Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa wilaya ya Chato mkoani Geita

Nasema hivi, endelea kujenga mzee Magu yaani jenga tu ila umetusahau na huku KAHAMA. Huku ukijenga hata University inatosha sana yaani ukimaliza tu kujenga ka uni tuache usilete chochote tuko vizuriiii. Wakiendelea kuzingua tujikate zetu aalaaah maana tuna kila kitu madini,maziwa,fertile land, na mengine mengiiii
 
Tanzania ni zaidi ya Kilimanjaro. Na tuna mikoa 120 kama tukiamua kila kitu kwenye wilaya moja mikoa mwingine inakuwaje?Kuna mikoa iko nyuma kimaendeleo siyo Chato tu.Hivi kwa nini hiki kidogo kisigawiwe kwa usawa?

Kwa nini adhabu wapewe watanzania wakati watawala walikuwa wabadhirifu including yeye mwenyewe.
Mikoa 120?!!
 
Anasababu zake.Lakini hata Rais hana busara.Keki ya Taifa igawiwe kwa watanzania wote,si kila kitu kijijini kwake.Kuna mikoa haina hata hospital za maana.

Ifike mahali tusikubali kila upuuzi unaofanywa.Kuna mikoa 120,keki ya Taifa igawiwe kwa wote na si ukanda mmoja
Kuna mikoa 120?!
 
Binafsi sioni tatizo, tusonge mbele tutafika tu. Kikubwa university pia ijengwe kuongeza huduma. Bunge ngoja kwanza
 
Mie Mkuu nimebaki nashangaa tu. Yaani hiyo picha inajieleza kabisa.

Tatizo tunapenda kudanganywa na vimaneno,picha inazungumza uhalisia kuliko maneno ambayo yangeansikwa na mleta mada,ikiwezekana hz mada ziwe znakuja kwa stail hii.
 
Ipo siku atakuja kuona maovu aliyoyafanya
kweli mkuu hoja sio hoslitali maana kila mkoa au wilaya ina hitaji? swali je ni sahihi au kuna uhitaji wowote wa hospitali ya Rufaa wilayani Chatoo??
hii ni dalili mbaya maana kila atayekuja atanuia kwa dhati kuopendelea kwao.
 
Acha kubeba hoja za jumlajumla. Unajua idadi ya shule za sekondari zilizopo huko Kilimanjaro? Na baada ya kujua hizo shule umejua ngapi ni za serekali, watu binafsi na taasisi za dini? Ukija na data hizo wangalau utakuwa kwenye nafasi ya kuongea hicho unachoongea.

Hajui kuwa shule nyingi za kilimanjaro zimejengwa na wananchi,mashirika ya dini nk,serikali wanashule chache sana.
 
Akili za kushikiwa hizi za kuandika kitu ambacho hakihusiani kabisa na mjadala husika.

Matatizo ya kuukimbia umande haya. Jaribu kuelewa mjadala husika kama hujaelewa kinachojadiliwa ni bora kukaa kimya badala ya kuonyesha ujuha wako hadharani.
achana naye anapayuka tuu Wilaya ya Moshi(v) haina hosp ya wilaya wanategemea Mawenz ambayo ni ya mosho MJINI
Rombo wanategemea hosp ya Huruma inayomilikiwa na KANISA.
 
Sera za wizara ya afya zinasema hospital ya rufaa itajengwa makao makuu ya kanda, au wameshabadili hiyo sera. Maana nilimsikia mtaalam fulani toka hazina enzi hizo anahoji hospitali ya rufaa ya singida iliyotelekezwa kukamilika kutokana na ufinyu wa bajeti kwamba nani ariidhinisha hospital ya rufaa ijengwe singida wakati makao makuu ya kanda ya kati ambayo ni dodoma hayana hospital ya rufaa. Sasa naona hospitali ya serikali ya rufaa inajengwa chato, hospital ni kitu cha muhimu sehemu yoyote itakayo kuwepo lkn naona mkulu anazikanyaga sera za serikali yake ambazo ndio ilani anayoiongoza!
Tatizo ni ubinafsi tu na ukwetu mwingi.
 
Kwa ninavyofahamu mimi hakuna wilaya hata moja nchi hii ikiwa pamoja na zile wilaya kongwe ambayo ina hospitali ya rufaa ya serikali. Kama ipo, naomba kurekebishwa.

Kama nipo sahihi, kwanini kipaumbele kimekuwa ni Chato na isiwe Tunduru, Lushoto, Kilwa, Manyoni, Biharamulo, n.k?

Wapo watakaodai Mkoa wa Geita kwa ujumla hauna hospitali yenye hadhi ya kuwa hospital ya rufaa! Hapa chini ni ramani ya Mkoa wa Geita kama inavyopatikana kwenye website ya mkoa.

Geita.png

Ukiangalia ramani ya mkoa nayo, Chato iko pembezoni kabisa manake endapo ingekuwa katikati tungesema hospitali inajengwa hapo ili kuwarahisishia wakazi wa mkoa wa Geita!!

Again, tukiacha masuala ya kitaifa na kuangalia kimkoa zaidi, ni kwanini Chato iliyo pembezoni kabisa na sio angalau Geita ambako ndiko makao makuu ya mkoa ambako possibly, ndiko kunafikika kirahisi kutokea wilaya zote? Why Chato and not Geita, Bukombe n.k?!

Ukiangalia hata idadi ya watu; kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya ya Geita ni zaidi ya mara mbili ya wakazi wa wilaya ya Chato!! Wakati population ya Chato ilikuwa 365K, ile ya Geita ni 807K.

Again, why Chato na sio Geita!!!!

Hivi kuna mtu anaweza kutaja kigezo kimoja tu cha msingi cha kuichagua Chato na sio sehemu nyingine yoyote ndani ya mkoa wa Geita ili tuachane na mawazo kwamba rais anajipendelea kwao?!
 
TatiZo lenu wachaga mlizoea kila kitu kizuri mnataka kijengwe kwenu!huko kwingine kuna watu pia na wanahitaji huduma bora kama mlizojaza kwenu!tulieni!
Viti gani Kilimanjaro walipendelewa ambavyo vimejengwa na serikali?
 
Charity begins at home! Hata mie nikiwa rais lazima nipajenge kwetu kwanza.

Masuala ya siku nikifa halafu nisemwe sikupajali home sitaki mie....

Selfishness is natural to all human beings! Tuache unafiki...
 
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020 ineazimia kuwa na zahanati katika kila kijiji, kituo cha afya katika kila kata, hospitali katika wilaya na hospitali za rufaa kwa kila mkoa.

Na haya yameshaanza utekelezwaji wake kujenga Hospitali za rufaa za Mikoa na Kanda kuanzia huko Njombe( iko eneo la takiriban heka 70 nje ya mhi)
Huko mtwara inajengwa Mikindani (nje ya mji)
Huko Simiyu
Huko Kogoma
Huko Kaskazini inajengwa Babati( Karatu wanayo kubwa tu ambayo Ksnisa na Serikali zinashirikiana na sasa kutajengwa ya Wilaya)

Zinaendelea kujengwa mikoa yote lkn hamsemi mmekazania Chato Chato.

Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ina Hospitali Mbili zenye hadhi sawa ya kiwilaya. Hospitali ya Bomang'ombe na Hospitali ya Machame ambayo ni ya KKKT inayoshirikiana na Serikali km zilivyo zingine za Mashirika ya Dini hapa nchini.

Mjini Moshi wana KCMC,Mawenzi(inafanyiwa upanuzi mkubwa lkn km kawaida ya wachaga walishawarubuni watendaji wakapiga mshiko na kupelekea ujenzi kukwama) wana vituo vya afya kila kata na Hospitali binafsi kibao.

Kilomita chache km 20 su 30 huko Kibosho wana ingine kubwa Kibosho hospital ambayo pia Serikali inahusika

Ukisogea Siha ipo ya Wilaya na Kibong'oto

Marangu iko Marangu hospital na Kulema zote zikiwa karibu sana

Jirani na Marangu unakutana na Huruma Hospital ambayo nayo ni ya RC iliyopewa hadhi ya Wilaya

Mwanga wana Usangi Hispita ni ya Wilaya

Same wana Hospital ya wilaya

Kote humo nilikotaja, kila kijiji kina zahanati ya kijiji ambayo imejengwa na serikili, zahanati zingine zinakosa wagonjwa kwa muda mrefu sababu population ni ndogo.

Huko kote ukitafuta population yao na ukalinganisha na za eneo linalopigiwa kelele kwa maana ya Geita, Biharamulo, Chato na maeneo jirani au population ya maeneo mengine kulikojengwa/kunakojengwa Hospital za wilaya, na rufaa za mikoa na Kanda. Ni wazi kuwa Hospital ya Chato itahudumia population kubwa kuliko Hospital nilizotaja hapo kuliko hizo za Kaskazini.
 
Back
Top Bottom