Rais Samia Suluhu aongeza bajeti kwa asilimia 230 Ujenzi wa JN-HPP

Ujenzi wa bwawa la JN-HPP pamoja na Usambazaji wa umeme vijijini Rais Samia ameongeza bajeti kwa 230% kutoka TZS 1.01T FY2020|21 hadi TZS 2.34T FY2021|22,

===​

Tufahamu lengo la Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ni ifikapo mwaka 2026 Tanzania iwe na umeme wa Uhakika unaofikia Jumla ya 5,000MW.

Rais Samia Suluhu anamaanisha tunakwenda kuwa electricity donor country ama kwahakika Watanzania kesho yetu ni bora sana kuliko leo,tushikamane na mama katika kila hatua matokeo tutayaona,

Sote tunafahamu,mahitaji ya Umeme Tanzania yanaongezeka siku hata siku kwa mfano mwaka 2020 mahitaji ya Umeme Tanzania yalikuwa ni 1,151.66MW lakini hadi kufikia mwezi mei 2021 mahitaji ya Umeme yalifikia 1,183.28MW sawa na ongezeko la 3% kwa mwaka.

Kwamsiofahamu,mwaka huu pekee umeme wetu umetajwa kuwa ndio umeme wenye bei chee zaidi African ya Mashariki kwani tunauuza kwa $0.099/KWh,

Tanzania ya Rais Samia ni raha tupu natutegemee bei hii kushuka zaidi baada ya JN-HPP kukamilika na kuanza kufanya kazi,

Faida ya mradi huu mkubwa sio umeme tu hata utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020|25 ya kuzalisha ajira 8M ifikapo 2025,

Tayari mradi huu umeajiri Jumla ya wafanyakazi 7,243 huku wazawa wakiwa ni 6,452 na wageni ni 791,

Mradi huu utakapokamilika unatarajiwa kuzalisha Jumla ya MW 2,115, Watanzania kamwe tusiache kumwomba Mungu atuvushe kwenye hili salama,

Mpaka Rais Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani ni 38% tu ya fedha zote za mradi huu wa TZS 6.55trilioni ndio zilikuwa zimelipwa kwa mkandarasi,

Pesa iliyokwisha kulipwa na Mtangulizi wake ni Jumla yake ni TZS 2.495trilioni sawa na Pungufu ya TZS 4.055trilioni ili kukamilisha mradi ambazo Rais Samia Suluhu Hassan atalazimika kuzilipa,

Hii ni sawa na kusema Rais Samia Suluhu Hassan hadi mwisho wa mradi huu atakuwa ameujenga mradi huu wa JN-HPP kwa zaidi ya 62%,

Tukiacha roho mbaya Mama huyu anastahili pongezi sana kwa kiwango hiki cha Uzalendo anachokionesha kwa nchi yake,

Zikiwa zimesalia miezi michache tu kumalizika kwa mkataba huu,Rais Samia Suluhu Hassan kupitia bajeti yake hii ya kwanza tayari ameshatenga 58% ya deni lote lililosalia,Hii ni sawa na kusema baada ya bajeti hii mradi utatudai asilimia 4 tu ya fedha ili kukamilika

Rais Samia Suluhu tayari ametoa TZS 2.34trilioni kwaajili ya usambazaji wa umeme na ukamilishaji wa mradi huu wa JNHPP,

Bajeti hii moja ya Rais Sami ni sawa na pesa yote iliyotolewa na mtangulizi wake tangu kuanza kwa mradi huu wa JNHPP mwaka 2019,

Tunaweza kusema "Bajeti moja ya Rais Samia kwenye usambazaji wa umeme na ujenzi wa JN-HPP ni sawa na bajeti zote zilizotolewa kujenga JN-HPP tangu ianze Mei 2019 "

Watanzania,Kama kuna mtu wa kuombewa kwa nguvu kubwa kwa sasa basi ni Rais Samia Suluhu Hassan.



|
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN YUKO BEGA KWA BEGA NA VIONGOZI WALIOMTANGULIA|

Kazi iendelee Tanzania, Mama anafanya makubwa sana
 
IMG-20221222-WA0224.jpg
 
Back
Top Bottom