Ujenzi wa lenta kwa nondo 3 unafaa?

Negemu

Senior Member
Dec 26, 2017
135
126
Habari wakuu,katika kubana matumizi fundi kaniambia ujenzi wa lenta kwa kusuka nondo 3 unafaa,naomba ushauri wananzengo
 
Wewe utakufa kwa kuangukiwa na paa ukiwa umelala
Kachukue kijana mwenye diploma tu atakuchorea nyumba na kukuwekea gharama za ujenzi kwa bei nafuu
Kwa njaa yake huyo fundi kuna siku atakuambia mtumie springi za malori badala ya nondo
 
Habari wakuu,katika kubana matumizi fundi kaniambia ujenzi wa lenta kwa kusuka nondo 3 unafaa,naomba ushauri wananzengo
Kitaalamu haufai kabisa.

Kwa sababu hiyo lenta(linta) ndiyo inapokea mzigo kutoka juu na kuleta msawazo wa jengo lako. Kwa sababu linta inapokea mzigo inatakiwa iipokee kwa usawa.

Kwanza kazi ya nondo ni nini kwenye linta??

Kazi ya nondo kwenye linta ni kuzuia kani(force) za mvutano ndani ya jengo lako!

Kwa nini sasa nondo tatu hazifai??
Ni kwa sababu standards zinashauri nondo lazima zifungwe symmetrically arranged. Ili zinapopokea mzigo na kuusambaza uwe sawa sawa.

Nondo tatu siyo symmetrically arranged. Sasa mzigo ukizidi kudogo tuu, jengo unaanza kuliona limeeanza nyufa na hata hiyo linta unaanza kuiona inapinda.

Suluhisho!

Ongeza nondo nyingine ziwe nne ili angalau ulete msawazo wa upokeaji wa mzigo na usambazaji wake.

Pia weka na nguzo kwenye kila kina na maungio ya jengo lako (kama ni nyumba kubwa na unataka idumu muda mrefu).

Ila kama ni banda tuu, komaa na aina ya ujenzi wako. Ila kama ni dream house, fuata hako kaushauri.
 
Asante kwa ushauri mkuu

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom