Ujenzi wa madarasa nchi nzima; Kuna hatari naiona mbele juu ya fedha za IMF

Komando tamimy

Senior Member
Nov 18, 2020
108
121
Habarini wadau.

Nimejaribu kupitia juu ya miradi inayoendelea wilaya Mbinga na Songwe. Kama Tanzania nzima ndio inatekelezwa kwa utaratibu wa namna hiyo lazima basi uzalendo wetu upo kwenye matumbo yetu.

Na ni hatari sana kuwa na watu wa aina hii katika taifa letu.

Miongoni mwa mambo yanayofanywa na wakuu wa shule katika wilaya hizi hayakubaliki.
Nani hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu.

Yaani ujenzi wamewapa watu walevi? Mtu anajenga jengo la shule huku anakunywa pombe ?

Mmmmmmhhhh sijawahi ona Tanzania hii. Kwanini suala la mafundi wameachiwa wakuu wa shule.

Wengi wao wameishia kutafuta cheap workers, sasa ni hatari sana kwa mstakabali wa maendeleo yetu.

Wengine wameishia kutishiana na watendaji wa kata. Wakuu shule waondolewe kwenye usimamizi wa pesa hizo kwani kuna majanga makubwa yatakuja.
 
Hapo kinacholengwa darasa likamilike na chenji ibaki......sasa ikitokea injinia kaenda kukagua hayo madarasa inaweza kuwa aibu, wasituulie tu watoto kwa kuangukiwa na mijengo mibovu.
 
Shida kubwa Kama taifa ni hiki, pesa inatolewa amna michoro wala standard moja iliyotolewa ili kifuatwe na wasimamizi kote kunakojengwa madarasa.
Baada ya miaka mitano tunaanza tena kujenga madarasa...serikali jaribuni kuwa makini yaani utafikiri amna washauri huko TAMISEMI.
 
Kwanza walimu wakuu wanataabika sana,yaani wakuu toka wilayani wanachukua mgao mkubwa sana,hata ningekuwa mwalimu mkuu lazima ningetafuta fundi mlevi
Kwa hali hiyo hakika tutaishia kulalamika na wakati ukipewa nafasi unaboronga
 
Mbona sijaona sababu zako za kimsingi. Kumbuk tangu kuanza kwa shule walimu ndio huw wasimamiz sasa haijawah onekan wamefeli sana.

Njoo Nikupelek wilaya zilizojengwa usimamia
 
ukiona miradi inafanya bila kuzingatia taratibu walizojiwekea kwa kisingizio cha uharaka jua tunapigwa na mradi kukamilika chini ya kiwango rejea kauli ya Sofia Mjema mkuu wa mkoa😭😭
 
Yeye siyo fundi isipokuwa anafundi wake amekosa 10%
Nawaza hivyo hata mimi maana sababu alizotoa hazina mashiko.
Et mtu anafanya kazi huku anakunywa, mbna hao wako wengi hata viongozi wakubwa serikalini. Kikubwa hapa je kazi inafanyika kwa viwango vinavyotakiwa full stop.
 
Nawaza hivyo hata mimi maana sababu alizotoa hazina mashiko.
Et mtu anafanya kazi huku anakunywa, mbna hao wako wengi hata viongozi wakubwa serikalini. Kikubwa hapa je kazi inafanyika kwa viwango vinavyotakiwa full stop.
Kunywa siyo issue watu wanakunywa wanaingia kanisani, kuendesha gari n.k, yeye aseme nini kimekosewa
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom