Ujenzi wa hosteli shule ya sekondari Nandembo kuwalinda wasichana dhidi ya 'mafataki'

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu Sekonari (MMES) inatekeleza miradi mbalimbali ya uboreshaji wa miundombinu ya shule za sekondari ikiwemo ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike ambao hukumbana na ukatili wa kijinsia wakati wakirejea nyumbani.

Kutatua kero hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa kushirikiana na Serikali Kuu inatekeleza miradi mbalimbali ya kuboresha miundombinu ya shule za sekondari katika wilaya hiyo.

Katika mwaka 2016/2017 Halmashauri hiyo imepokea shilingi milioni 259 ambazo zimeelekezwa katika shule ya sekondari Nandembo iliyopo kata ya Nandembo ambayo inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa, vyoo, maabara na hosteli za wanafunzi.

Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Halmashauri ya Tunduru kinaeleza kuwa fedha hizo zitajenga vyumba vinne vya madarasa, hosteli mbili, matundu 10 ya vyoo na ukarabati wa maabara tatu za masomo ya sayansi. Na ujenzi huo tayari umekamilika kwa asilimia 90 na kukamilika kwake kutapunguza tatizo la ubovu wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia.

Ujenzi wa hosteli katika shule hiyo kwa kiasi kikubwa itapunguza changamoto za wanafunzi kutembea umbali mrefu, ikizingatiwa kuwa Kata ya Nandembo ina shule moja ya sekondari ambayo hutegemewa na shule za msingi 5 za Naluwale, Majala, Nangunguru, Tumaini na Nandembo.

Umbali wa shule hiyo ya sekondari huwa kikwazo kwa wanafunzi kufuatilia masomo kwa sababu hutumia muda mwingi kutembea na wafikapo shuleni wanakuwa wamechoka na kushindwa kufuatilia masomo inavyotakiwa.

Shue hiyo ina hosteli moja tu ya wasichana ambayo haikidhi mahitaji yote ya wanafunzi. Hali hiyo inaathiri ufaulu na wa wanafunzi wa shule hiyo hasa wasichana ambao wangewekewa mazingira rafiki wangefanya vizuri zaidi katika masomo yao.

Ujenzi wa hosteli mbili katika shule hiyo unaonekana kuwa mkombozi kwa wanafunzi ikizingatiwa kuwa shule hiyo inafanya vizuri katika mitihani ya kitaifa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali za uhaba wa miundombinu ya kujifunzia.

Mathalani, katika matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2016/2017 shule hiyo ilishika nafasi ya 31 kati ya shule 82 zilipo katika mkoa wa Ruvuma. Pia ilikuwa ya 835 kitaifa katika ya shule 3280 zilizopo Tanzania. Wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 56 lakini waliofeli ni 7 pekee.


Mwalimu Mkuu Nandembo atoa neno

Mwalimu Mkuu wa shule msingi Nandembo, Marry Ndunguru anasema ujenzi wa hosteli hizo upo katika hatua ya mwisho na zitaanza kutumika muda si mrefu. Anaeleza kuwa maboresho yaliyofanyika katika shule yake hasa ujenzi wa hosteli yatainua kiwango cha elimu katika shule hiyo kwa kuweka mazingira salama kwa wanafunzi kujisomea.

“Hosteli hizi zitaongeza tija kwa wanafunzi kuishi katika mazingira ya shule, kupata muda mwingi wa kujisomea, kuishi mazingira salama hasa wanafunzi wasichana na kuthibiti nidhamu ya wanafunzi wetu”, amesema Mwalimu Marry Ndunguru.

Zaidi, soma hapa => Ujenzi wa hosteli shule ya Nandembo kuwalinda wasichana dhidi ya ‘mafataki’ | FikraPevu
 
Mfataki wanawatesa sana wasichana, hatua ya kujenga hosteli hizo kutafanikisha elimu ya watoto kufikia ndoto zao
 
Back
Top Bottom