Ujenzi wa "Mfumo Magufuli", hatari na janga kwa taifa kuliko Rais Magufuli mwenyewe

Mimi nimeishi kanisani (katoliki)kwa miaka isiyopungua 15 nikatoka kwa hiari yangu # kifupi msiwategemee viongozi wa kidini kuwateteeni kwani ndani ya kanisa katoliki wanaamimi sana katika mateso,kanisa katoliki linahubiri mateso ya Kristo ,hivyo tunapompata kiongozi wa nchi kama Jiwe akiwatesa wananchi katika maeneo mbalimbali basi hii ni habari njema kwa kanisa katoliki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu acha uongo, kanisa katoliki ndilo dhehebu pekee linalohubiri upendo kama ulitoka baada ya kutongoza wanakwaya nenda tu. Mtu mbaya anayefumbia macho uovu kea sababu anatoka upande wetu ni huyu anayejiita MAPENGO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi pia nimeliona hili. Yaani kwake yeye hakuna hata mmoja mwenye jema! Kila zama kwake ni mbaya? Basi labda ije ghalka ndio labda nafsi yake inaweza ridhika.
Nimesoma lakini nilipofika sehemu unaleta utovu wa nidhamu kwa mzee Mwinyi aliyetufungua minyororo ya sera za kimasikini za ujamaa, mtu aliyesaidia tuache kuvaa midabwada na foleni za duka la Kaya, nikasema mleta mada hajui what is he talking about!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na bado tutasikia mengi sana kutoka kwenu wachumia tumbo mwaka huu,kwani nia yenu kubwa ni kumkatisha tamaa huyu mzee wetu kwa maendeleo anayotufanyia,hakuna zuri kwenu vibaraka ,JPM songa mbele sisi wanyonge tupo bega kwa bega nawe
Afadhali umepewa like mbili tu na watu dizaini yako. Unaona kabisa hadi sasa wameamua kufukuza kampuni zote za ndege ili yabaki mapangaboi harafu bado unaona hayo ndiyo maendeleo! Maendeleo yasio na ushindani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unacho kijua wewe kichwani mwako kuwa ukitongoza mwanakwaya unaachishwa ! Siwezi argue na mtu ambaye ni lay person tu katika mambo ya kanisa! The very big problem you know nothing about Catholic church na mifumo yao ya kiutawala ! So kaa kimya
Ndugu acha uongo, kanisa katoliki ndilo dhehebu pekee linalohubiri upendo kama ulitoka baada ya kutongoza wanakwaya nenda tu. Mtu mbaya anayefumbia macho uovu kea sababu anatoka upande wetu ni huyu anayejiita MAPENGO

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajamvi wenzangu wa The Home of Great Thinkers niwasalimu. kwanza nichukue nafasi hii kuwaaga wale wadarisalama maana sisi wenzenu watumishi wa umma kikokotoo cha kutuhamishia Dodoma ndio kimekamilika mwaka huu hivyo wachache tuliobaki kumpa joto mzee ndio tunapaki mabegi tayari kwa safari muda wowote atakapotoa kauli.

tunapoanza mwaka wa 2019 nataka niwaachie mada ya kutafakari kuhusu Rais Magufuli. leo sitataka kujadili mambo yaliyo nyuma ya matukio na maneno yake ambayo wakati mwingine yako kama bongo muvi bali nataka mumtazame magufuli kama mfumo na hatari inayoikumba nchi yetu sasa na huko tuendako kutokana na mfumo magufuli. kama kawaida, nisome ukiwa na fikra huru ili unielewe.

kama mbavyo Mwalimu Nyerere amewahi kutuambia huko nyuma, katiba yetu imempa rais wa nchi mamlaka ya kifalme. yule mzee wa kikwere pale msoga asiyetuletea janga kupitia magufuli aliwahi kusema katiba imempa mamlaka makubwa sana hadi anaogopa kuyatumia. ukubwa wa mamlaka haya una mambo mengi lakini kubwa ya yote ni jinsi ambavyo yanampa rais uwezo wa kujenga mifumo mingi ambayo inaweza kuwa na faida au hasara na ikaleta kicheko au mamumivu kwa wananchi kwa muda mrefu. nitoe mifamo michache.

nguvu ya mamlaka ya rais ndio ilimfanya Mwalimu Nyerere aheshimiwe na fikra zake kuchukulia kama vile ni maandiko ya dini hadi leo. urasi ulimfanya awe wa kipekee. pia ndio ilimfanya aweze kutekeleza kila mpango alituletea hata kama ulikua na maumvi na bado tukaona ni sawa tu. alituletea azimio la Arusha, vijiji vya ujamaa, kilimo cha kufa na kupona, na mengine mengi na tulitekeleza. hii ni kwa sababu nguvu aliyokua nayo ilimtisha kila mtu. nguvu ya urais wake ilimrahisishia kujenga mfumo Nyerere wa taifa la watu wapole, wenye utu, na wenye kiburi cha mdomoni na maneno mengi lakini wanyonge kifikra mbele ya mataifa mengine.

mzee Mwinyi alipokuja na mama Siti wake nao wakaja na yao. mamlaka ya urais ikamfanya kutekeleza sera zake tofauti na za Mwalimu na kuacha mambo mengi yakaenda ovyoovyo ikiwa ni pamoja na mama Siti kuwa na mamlaka kama vile ndio msaidizi wa rais kikatiba. hakuna aliyeweza kupingana na waliyokua wanayafanya. matokeo yake nchi ikawa na mfumo wa ovyo, rushwa ikatapaa na kuzidi, siasa ikawa biashara, na mengine mengi. wale wazee wenzangu mutakumbuka maisha yalivyokua na madhara mfumo mwinyi ulioendelea hata baada ya kuondoka kwake.

ngumu hiyohiyo aliingia nayo mzee mkapa na sera ya uwazi na ukweli. pamoja na mambo mengine mazuri aliyofanya kujenga uchumi na taasisi, ilimwezesha kuuza mashirika ya umma ovyoovyo, kuuza nyumba za serikali kishikaji hadi magufuli akahonga zingine kwa ndugu na mahawara zake, na akaruhusu baadhi ya watu wakawa na nguvu kubwa sana kiuchumi. huyu akatuachia mfumo mkapa ambapo ukata ulionekana sehemu ya maisha huku kundi dogo likifaidi.

mzee wa kikwere alipokuja na mfumo wake wa wanamtandao, alitumia mamlaka makubwa ya kiti cha urais kuishi kifahari yeye na familia yake na kufanya kila alichotaka. tutakumbuka alivyoanza uraisi kwa starehe za safari ya kuzunguka dunia kwa kile alichoita kujitambulisha na akaendelea hivyo kwa miaka kumi hadi mwezi wa mwisho wa urais wake akiendelea na ziara za alichokiita kuaga nchi washirika utadhani walimchagua wao. madaraka na utajiri wa nchi ulioachwa na mkapa akafanya vikawa vya kugawana na washikaji wake. akajenga mfumo wa watumishi wa umma kula bata kwa safari za kila siku na kila mahali. kwa urais wake akaruhusu wala rushwa wengi wao wakiwa ni washikaji wake na waliomweka madarani wakafanya wapendavyo huku yeye akitabasamu. tunajua ni skendo ngapi za wizi kaziacha. kama vile haitoshi, familia yake ikawa ya kifalme na tukashuhudia watoto wake wakitoa kauli za ajabu kabisa hadi siku za mwisho za uongozi wake na hawakua na hofu. akatuachia nchi yenye mfumo kikwete ambao ni mdebwedo, wa kizembe, na dhaifu kama ambavyo wapinzani wake walivyokua wanamwita. mbaya akataka kutuamulia nani awe rais ili kuendeleza mfumo kikwete na matokeo yake ndio yakalipelekea taifa kupata janga kubwa la rais ambaye hadi sasa anaendesha nchi kikatili na kama familia yake. yako baadhi ya mambo machache mazuri ya kuenzi kama ilivyo kwa waliomtangulia aliyoyaacha lakini sio sehemu ya mada hii kuyajadili kwa sababu yanafunikwa na janga alilotusababishia.

nimekupa mifano hiyo ili ikusaidie kuelewa ninachamaanisha kwa kumtazama Magufuli kama mfumo na madhara yake kwa taifa. hao wote waliotangulia walitumia nguvu ya mamlaka ya urais kujenga mifumo ambayo kwa namna moja ua nyingine iliboresha hali ya maisha yetu na wakati mwingine ikatuletea matatizo ambayo hadi sasa yanatuandama. hata hivyo uharibifu wao ni ngumu kuufananisha na ubaya wa mfumo magufuli.

sasa tumfazame ujenzi wa mfumo magufuli. kwa kuwa lengo kuu ni kuitahadarisha nchi juu ya madhara ya Mfumo Magufuli nijikite kwenye yale ambayo nataka tuyatafakari na yatusaidie kuamua mustakabali wetu juu ya uongozi wake huko tuendako. yale machache mazuri ya kumsifia niwaachie waliopewa jukumu la kusifia na kuyatumia hayo kama kivuli cha kufunika ujanga unaotukabili. nitaongea kwa kifupi ili nisikuchoshe.

matendo na maneno ya magufuli tangu aingine kwenye urais yanajulikana. ni mtu anayejitahidi sana kujionesha ni mwema lakini ndani yake akiwa na roho mbaya, katili, na yenye ushetani mwingi. tumeshuhudia chuki ya ajabu toka kwake kwa wale anaowaona kama adui au wapinzani wake. tumeona vifo na tumeona uminywaji mkubwa wa haki na uhuru kupitia matamko, amri, sheria na kanuni mbalimbali. kwa mara ya kwanza tumeona rais ambaye anafurahi majeshi kuliko raia na ambaye haoni aibu kuwasifia hadharani hata wanapotenda kinyume na katiba. kwa mara ya kwanza kwenye historia ya nchi tunaona rais ambaye hajali maadili na utukufu wa utumishi wa uma. kateua watu wa ajabu kuwa viongozi na kawapa amri na mamlaka ya kukandamiza wengine. ni rais anayewapa zawadi watenda makosa na anayepandisha vyeo wala rushwa, wakatili na wasiotii sheria. tunaona rais ambaye ana chuki ya kutisha kwa vyama vya upinzani na kaamua kuongoza zoezi la rushwa ya kununua wapinzani wawe upande wake. tuna rais anayechukia haki na demokrasia kupita kiasi. kwa mara ya kwanza taifa linaongozwa na rais ambaye halijawahi kumwona akijitambulisha na familia yake. taifa halijui watoto wake, watoto hawana ujasiri wa kujitambulisha na sina hakika kama wana ufahari na urais wa baba yao, na mke wake siku zote ni mnyonge. tuna rais anayejisifia hadharani kwamba watoto wake hawafanyi hata sherehe za harusi kwa amri zake na anataka tuone ni sawa.

bila shaka umeona mfumo magufuli, ujenzi wake na una sifa gani. mzee huyu anatujengea nchi ya mfumo wa kikatili. mfumo unaonyima watu haki zao kwa amri za kijinga. mfumo wa mtu kutokua na hakika ya kuishi maana muda wowote unaweza kuuawa kwa kwa sababu yoyote ile. mfumo ambao watu waovu walio karibu na rais wako salama na wanaweza kufanya lolote na maovu yao kutakatishwa. mfumo magufuli ndio umezaa viongozi aina ya Makonda, Ali Happi, Jeri Muro, Sabaya, Mnyeti, kamanda Siro, Mwambosasa, na wengine kama wao. mfumo wenye jeshi la polisi katili kwa raia na usalama wa taifa kuwa chombo cha mauaji na mateso ya raia. mfumo usiojali maisha na uhai . mfumo unaodharau katiba na sheria za nchi. mfumo wa watu wasiokua na fikra huru bali wako radhi kusifia kila kauli na matendo ya rais hata kama yeye mwenyewe haamini katika hayo, mfumo wa chama cha mapinduzi cha mazuzu wasio na uwezo wa kuhoji wala kuuliza bali kufuata maagizo ya rais. mfumo ambao umewafanya wasomi na wanataalamu kukosa uhuru wa kutoa mawazo ya kisomi kwa uhuru kwa kuogopa kupingana na rais maana hajulikana anasimamia nini. mfumo uliotuondolea uhuru tuliokua nao wa kujadili siasa na viongozi kwa uhuru na mtu yoyote mahali popote bila kuogopa kuwa unawindwa. mfumo uliowateka viongozi wetu wa kiimani na kuwafanya kuwa wanafiki bila woga. mfumo wa chaguzi kukosa maana na kura kuporwa mchana na watu kumwaga damu.

watanzania, hii ndio hatari inayotukabili. tunaohoji kauli, matendo na uongozi wa magufuli haya ndio tunayotaka watu wayaone. yeye mwenyewe ni janga na tishio lakini kinachotisha kupitiliza ni mfumo magufuli anaotujengea. mfumo unachukua muda kujengwa na kuimarika na unachukua muda kuuvunja na kuubadilisha. ndio maana hadi leo tunateseka na baadhi ya mifumo tuliyoachiwa na Nyerere. pia magufuli bado anapambana na mfumo kikwete. mfumo huu wa kikatili utaitesa Tanzania kwa miaka mingi sana baada ya urais wa magufuli hasa iwapo tutamruhusu kuendelea kuujenga kwa miaka 10. nchi zilizoongozwa na viongozi wakatili zimeteseka kwa miaka mingi sana kuvunja mfumo huo. mfumo wa mauaji uliojengwa na chama cha KANU chini ya Moi unaitesa Kenya hadi sasa. wakenya wamendelea kuuana na kuchukiana hadi leo. ni kawaida kupigwa risasi, kupotea au kuuawa njiani. uganda wanateseka na mfumo wa iddi amini hadi leo. ukatili ndio unaendesha nchi na umetamalaki kwenye majeshi.

watanzania, magufuli ni janga kwa nchi yetu maana anatujengea mfumo magufuli ambao ni hatari na wa kutisha kuliko magufuli mwenyewe . tuna nafasi ya kuukataa mfumo huu na kuharibu ujenzi wake kabla hatujachelewa. tusidanganyike na miradi ya ujenzi na maamuzi ya ajabuajabu kama ya kununua ndege kama nyanya sokoni. haya ni mambo madogo sana ukilinganisha na athari ya mfumo magufuli.

wekeni kumbukumbu ya ujumbe huu kwa matumizi ya baadaye

#MfumoMagufuliNiJanga

tukutane Dodoma
Vipi bado unajichoma sindano za kutoka sober house?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukikosa aibu ni sawa na mbwa wanaopandana mbele ya kadamnasi. Huna tofauti

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumtaka hayawani aishi kama binadamu ni kukosa akili.
Mbona haumvalishi chupi na gauni au suruali huyo mbwa ili kuficha tupu zake?
Si unataka aishi kama binadamu?

Kilicho cha aibu ktk jamii yako sio aibu kwa jamii nyingine. Aibu au haya ni subjective, ninaweza kuona haya kula hadharani lakini kwa mwingine haoni haya tena anaona anaekula ndani kwa kujificha ni mchoyo.

Wewe unae mcheka mtu anaekula hadharani kesho unaenda shuleni wanakofunza maadili unakula hadharani au harusini unakula hadharani na waalimu wako wa nidhamu?!!!
 
Mkurya wa dar kapewa hongo ya teuzi na cheo sababu ya kuwatukana chadema na Mbowe kama shukrani yake.
Nimekuelewa sana mkuu, kwa bahati mbaya ni wachache sana watasoma kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Mfumo katili umeshaanza kutamalaki, uliowataja Makonda, Ally Happy, Mambosasa ni kielelezo tosha. Wanaokiuka maadili na kuchukia sheria na katiba wanaonekana ndo watu sahihi. Taifa limepotea lakini tufanye nini? Ni wajibu wetu waona mbali to put counteracting forces to avert the status quo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unacho kijua wewe kichwani mwako kuwa ukitongoza mwanakwaya unaachishwa ! Siwezi argue na mtu ambaye ni lay person tu katika mambo ya kanisa! The very big problem you know nothing about Catholic church na mifumo yao ya kiutawala ! So kaa kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe puss.. y usiniharibie siku. Kama uliondoka kanisa Katoliki sie bado tumo na hatutegemei kutoka. Narudia hakuna kanisa linalohubiri upendo kama Kanisa katoliki au RC kwa kifupi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulipokuwa tunawakataza muache zile dua zenu Za kutaka Rais Dikteta 2005-2015 mlituona hatuna akili!

Mlitaka Rais Dikteta wa kuruhusu Michakato yote ya Kikatiba Na uhuru wa maoni?

Next time kabla ya kuanza Maombi Muwe Mnajua vyema sifa Za mnachokiomba

Ninavyojua mimi hata siku moja hakuna mtu aliyeomba dictator tu bali siku zote wakati wa awamu ya nne watu walikuwa wanaomba 'benevolent dictator'; siyo 'ruthless dictator. Mfano wa benevolent dictator ni Nyerere mwenyewe.
 
Contradictions:
Mzee Kikwete analaumiwa kwenye Uzi huu kwa kuifanya familia yake iishi kifalme na watoto wakawa na kauli hadi siku za mwisho wa utawala wa baba yao.
Ndani ya Uzi huo huo, unamkosoa Rais JPM kwa kutoitambulisha familia yake, kuozesha wanawe bila sherehe n.k.
Nashindwa kuelewa, tusimamie lipi ikiwa ulichokikosoa kwenye utawala uliopita, kimefanywa tofauti awamu hii lakini pia hujaridhika nacho.
Tuwe na kauli thabiti...ili tujulikane tunalolisimamia.

Sent using Jamii Forums mobile app

itabidi utafute kamusi ikusaidie kuelewa maana na matumizi ya maneno. kutambua familia ni tofauti sana na familia kuiishi kifalme. hakuna hata uhusiano wa kauli hizo. ila ukisoma mada ngumu kuelewa kama hizi uwe na soda fanta pembeni huwa inasaidia kuongeza nguvu
 
Back
Top Bottom