Ujenzi wa Gas-Pipeline kutoka Mtwara-Dar unaanza kuingia nyongo.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujenzi wa Gas-Pipeline kutoka Mtwara-Dar unaanza kuingia nyongo..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwakalinga Y. R, Feb 19, 2012.

 1. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Katika siku za karibuni husani mwaka 2000-2010 wanaharakati wamekuwa wakipiga kelele jinsi mataifa ya nje yanavyoshirikiana na baazi ya viongozi wasio waaminifu kuhamisha rasilimali za nchi kutoka tz kupeleka mataifa ya magharibi.
  Mifano imejitokeza kwenye secta ya madini ambapo wawekezaji wamediriki kuchukua mchanga na kupeleka ulaya ukachekechwe kisa teknolojia ya kufanya hiyo shughuli haipo hapa kwetu.

  Siku za hivi karibuni Mh. JK ameweka bayana juu ya mpango wa serikali kuweka pipeline ya gas kutoka Mtwara kuipeleka Dar ili kuzalisha umeme.Habari zilizopo ni kwamba baazi ya wakazi wa Mtwara wameanza kuhamasishana kuupinga mradi huo kwa kilelezo cha kuwa kwa nini umeme usizalishwe Mtwara kisha ukasafirishwa? Kuna ugumu gani kwa hilo?.

  Mara nyingi serikali kupitia viongozi wasio na uzalendo wamekuwa wakikwepesha miradi kwenye maeneo fulani na kuipeleka kwenye maeneo wanayotoka wao bila kujali uwiyano ktk mgawanyo wa rasilimali za nchi.Hili la mtwara kuukwepesha mradi wa ujenzi wa power plant na viwanda vikubwa unakwepeshwa kwa makusudi.
   
 2. L

  LazaroSMtindi Senior Member

  #2
  Feb 19, 2012
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  10% itapatikanaje umeme ukizalishwa Mtwara.......hapa ni umimi tu.......
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,274
  Likes Received: 19,420
  Trophy Points: 280
  Mtwara bado wamelala na hao hao ndio kila siku huipigia kura ccm ngoja ile kwao wakiamka mda utakuwa umeshapita
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mleta mada nadhani hujafanya utafiti wa habari zako japo kidogo, Mitambo ya kufua umeme imejegwa Mtwara na inazalisha kwa sasa na kampuni inayoitwa Artumas na wapo mbioni kupanua shughuli hizo.

  Hii ni iliopo sasa:

  [​IMG]

  [​IMG]

  Halafu kumbuka pipe line ikija Dar, hiyo gas tayari ina soko huku kwenye viwanda na mitambo iliyopo na haitotumika kwenye umeme pekee.

  Tena usiwe na hofu hivi sasa wahi kununua viwanja huko, miradi mingi sana inakuja huko. Lindi na Mtwara inategewa kuwa ni miji ya Gas yenye kiwango cha dunia kwa wingi wa Gas ilivumbuliwa huko. Utaona wimbi la makampuni ya nje ya kazi za kila namna huko kuanzia hivi sasa. Nitafutie eka 20 za shamba karibu ya mjini.
   
 5. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #5
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Inashangaza sana ,awamu ya kwanza ya Mtwara Corridor umeaanisha wazi kwamba kutajengwa power plant yenye kuzalisha 300 MW za umeme,kisha baadae ziongezeke.Ila kwa sababu kama ulivyosem umimi kuna watu wanatamani hata mbuga ya serengeti na mt Klm uhamishiwe Bagamoyo ama Pwani kam sio Iringa na Dodoma.
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Bwagamoyo na maeneo ya karibu na Mlandizi mtegemee kusikia habari njema hivi karibuni, mafuta mengi sana yanategemewa kutangazwa onshore na offshore. Tayari kuna makampuni yanafanya utafiti wa kina na habari mpaka sasa ni njema sana.

  Nnayajuwa hayo kwa kuwa nna uhusiano wa karibu sana na "Main Contractor" wa maeneo hayo.
   
 7. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #7
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Acha kupotosha mambo mitambo iliyopo sasa inazalisha umeme chini ya 18MW ambapo sio lengo na mpango wa awali kwa nini wasimalizie mpango wa awali MW300 .Kwa nini wanaibua mradi mwingine wakati ule wa mwanzo haujafikia robo wakati lengo ni moja?.
   
 8. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,835
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Nadhaan Huu Mradi Kama Hakuna Ufisadi Katikati Yake nadhan ni Bora gas isafirishwe kwa Bomba kwani Matumizi ya Gas yapo ya aina nyingi!! Kwanza Kuzalisha Umeme; Pili Kutumika Raw Viwandani; Tatu Matumizi ya Nyumbani!! Kama huko Mtwara watakuwa wanahitaji raw gas nao wataachiwa Matoleo Yao!! Suala la umeme Mtwara Tayari wanao wa Kutosha Unaozalishwa na Artumus!! Nadhani cha Muhimu wanachotakiwa kukifanya ni Kuwashauri wabunge wao wasimame Kidete waweze Kuiondoa Tanesco Kwenye Supply ya Huo Umeme kwani nadhani Ukiritimba na Gharama zitapungua sana!! Hawa Jamaa wanazalisha Megawati 18; Ila matumizi kwa sasa ni Megawati 10; Megawati 8 hazina Watumiaji!! Live Data!!
  Huwa Wachina ni watu ambao wako so Corrupt!! Ingekuwa ni fresh Deal kutoka nchi ambayo ina reputation Nzuri katika suala la Kuzuia Rushwa nisingekuwa na Wasi!! Ila kwa wachina!!! Sijui!! Yangu Macho!! Mimi ningependekeza Hao Wachina watukopeshe Hizo Hela na sisi tutafute Reputable Contractor kwa free Tendering procedure Aweza kufanya Kazi hiyo ya Ujenzi!! Kwani by any How we are supposed to pay for the loan!! Nawasilisha
   
 9. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #9
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mkwe21

  Nipo na wewe katika hilo.Ila kwa nini wasimalizie miradi ya awali kwanza kwa sabubu katika mpango wa mwanzo manufaa yapo na yashafanyiwa visibility study ya kutosha na impact ishaanza onekana.Wenzetu wa Mozambique wapo mbali sana kwani wameshatoka kwenye awamu ya kwanza ya maputo corridor .Sisi tunasua sua kutokana na siasa.Zambia na malawi wanasubiri kwa hamu mpango huu kwani nao wapo kwenye huu mpango ambapo chimbuko lake ni Mtwara -Tanzania.

  Inabidi viongozi waache ubinafsi sio lazima viwanda vijenge Dar na Pwani peke yake .Huo sio mgawanyo bora wa rasilimali za taifa.
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Feb 19, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mitambo ya Arumas iliyopo hivi sasa Mtwara inazalisha umeme kidogo tu kwa ajili ya Mtwara na Lindi. Mradi anaouzungumzia mleta mada hauhusiani na mradi wa Artumas.
  Lakini pia, kuna gesi Songosongo na bomba toka huko hadi Dar. Pia kuna gesi nyingine Mkuranga. Hivi hiyo haitoshi kuwagawia hao wa dar mpaka itolewe nyingine kutoka Mtwara?
  Huo mradi wa bomba toka Mtwara ni ufisadi tu. Ni rahisi zaidi kiuchumi kuzalisha umeme pale pale Mtwara inapozalishwa gesi na kisha kuusafirisha umeme huo mpaka dar. Kwa kufanya hivyo, tutawezesha na wilaya, miji na vijiji vilivyo njiani navyo kupata umeme, kama ukijenga bomba la gezi, wilaya, miji na vijiji hivyo havitanufaika na lolote. Na pia kutakuwa na umeme wa uhakika katika mikoa ya kusini, nayo itakuwa imeunganishwa kwenye gridi ya taifa
   
 11. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #11
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Namuunga mkono asilimia 100 mtoa mada. Mikoa ya Kusini ya Lindi,Mtwara na Ruvuma imesahaulika ki- maendeleo kwa karne nyingi. Wananchi wa mikoa hiyo kwa mfano wamekatazwa wasilime pamba eti kuna wadudu kutoka Msumbiji ambao watavuka na kuharibu pamba hiyo na kuenea hadi Kaskazini. Haiingii akilini hoja hiyo kwasababu pamba yote inayolimwa inatumia madawa yenye gharama kubwa kuulia wadudu (thiodan). Je, ina maana hao wadudu wa Msumbiji hawawezi kuuwawa kwa dawa? Kwa hiyo kuweka bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dsm ni mikakati ile ile ya kuifanya mikoa hiyo isichupe kimaendeleo. Upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mikoa hiyo utachochea uanzishwaji wa viwanda vingi na hivyo kutengeneza ajira. Matatizo yanayoukabili Mji wa Dsm kuwa na wamachinga wengi ni kwasababu ya uwepo wa shughuli nyingi za kibiashara. Serikali ijenge mitambo mikubwa ya kufua umeme wa gesi huko huko Mtwara na kuuweka kwenye gridi ya taifa. Kuhusu gesi ya kupikia, kijengwe kiwanda cha kujaza kwenye mitungi huko huko pia kama tunavyonunua mitungi ya Oryx.
  Umeme ukiwa mwingi huko Mtwara na Lindi, viwanja vya ndege vitapanuliwa na bandari kubwa zitajengwa. Vinginevyo, upanuzi wa miundo mbinu na Mtwara Corridor itakuwa ndoto!
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jamani ivi gharama ya kujenga power plant mnaifahamu?
  Alafu unapolocate power plant unaangalia na walaji kama wapo karibu bse kuusafirisha umeme on the way unapotea kheri kusafirisha gas.
  Kama ni umeme hao jamaa Artimus inawatosha
   
 13. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #13
  Feb 19, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hivi Huyu Mh. Membe si wa kusini?

  anawasaidiaje watu wa kusini??

  Hawa wabunge wa kusini wengi wao si wa Xixm? Mbona hawana ushirikiano?

  Membe anashindwa kuwasaidia wananchi wa kanda yake kwa nafasi aliyonayo? Je akipewa urais ndo ataweza kuwasaidia watanzania?
   
 14. TASLIMU

  TASLIMU Senior Member

  #14
  Feb 19, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafuatilia hili nione tunafanya nini watu wakusin wenzangu
   
 15. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #15
  Feb 19, 2012
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Umeanza vizuri na nikakubaliana na wewe. Lakini kuwalundika wachina wote kwenye kapu moja si haki na si kweli! Ingekuwa ni hivyo tungekuwa na shida kubwa nchi nyingi za kiafrika. Ni mradi upi umesikia wachina wamerubuni kiasi cha kuwaita wala rushwa! Au unawafananisha na nani? Mwiningereza(sijasema waingereza) BAE, British Gas? Mkanada kule kwenye mradi wa Songas? Madini kule Ulyankulu, Geita, Mara? Mwamerika kule Iraq, Nigeria? Mrusi kule Albania au nani?

  Kule Mtwara kumekucha wapo makampuni mengi sasa including British Gas(the world leader kwenye fani hii, na tajiri kuliko wote), Arthumas kakimbia, yuko Msumbiji lakini upande wa pili tu wa Mnazi Bay, kauza share zake kaacha kiduchu.

  Lakini wachina wapo! Wana miradi miwili, mmoja ndio wa kuleta Gas Dar lakini kama wafadhili, bomba litamilikiwa na TPDC, litaendeshwa na TPDC, gas itauzwa na TPDC, Shirika letu lililotulindia heshima miaka nenda rudi hadi Nkapa alipowasulubu! Wa pili, wanataka kuzalisha umeme pale pale Mtwara halafu wausafirishe kwa nyaya hadi Singida(singida!) ili kutoka pale uhudumie mikoa ya magharibi. Hizo dalili za rushwa umeziona wapi?
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Lengo ni moja nia tofauti.
   
 17. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Nawe pia inakubidi uchukue hatua sio kusubiri tu...
   
 18. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nchi ya maziwa na asali, tumeshindwa kuila wenyewe tumeamua kugawa vyetu na sasa hata hiyo gas itatuchukua miaka kadhaa kuifaidi. Nashindwa kuelewa kwanini mpaka sasa gas inayopatikana nchini kwetu imeshindwa kuandaliwa itumike na watanzania wote zaidi ya matumizi ya kuzalisha umeme na viwandani! Sidhani kama bei ya gas leo mtungi ungefika 50,000.. hii ni balaa utafikiri hatuna wataalamu kila nyanja, ukizingatia mabadiliko ya tabia nchi sasa tunaelekea kuwa jangwa kwa jinsi miti inavyokatwa ovyo kuzalisha mkaa na kuni, watakapo zinduka na mikakati ya kuokoa mazingira gharama itakuwa bora wangegawa gas bure..
   
 19. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,275
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  ni kweli unachokisema Njowepo. mtoa mada anapaswa kufanya utafiti kidogo, kusafirisha umeme ni ghali sana na unapotea mwingi ni afadhali kusafirisha gas kwenye pipe. pia akumbuke kuna mitambo ya umeme kule mtwara na hili la kwamba gas ina matumizi mengi sana huku dar na mikoa mingine kama viwanda, majumbani nk
   
 20. MMAHE

  MMAHE JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 831
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kuna Membe, Mkuchika,Ghasia. tena Ghasia na Mkuchika ndio vinara wa kusapot huo ufisadi. wote vilaza tu!!
   
Loading...