Ujenzi wa lenta kwa nondo 3 unafaa?

Huo ni umaskini na kutojua kazi za nondo afu mafundi wenu hawaelewi chochote zaidi ya kukulahisishia ili usije kosa hela ya kumlipa,kama nondo tu zimezua ishu hizo stirrups itakuwaje,fundi ukimwambia stirrups zinafaida gani hajui utasikia kufungia nondo😂😂😂😂
 
Mondo moja= 22000 sasa mkuu kwa nini kama uwezo huna usisubiri kidogo? Kwa nini ufanye kitu chini ya kiwango ukijua baadae kitaleta majanga?

Usinunuwe vifaa vyote kama uwezo huna.
Mwambie fundi akupe idadi ya vifaa andika kwenye karatasi.mf. Mwezi huu nunua nondo tu 15 ×22000 zinatosha.
Mwezi ujao nunua mabati etccccc

Bora ufanye kitu kidogo ila quality hata kama ukichelewa kumaliza.

Vifaa vya ujenzi vina gharama inategemea nyumba unayotaka kujenga.
Juzi kuna mtu mwenyewe mipesa yake aliniomba nitafutie fundi professional nimpeleke site anihesabie gharama na vifaa nimtumie budget, ahaa kwa nyumba anayoitaka msingi tu ni mil 21 vifaa sasa tukaenda dukani nikauliza bei ndo nilijua kujenga sio mchezo.
 
Unaweza kutumia nondo nne(kama standards zinavyosema) lakini ukawa umevurunda sehemu nyingine za nyumba hivyo weakness ikawepo sehemu nyingine.

Labda tuulize chini/foundation umeijenga vipi(kwa standards zipi), je uliweka beams/nguzo kwenye pembe za nyumba? Ulitumia matofali yenye viwango vya juu/kati/chini?(kumbuka siku hizi tunauziwa tofali za ajabu sana).

Tukumbuke kuwa nyumba ni kama mwili wa binadamu tu, kila sehemu inategemea mwenzake.

Kama ulijenga chini vizuri, nyumba haijapinda, then hizo nondo tatu zinaweza kustahamili force kitoka juu .
 
Kitaalamu haufai kabisa.

Kwa sababu hiyo lenta(linta) ndiyo inapokea mzigo kutoka juu na kuleta msawazo wa jengo lako. Kwa sababu linta inapokea mzigo inatakiwa iipokee kwa usawa.

Kwanza kazi ya nondo ni nini kwenye linta??

Kazi ya nondo kwenye linta ni kuzuia kani(force) za mvutano ndani ya jengo lako!

Kwa nini sasa nondo tatu hazifai??
Ni kwa sababu standards zinashauri nondo lazima zifungwe symmetrically arranged. Ili zinapopokea mzigo na kuusambaza uwe sawa sawa.

Nondo tatu siyo symmetrically arranged. Sasa mzigo ukizidi kudogo tuu, jengo unaanza kuliona limeeanza nyufa na hata hiyo linta unaanza kuiona inapinda.

Suluhisho!

Ongeza nondo nyingine ziwe nne ili angalau ulete msawazo wa upokeaji wa mzigo na usambazaji wake.

Pia weka na nguzo kwenye kila kina na maungio ya jengo lako (kama ni nyumba kubwa na unataka idumu muda mrefu).

Ila kama ni banda tuu, komaa na aina ya ujenzi wako. Ila kama ni dream house, fuata hako kaushauri.
Acha ubabaishaji hapa, mondo Tatu zinafaa kabisa ili mradi nyumba iwe imefungwa mkanda kwenye msingi!
 
Nondo 3 zinafaa kabisa, lakini ziwe za mm 12, asije kukushauri uweke mm 10 hazitafaa. Hizo za mm 12 azisuke katika umbo la pembe 3 (yaani mbili chini kwenye base ya linter na moja juu, yaani ikae umbo la pyramid) lengo hapa ni kupata balance), fundi anaweza akazisuka na binding wire au anaweza asisuke pia; inategemea na ustadi wake katika kuzipanga inavyotakiwa. Mimi nimejenga nyumba yangu kubwa tu ya room 3, sebule kubwa tu, dining, jiko na store; na linter yake nimetumia nondo 3 za mm 12, juu ya linter nimeweka tofali za course 3, so naelezea kitu nnachokifahamu.
 
Sisi tunafungia NONDO 1 hata 10mm inatosha na nyumba inakaa huoni ufa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom