Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,679
- 149,864
Mimi nafikiri tunapaswa kupata mchanganuo wa Bajeti nzima ya ujenzi wa hospitali hiyo ya mkoa kabla ya kuendelea kulumbana maana huenda katika hiyo bajeti ya bilioni 46 kuna fedha za kujenga nyumba chache za madaktari,manesi na watumishi wengine wa hospitali hiyo pamoja na mambo mengine mbali na jengo tu la hiyo hospitali.
Isitoshe huenda ni pamoja na wodi za wagonjwa na hatuji ni wodi ngapi na mambo mengine ya aina hiyo na kama ni jengo la ghorofa basi tunapaswa kujua ni jengo la ghorofa ngapi na kutakuwa na majengo mangapi ya aina hiyo.
Inawezekana Raisi amechukulia kuwa ni jengo moja tu ndio litakalotumia hiyo bilioni 46 bila kupewa mchanganuo mzima maana sidhani kama alikosoa gharama hizo kwa kutaja/kuhoji gharama ya kila item katika ujenzi huo badala yake amehoji gharama ya jumla tu.
Alafu hivi hata kamati ya Bunge inayohusika na hata Bunge zima wakati wanapitisha hii bajeti ya ujenzi wa hii hospitali nao wote kwa ujumla wao walishindwa kweli kuona kama kulikuwa na tatizo katika hizi gharama?
Kama ni wizi basi hii itakuwa ni toomuch na wahusika watakuwa na roho ngumu tena wasiosoma alama za nyakati na ndio maana nasema katika hili tunahitaji kusikia kutoka upande wa pili.