hatari ya kufa wakati rais wa sasa atakapoondoka madarakani.

  Mchezo huu mchafu ukiachiwa kuendelea kushamiri ipo hatari nyingine itakayoinyemelea Tanzania siku za usoni.Tutakuwa tunachagua viongozi wataokuwa wanatazama zaidi sehemu walipo toka kwanza badala ya kuitazama Tanzania.
   
 14. C

  Chuma JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  By the way itawasaidia wananchi wote wa Tanzania...!!! kama ikifanikiwa hio Miradi...!!!
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hii ni zawadi ya JK kwa wakwere wenzake, Mkapa yeye aliwapatia daraja la mto rufiji na barabara, hapa ndipo umuhimu wa kuwa serikali ya majimbo unapokuja. Yaani rasilimali zinatoka mikoa mingine zinaenda kuendeleza mikoa mingine. Kama mimi ningekuwa ni mpiga kura pekee wa Tanzania basi ningemwambia JK aende akaombe kura Bagamoyo, si ndiko anakotekeleza ahadi ya maisha bora kwa kila Mbagamoyo!
   
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Binafsi sioni tatizo kabisa kujengwa kwa bandari Bagamoyo kwa sababu ya pale Dar imewashinda, nadhani wote tunakumbuka pia jinsi watu wanavyoteseka na foleni barabara ya Mandela kwa misemitrela kutoka au kwenda bandarini.

  Na pia mizigo inayoenda sehemu kama Rwanda, Burundi na sehemu ya DRC kutumia bandari Mtwara ni mbali sana, angalieni Tanzania map. I think this is very clear.

  Ila hili la uwanja wa ndege I say NO please. Waache tu ukajengwe huko mkuranga unless watoe sababu za kueleweka.

  Lakini pia nahisi mikoa ya pwani siku zote huwa wanalalamika kuwa imeachwa nyuma kimaendeleo kwa makusudi kwani ndo ilikuwa ya kwanza kabisa kupata maendeleo lakini viongozi waungwana walipokuja wakaichinjilia baharini ila damu yao ilionekana labda ndo maana Muungwana aliopo madarakani ameamua angalau kuikumbuka kidogo.

  Kwa wale mliofika Pwani Tanga na kadhalika nimashahidi, mfano mkoa wa Tanga umepangika vizuri sana lakini maskini watu wa hapo wamechoka ile mbaya, mida yote utaona vibaraka shehe vingi kichwani wakiendesha baiskeli huku uchumi waliokuwa wanajivunia kama vile viwanda na dandari vikiwa either vimekufa or viko taabani ICU.

  ILa mikoa ya kati na magharibi ndo kabisa haijapata muungwana labda tusubiri mzee Malecela achukue ofisi 2015 labda wataweza ona mwezi na wao pia.
   
 17. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #17
  Jul 5, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mimi sina problem na kujengwa miradi hii bwagamoyo, my concern ni why wamewalipa na kuwahamisha watu kipawa while walikua na mpango wa kujenga kaluwanja bwagamoyo
   
 18. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #18
  Jul 5, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  1. Barabara through Bagamoyo kutokea msata ni muhimu sana kwani itapunguza fujo kwenye barabara ya Morogoro, watu wa kazkazini watapita kiurahisi badala ya kuzunguka chalinze. big up

  2. Bandari ya Bagamoyo ni muhimu sana kwani bandari ya dar haiwezi kupanuliwa zaidi na si natural habour ni ya kuchimba tu. na itaserve kama inavyoserve bandari ya dar. big up

  3. Kuhusu uwanja wa ndege sina la kusema

  4. Chuo kikuu. big up

  tatizo ninaloliona ni kuwa wale wenyeji watanufaika vipi na vitega uchumi hivi? waliowengi ni watu wa hali ya chini hasa kielimu. otherwise Bagamoyo ni eneo ambalo litawanufaisha wengi ni kama dar es salaam hainufaishi wazalamo pekee bali nchi nzima. hebu nenda pale uone profile za watu wanaofaza kazi/kufanya biashara pale utajua
   
 19. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #19
  Jul 5, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  hilo la bandari ni upuuzi mtupu, Bagamoyo hipo katikati ya bandari mbili ya Tanzga na Dar, sasa unaweka bandari nyingine ya nini katikakti, cha muhimu ilikuwa ni kuipanua na kuiboresha ile ya Tanga tu
   
 20. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hakuna sababu yoyote ya maana bali ni ulimbukeni wa Jakaya Kikwete tu.
   
Loading...