DOKEZO Ujenzi wa jengo la Mkurugenzi wa Uyui liko chini ya kiwango, wahusika wawajibishwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Uyui

Member
Nov 11, 2022
24
20
Wilaya Uyui ina maaajabu yake ambayo nahisi sijawahi ya kuyaona katika wilaya nyingine.

1. Kuna ufisadi wa kutisha katika majengo yaliyojengwa (jengo la mkurugenzi jipya)

Yaani jengo la serikali limekabidhiwa hata miezi miwili halina tiles zinabanduka, helper za kupandia ngazi ya ghorofa zimeanza kutoka, gypsum board zinabanduka ukiliangalia ghorofa ile unaweza ukadhani hakuna injinia, hakuna suveyor wa wilaya.

Yote Zaidi ya yote mkurugenzi akaamlisha wafanyakazi wote wahamie kwenye jengo ambalo halijakamilika, Unajua sababu yake, ili wapate hela za ukarabati mapema.

Nchi hii imekuwa wafanyakazi wa umma hawana huruma na kodi za wananchi wanajilia tuuu,


2. Ni wilaya ambayo inaongoza kwa coustomer care mbovu unaweza ukawekwa zaidi ya masaa 7 huku watu wa mapokezi wakiendelea kupiga soga, Kuna wadada fulani wako sehemu fulani wenyewe wanaendekeza rushwa bila rushwa no service.

3. Ni wilaya ambayo inaongoza kwa wafanyakazi kukaimi nafasi za uongozi. unaweza kukuta mtu fulani amekaimishwa nafasi yake kwa miaka 5 na hana sifa za kukaimu kwa masharti kama ni mwanamama awe ni mtoa ngono(Rushwa ya ngono) kama ni mkaka ni kumuonga huyo afisa mpaka ili aendeleee kukukamisha nafasi hiyo.

4. Ni wilaya ambayo matokeo yake huwa mabaya kuanzia darasa la 7 form 4 na form 6 kwa sababu uwajibikaji mbovu.

(b) Kukaimishwa nafasi za uogozi watu kwa muda mrefu.

(c) Ujuaji mwingi na kuwaza kupiga nilikuwepo huko kwenye ujenzi wa madarasa ya covid,Ujenzi ulijengwa chini ya kiwango na vifaaa vilivyobaki waliishia kugawana wakuu wa idara na wafanyakazi na viligombaniwa kama nzige.

Tamisemi imulikeni wilaya hii korofi kuanzia wakuuu wa idara mpaka wafanyakazi wa chini.

Nasikia kuna hela za samia za madarasa wajanja wameshaaanza kuandaaa mbinu za kivita.
 
Hao wanaendekeza rushwa hao wadada tongoza mmoja harafu peleka moto wakutosha kesho ukifika shemeji shemeji mnalalamika Sana na njia mnazo ukiweza ukuta unauruka vilevile
 
Acha uchochezi kama una duku duku lako ni vyema kuwa muwazi kuliko kuandika vitu ambavyo huna it hunitishi navyo.
 
hii wilaya ni jip mtu anakaimu nafasi miaka 10 kazi yake ni kupeleka mgao tuu wakubwa
 
Back
Top Bottom