Ujenzi wa "flats" 20 za ghorofa nne kwa Tshs bilioni 10, kila flat ni Tshs milioni 500. Twende kazi!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,873
Kwanza naomba kuweka wazi kuwa mimi ni Engineer na nimeshiriki miradi kadhaa ya ujenzi katika mikoa mbalimbali hapa Tanzania.

Nimejikuta nikitamani sana kwenda kuukagua ujenzi unaoendelea pale UDSM ambao ni (typical lay out) ya flats 20 huku kila flat ikiwa na ghorofa nne. Kwa mantiki ya "typical lay out ina maana kila flat imegharamiwa sawa, hii ni kusema kuwa kila flat imegharamiwa kwa Tshs milioni 500?

Ikumbukwe kuwa TBA ni consultant tu ambaye inamlazimu kutafuta main contractor na huyo main contractor ambaye ni mjenzi pia atafute sub contractors kwenye upande wa plumbing na electrical. TBA amejithibitisha mbele ya rais Magufuli kuwa tender document ya contractor pamoja na subs aliowatafuta haikufika Tshs bilioni 10 kwa flats zote maana na yeye ni lazima kwenye hiyo bilioni 10 apeleke wakaguzi site na vikao vya kila muda kwa mujibu wa taratibu pia ni lazima abaki na akiba kama mfanyakazi anayetakiwa kuendesha ofisi. Any way swala la usafiri limeepukwa kwa kuwa mradi upo kilomita chache tu kutoka zilipo ofisi za TBA.

Sasa kweli kila flat imegharimu Tshs milioni 500 kwa kila kitu? Building structure + mechanical, plumbing + electrical installations? Ubora wa jengo?

Kwenye mambo ya ujenzi kama haya huwa kuna kitu tunaita "additional works" yaani kutokana na mabadiliko ya bei za vifaa, kukosea kwenye quotation, kuongezeka vitu vya ziada inamlazimu mkandarasi kuandika "claim" ya kuomba fedha zaidi kutokana na hilo.

Pengine huu mradi wa Tshs milioni 500 kwa kila flat una "claims" kibao za additional works ila tutakuja kuambiwa kuwa zimetumika tu Tshs milioni 500 kwa kila flat. Nani atakagua? Mchakato wa ujenzi na taratibu zilifuatwa?

Hata ukinichinja nipo tayari kuliko kuamini kuwa pale UDSM flat moja ya ghorofa nne imegharimu Tshs milioni 500 hadi kukamilika!

............................... ...................
Kwa hesabu za kawaida emb tuangalie uwezekano wa ukubwa wa blocks zenyewe na ubebabji wake wa wanafunzi
Tunazo blocks 20
Kila block ina floor tano including ground floor (0-4)
Kwa hiyo floor zitakazobeba watu zipo 5
Tuchukue 4000/20=200 Ina maana kila block moja inabeba wanafunzi 200.
Chukua 200/5 = 40,
hapo ni kuwa kila floor inabeba wanafunzi 40. Kutokana na hilo inamaana kuwa floor moja ina 40/4=10 (Vyumba 10) Vya kulala wanafunzi, imagine kila floor kuna vyumba 10 vya wanafunzi wanne-wanne kila chumba. Sasa kwa structure kama hiyo ninayoona hapo kwenye picha ya MsemajiUkweli ina maana kuwa jengo moja lina Lot 2, kwa maana hiyo kila Lot ina vyumba vitano (Vya kulala per a floor) kutokana na namba ya wanafunzi. Sijajua idadi ya vyoo hadi labda nione mchoro. Possible kila chumba kikawa na vitanda vinne vya ghorofa moja moja kwa kiwango cha chini cha kubana matumizi ya nafasi (juu na chini)

Kitanda cha kawaida kina futi 6+6 + door space unapata takriban 7. 5m!!! Upana labda tukadirie 4m (Kiwango cha chini) kwa kila floor (Section ya vyumba vya wanafunzi W×B) Hapo bado upana wa ngazi + Vyoo, mabafu na Electric cubicles! Bado nyie ni Matomaso??

Alaaaa kumbe huu ni mradi mkubwa sana na kwa harakaharaka Total amount ya kwenye BOQ haiwezi kupungua bilioni 40 Tshs!!! Nipo tayari kusimamia hilo hadharani na kama wanabisha waweke hesabu hadharani..Anayedhani kuwa huu mradi uko chini ya Tshs bilioni 35 kwenye BOQ (Bado hujaweka Preliminary costs) basi ajichunguze akili yake!!!!!! Ngoja kwanza nikapate details zaidi hiyo jumanne!!
..............................................
Wakuu, naahidi kuwa hii thread nitai-update baada ya kutembelea ujenzi wa UDSM hapo jumanne wiki ijayo. Naahidi kuwa nitadadavua kila kitu na mwisho tukubaline kuwa kama ni sahihi kudanganywa kuwa kila block imegharimu Tshs 500 milioni mpaka kukamilika. Nitakagua ubora wa jengo na nitaweka humu kila kitu!

======

UPDATES

Hosteli za Magufuli chuoni UDSM zimeanza kubomoka. Nini chanzo? Watoto wetu watapona?
 
Ipo tofauti kati ya apartment na block. Block is a large building that contains apartments/flats. Rekebisha heading- ujenzi wa block 20 za ghorafa nne. Swali muhimu - kila floor inayo flats au vyumba vya wanafunzi vingapi?
Nimekuelewa mkuu ila nimetumia lugha ya mkuu sana. Najua kuwa kwa kutumia neno flat basi jengo lingekuwa moja tu.

Unaamini kuwa kila jengo limegharimu Tshs 500 milioni?
 
Nimekuelewa mkuu ila nimetumia lugha ya mkuu sana. Najua kuwa kwa kutumia neno flat basi jengo lingekuwa moja tu.

Unaamini kuwa kila jengo limegharimu Tshs 500 milioni?

Gsam hebu tufungue macho, kwa flat moja kama hilo unadhani wangalau kadirio ilipaswa kuwa ngapi? Maana katika maelezo yako hapo juu nimeshindwa kuelewa hiyo mil 500 ni nyingi sana ama ni kidogo sana? Ama una maelezo ya ziada kwenye hiyo shaka yako? Hebu funguka mkuu.
 
Jamaa waliropoka tu ka kuwanyima wenzao contract. Sasa kimbembe ni wakati JPM atakapo amuru kuwa wapewe wao hiyo contract iloshindikana, ndio watajua ni mbichi au mbivu.
 
Hakuna kitu kama hicho kwenye ujenzi. Usijidanganye kuwa fedha iliyotumika ni hiyo!
Nimemalizia kujenga nyumba yangu huku Bariadi,quantity survayor alinipa gharama mwaka jana mwezi wa kwanza 60M.Nilipuuza nikaamua kununua cement na kufyatua mimi mwenyewe,vifaa vyote nilikaba penalt na 99.99% hakuna aliyeninunulia kitu next month naezeka nimegharimikia kwa 5.2M pekee. Naamini kuja kumaliza kila kitu nitatumia 15M tu
 
Nimemalizia kujenga nyumba yangu huku Bariadi,quantity survayor alinipa gharama mwaka jana mwezi wa kwanza 60M.Nilipuuza nikaamua kununua cement na kufyatua mimi mwenyewe,vifaa vyote nilikaba penalt na 99.99% hakuna aliyeninunulia kitu next month naezeka nimegharimikia kwa 5.2M pekee. Naamini kuja kumaliza kila kitu nitatumia 15M tu

Mkuu hiyo nyumba ina vyumba vingapi?
 
117 Reactions
Reply
Back
Top Bottom