Ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto Arusha iliyoasisiwa na mbunge wa Arusha mjini Lema umeshaanza

Safi sana magufuli.

Talk less, do more

Ulichoahidi ndicho unachotenda ,siyo kama chadema leo unahubiri Lowasa ni fisadi kesho unahubiri Lowasa ni mleta mabadiliko aende ikulu!!!!
Hongera Hon.Lema juhudi zako tunaziona Na kushuhudia ahadi zako.Long live Hon.Lema.
 
Mods mbona mnafuta comment zangu na mimi sijamtusi mtu wala kuvunja kanuni za JF!
 
Sijawahi kumkubali mtu mwenye mdomo mchafu na mwenye vurugu vurugu. Akae jela tu.
 
Kampuni ya kichina iliyoshinda zabuni ya kujenga Hopsitali maalumu kwa ajili ya mama na mtoto eneo la Matevesi Wilaya ya Arusha, CRJE (EA) Ltd imekwisha aanza kazi ya ujenzi baada ya kukamilisha usajili wa mradi na kuandaa eneo la kazi, ofisi na kuunganisha umeme na maji.

Mradi wa Hospitali maalumu kutatua kero kwa masuala ya kina mama na watoto uliasisiwa na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema na kutangazwa kwa umma mwaka 2010 wakati wa kampeni za Uchaguzi mkuu za mwaka huo. Wananchi wa Arusha walimuelewa na kumchagua Godbless Jonathan Lema kuwa Mbunge wao.

Mwaka mmoja baadae Mbunge Lema kupitia taasisi aliyoianzisha baada ya kuwa Mbunge ya ArDF-Arusha Development Fund, akafanikiwa kupata kiwanja cha kujenga Hospitali hiyo kutoka kwa Mawalla Advocates kupitia kwa Mkurugenzi wake marehemu Nyanga Mawalla mahali ambapo ndipo inapojengwa Hospitali hiyo sasa.

Makabidhiano ya kiwanja hicho toka kwa Mawalla Advocates kwenda ArDF yalishuhudiwa na Kiongozi Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh Freeman Mbowe, Mkurugenzi wa ArDF Elifuraha Mtowe pamoja na viongozi wa chama chake wananchi wengine.

Kikapita kipindi cha ukimya wakati huo Mbunge Lema akiwa amevuliwa ubunge. Aliporudishiwa baada ya kukata rufaa na kushinda akaendeleza wazo lake kwa kutafuta wafadhili wa kuweza kufanikisha mradi wenyewe tayari akiwa na kiwanja mkononi.

Jitihada za Lema kupitia marafiki na wadau mbalimbali zilimkutanisha na watu wa ulaya kutoka Shirika la Maternity Africa ambao waliafiki wazo lake na kuamua kuendeleza mchakato kwa kuanzisha michango kwa jamaa zao ulaya ili kupata fedha za kugharamia mradi.

Kufikia mwaka 2015 ArDF ya Lema wakasainishana mkataba na Maternity Africa wa kuendeleza mradi huo kwa ArDF kuwakabidhi rasmi kiwanja maalumu kwa Hospitali hiyo. Sherehe za makabidhiano zilifanyikia kwenye kiwanja hicho na kushuhudiwa na wadau wa pande zote wakiwemo wenye maslahi na mahitaji ya kimsingi ya kina mama na watoto.

Mpaka kufikia mwezi Agost 2016 Maternity Africa walikuwa wameshapata pesa za ujenzi na kuandaa michoro na kumtafuta mtaalamu mshauri na mkandarasi ambaye ndio sasa amekwishakuanza kazi ya ujenzi ambayo inatakiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja.

Hospitali hiyo ikikamilika itasaidia kupunguza kero ya huduma za uzazi kwa mama na mtoto, kama ambavyo Mh Lema aliona miaka mingi na kudhamiria kulifanikisha bila kujali ingemgharimu muda na pesa kiasi gani.

Ni jambo la kutia faraja sana kwamba Mbunge yuko Magereza kwa zaidi ya miezi miwili sasa lakini aliyoyaasisi yanaendelea kuwepo.

Tuzidi kumuombea mkandarasi, wataalamu wengine na wafadhili wakamilishe mradi huu kwa wakati kama walivyopanga ili wananchi wa Arusha waonje matunda mengine ya Mbunge Lema.

IMG-20170104-WA0007.jpg

IMG-20170104-WA0006.jpg

IMG-20170104-WA0008.jpg
 
Pia ni vyema wa

Pia ni vyema wafu wakapongezana maana hakuna pa kutokea wala kupumulia,
 
Back
Top Bottom