Ujenzi wa Gabion, nyumba kwa milioni 2 tu!

goodfool

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,664
993
Hamjambo wakuu,

Moja kwa moja kwenye mada,

Wakati nikisubiri zile milioni 3 zangu zijae ili nijenge, nimepata wazo jingine la ujenzi rahisi kabisa.

Ujenzi huu unahusisha mawe na mesh (nyavu), nimeona ni less cost kwa kuwa simenti haihitajiki sana na unaokoa muda

""""" kumbuka nia yangu ni kufanikisha kujenga kwa gharama nafuu zaidi na makazi yenye hadhi, kwa gharama ileile"""""

Nawashukuru watu wachache wa hapa JF walioyeyuka mioyo na kuonyesha nia ya kunisaidia kimawazo hata kitaaluma kabisa, huko PM wapo wengi tu.

Katika ujenzi huu nitapaua kwa zege nyumba ya vyumba viwili tu na kisiitingi rumu.


Hapa napunguza gharama za:-

Mbao,
Ceilings
Bati
Misumari


Katika zoezi hili nitatumia wire mesh za bei nafuu kabisa na nondo chache.

Kwanini tusimiliki nyumba???

Nawasilisha.
Screenshot_20190309-025745.jpeg
IMG_20190309_202939.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom