Ujenzi wa Maghorofa: Kwanini Neti zinazotumika zinakuwa ni za kijani?

miss confidence

JF-Expert Member
Jul 9, 2016
393
273
Wakuu naomba Leo kuuliza hivi ni kwanini wakati ujenzi wa maghorofa ukiwa unaendelea neti zinazotumika ni neti za kijani katika kufunikia majengo wakati ujenzi ukiwa unaendelea????
Naomba kuelishwa je nikwanini hakuna rangi tofauti na rangi tajwa hapo juu ktk ujenzi wa maghorofa??? Je kuna sababu za kitaalamu za kutumia rangi ya kijani katika zoezi hilo??? Na sababu hizo ni zipi????
 
zipo nyeusi, kijivu na kaki ila nyingi ni za kijana. zinawekwa kwa lengo la usalama zaidi mkuu kwa fundi na yeyote anayepita chini endapo kitu kitadondoka chini
 
Mkuu uliyezungumzia suala la kuvaa nguo za kijani wakati wa upasuaji ungefanya kututoa tongotongo ikiwezekana ueleze na kwanin wapasuaji wanapoingia wanaweka mikono Kama wanaomba dua hivi sijajua huwa wanamaanisha nini
 
Zinaitwa safety net, kazi zake ni:
1. Kuzuia material zozote zinazondoka zisitoke nje ya site mf kwenda barabarani, au majengo jirani.
2.Kupunguza vumbi kali litokalo kwenye shughuli za ujenzi ndani ya jengo kama ubomoaji, na mengine, hunyunyuziwa maji ili kunasa vumbi linalozalishwa ndani ya jengo.
3.Rangi ya kijani inapunguza miale mikali ya jua hivyo kusaidia maji kupenya vizuri kwenye nguzo na kuta za jengo.
4.Kuzuia watu wasione kinachoendelea na pia watu wasione muonekano wa jengo mpaka kukamilika kwake.
 
Back
Top Bottom