kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,871
Habari iwe kwenu!
Kwanza nianze kwa kusema mimi ni muumini wa dini (Mkristo) na naheshimu sana dini za watu wengine. Niseme wazi kabisa kwamba Mungu ana utaratibu na Mungu anapenda utaratibu. Mungu hapendi kelele, hapendi vurugu na hapendi mambo yasiyo na mpangilio.
Pamoja na kwamba Mungu anatutaka kumuabudu, hataki kabisa tumuabudu hovyo hovyo, kila mahali (kwenye gari,njiani, sokoni, chooni, porini etc). Ndiyo maana Yesu anasema mnapotaka kusali ingia ndani mwako (inaweza kuwa kwenye nyumba kama kanisa au msikiti au ndani ya chumba chako) na usali katika roho na kweli. Kwahiyo Mungu wala si lazima asikie sauti zetu yeye anataka tumuabudu katika roho na kweli , unaweza kukumbuka habari ya yule mtoza ushuru na farisayo waliopanda kwenda hekaluni, jinsi mtoza ushuru alivyosali kwa moyo bila hata kusikika anasema nini , na Yesu ANASEMA SALA YAKE ILIPOKELEWA NA MUNGU.
Baada ya utangulizi huo, napenda kuikumbusha serikali kuacha kulea hiki kirusi cha kufanya kila sehemu kuwa nyumba ya Ibada. Yaani katikati ya nyumba za watu kuna makanisa na misikiti kama utitiri. Unavuka nyumba ya kwanza yapili kuna kanisa au msikiti, halafu kuna miziki mikubwa na sauti kubwa zinazofanya wengine washindwe kujipumzisha baada ya kazi za kutwa au hata kulala vizuri usiku. Najua watu wana haki ya kuabudu lakini pia ni wajibu kufuata utaratibu katika kutimizi haki hiyo. Na kama wenye imani yao hawataki kufuata utaratibu basi serikali ina wajibu wa kuwalazimisha wafuata utaratibu huo. Leo maeneo ya mijini hadi barabara zinafungwa na watu wanaosali/ swali. Ukitaka kuuliza unaambiwa ni haki yao au tuvumiliane, tunavumilianaje na watu wanaovunja haki za wenzao ya kutumia barabara?. Unamvumiliaje mtu anayekuzuia kulala kwasababu anatimiza haki yake ya kusali? , kwanini tuvumilie huku haki zetu zinavunjwa?. Watu wa dini watafute maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuabudia, hii ya nyumba ya mbele kuna kanisa halafu ndani kuna wapangaji ni uholela.
Najua watu watasema kwanini navumilia kuwa karibu na baa au kumbi za harusi ila naona shida kuwa karibu na kanisa au msikiti mtaani?. Jibu ni rahisi sana, baa ikijengwa karibu na makazi ya watu siku serikali wakitaka kuivunja hakuna atakayeongea. Watu watakuwa kimya tu kuona greda linakuja kulibomoa kama walivyokaa kimya kuona nyumba za kimara au TANESCO zikivunjwa, lakini siku serikali ikisema tunavunja misikiti yote au makanisa yote yaliyojengwa karibu na makazi, hapo ndipo tutashuhudia maneno na kauli za kila aina za waamini na viongozi wao. Kama kwa wakati huo Rais atakuwa mkristo utasikia lawama kutoka kwa waisamu na udini utaingizwa na kama atakuwa muislamu basi huenda wakristo nao wakaona wananyanyaswa na kuingiza udini. Sasa kuondoa hayo yote ni vizuri serikali ikapiga marufuku ujenzi wa misikiti na makanisa kiholela. Bora tukubali raia kujenga bila kibali maana siku hata zikivunjwa hakuna madhara makubwa kwa taifa kuliko kuacha makanisa na misikiti ikajengwa kwa holela kama tunavyoshuhudia sasa.
Ni heri kuziba ufa kuliko kujenga ukuta, narudia Mungu napenda utaratibu na kuheshimu haki za wengine unapotimiza wajibu wako.