Ujenzi wa "flats" 20 za ghorofa nne kwa Tshs bilioni 10, kila flat ni Tshs milioni 500. Twende kazi!

Nimemalizia kujenga nyumba yangu huku Bariadi,quantity survayor alinipa gharama mwaka jana mwezi wa kwanza 60M.Nilipuuza nikaamua kununua cement na kufyatua mimi mwenyewe,vifaa vyote nilikaba penalt na 99.99% hakuna aliyeninunulia kitu next month naezeka nimegharimikia kwa 5.2M pekee. Naamini kuja kumaliza kila kitu nitatumia 15M tu
Kweli kabisa. Ukitaka usijenge wewe wasikilize Wabongo, maana ni hatari sana kwa kuzusha vitu , kitu cha mia 200 atakuambia kinauzwa eflu 10
 
Mkuu hiyo nyumba ina vyumba vingapi?
Unasoma na kuamini mzaha wa huyu ndugu?

Hakuna kitu hapo. From 60M eti hadi 15M tena Bariadi ambako ili simenti ifike huko, basi itauzwa kati ya 16,000 na 20,000!!...Hata ukabe penati na hadi ujikabe koo mwenyewe ni impossible ku - reduce gharama kwa 45M toka makadirio ya awali ya 60M....Mzaha huo tena wa kipuuzi kabisa ktk ishu serious kama makazi a.k.a nyumba!!

Kwa gharama yake hii, hata kibanda cha nyasi tu na tofali za tope la udongo wa mfinyanzi wa huko kijijini kwao Lagangabilili - Itilima hawezi kukamilisha kujenga....Ni mzaha wa ki - CCM tu huo, achana naye!!


Nimemalizia kujenga nyumba yangu huku Bariadi,quantity survayor alinipa gharama mwaka jana mwezi wa kwanza 60M.Nilipuuza nikaamua kununua cement na kufyatua mimi mwenyewe,vifaa vyote nilikaba penalt na 99.99% hakuna aliyeninunulia kitu next month naezeka nimegharimikia kwa 5.2M pekee. Naamini kuja kumaliza kila kitu nitatumia 15M tu
 
Nyie ndio mliozoea zile enzi za JK,

Kwani waliopokea hiyo kazi hawajui hayo unayoyasema?

Tusubiri wakamilishe then ukaguzi ufanyike.
Na nyie ndo ambao mmejitoa ufahamu na kukubali kulishwa UONGO na Rais wenu kila kukicha,
 
Kwanza naomba kuweka wazi kuwa mimi ni Engineer na nimeshiriki miradi kadhaa ya ujenzi katika mikoa mbalimbali hapa Tanzania.

Nimejikuta nikitamani sana kwenda kuukagua ujenzi unaoendelea pale UDSM ambao ni (typical lay out) ya flats 20 huku kila flat ikiwa na ghorofa nne. Kwa mantiki ya "typical lay out ina maana kila flat imegharamiwa sawa, hii ni kusema kuwa kila flat imegharamiwa kwa Tshs milioni 500?

Ikumbukwe kuwa TBA ni consultant tu ambaye inamlazimu kutafuta main contractor na huyo main contractor ambaye ni mjenzi pia atafute sub contractors kwenye upande wa plumbing na electrical. TBA amejithibitisha mbele ya rais Magufuli kuwa tender document ya contractor pamoja na subs aliowatafuta haikufika Tshs bilioni 10 kwa flats zote maana na yeye ni lazima kwenye hiyo bilioni 10 apeleke wakaguzi site na vikao vya kila muda kwa mujibu wa taratibu pia ni lazima abaki na akiba kama mfanyakazi anayetakiwa kuendesha ofisi. Any way swala la usafiri limeepukwa kwa kuwa mradi upo kilomita chache tu kutoka zilipo ofisi za TBA.

Sasa kweli kila flat imegharimu Tshs milioni 500 kwa kila kitu? Building structure + plumbing + electrical installations? Ubora wa jengo?

Kwenye mambo ya ujenzi kama haya huwa kuna kitu tunaita "additional works" yaani kutokana na mabadiliko ya bei za vifaa, kukosea kwenye quotation, kuongezeka vitu vya ziada inamlazimu mkandarasi kuandika "claim" ya kuomba fedha zaidi kutokana na hilo.

Pengine huu mradi wa Tshs milioni 500 kwa kila flat una "claims" kibao za additional works ila tutakuja kuambiwa kuwa zimetumika tu Tshs milioni 500 kwa kila flat. Nani atakagua? Mchakato wa ujenzi na taratibu zilifuatwa?

Hata ukinichinja nipo tayari kuliko kuamini kuwa pale UDSM flat moja ya ghorofa nne imegharimu Tshs milioni 500 hadi kukamilika!

Wakuu, naahidi kuwa hii thread nitai-update baada ya kutembelea ujenzi wa UDSM hapo jumanne wiki ijayo. Naahidi kuwa nitadadavua kila kitu na mwisho tukubaline kuwa kama ni sahihi kudanganywa kuwa kila block imegharimu Tshs 500 milioni mpaka kukamilika. Nitakagua ubora wa jengo na nitaweka humu kila kitu! Mods naomba mnilindie thread yangu.
Kuna mtu aliwahi kuniambia wasiwasi wako huo. Ujenzi haujawahi kuwa rahisi kama watu wanavyofikiri, hasa kupata kitu quality Ndiyo maana kampuni makini kama NOREMCO, Skanska et al waliondokoa Tanzania, kwanza kwa sababu ya wao hawatoi rushwa kabisa kwa mujibu wa sera za Norway lakini pia wao huzingatia vigezo vyote na ubora na kwa hiyo bei zao ni ghali lakini unapata kitu roho inapenda. Hivyo hata kama ni kweli kuwa gharama ni hizo tulizoambiwa lakini tunaomba iwe kwa Quality inayotakiwa.
Iko hivi, kama huna uhakika wa gharama za jengo, fanya kitu kinachoitwa PRO RATA RATES. Kwa sasa, jengo standard pro rata rate kwa Square metre ni kati ya 400,000-700,000!
Sasa kama jengo lina ukubwa wa mita 15x22=330 m square. Likiwa na floor nne tayari ni square metre 1320. Hizo ukizidisha kwa wastani wa 500,000=660,000,000/-

Kwa kuwa kazi hii hufanywa na Wakadiriaji majenzi(Quantity Surveyors) basi ni wao pekee wanaoweza kuelezea uhalisia wa gharama kutokana na current market price ya materials.
 
Bedroom tatu na master moja,seating room,jiko,store,korido,choo na bafu na varanda mbili.
Nilifyatua tofari 4500 kwa mfuko mmoja ratio ya tofari 28-30 concrete.
Quantity surveyor aliandika tofari 1@1200 mimi kwa gharama zangu ni 700Tsh.Mchanga alisema trip moja 150K mimi nikapata kwa 45K peke yake,maji alisema trip moja kwa 20K mimi nikapata 5K peke yake.
Wakati wa ujenzi mbao za matumizi nilipasua miti yangu kwa shilingi 3500 kwa ft 7.Kila kitu nilinunua mimi,baba alianza kusimamia mwanzoni nikaona analegeza nilimpiga chini nikawa incharge wa kila kitu mimi japo niko mbali nilifanikiwa

Acha fujo wewe...weka picha hapa..

Lori la 45k ni m3 ngapi?Na Bariadi mchanga mzuri wa kujengea mnatoa wapi,kadiria umbali tukushike vizuri

Mbao umepasua miti yako?Hizo mbao ni za kupaulia au?Maana nyumba ya chini mbao ni minor issue..

Tofali umeokoa kitu kidogo mno...Hiyo idadi ya tofali kwa vyumba vyote hivyo umedanganya...ni uwongo...nipe total parameter,outer na individual spaces ndani ya nyumba..

Nipe hesabu za nondo,cement,kokoto,kupaua,nichambulie bati na mbao treated na accessories zake,bandering+cealing,plaster,madirisha,milango,machoo,jikoni...halafu uje na uongo wako wa 15mil...muongo mkubwa wewe,katubu dhambi
 
Nimemalizia kujenga nyumba yangu huku Bariadi,quantity survayor alinipa gharama mwaka jana mwezi wa kwanza 60M.Nilipuuza nikaamua kununua cement na kufyatua mimi mwenyewe,vifaa vyote nilikaba penalt na 99.99% hakuna aliyeninunulia kitu next month naezeka nimegharimikia kwa 5.2M pekee. Naamini kuja kumaliza kila kitu nitatumia 15M tu

Mkuu samahani lakini.
 
Sasa unatuaminisha nini labda mkuu??? Majungu tu hizi gharama unazopiga usisahau kua Magufuli amekua waziri wa ujenzi kwa miaka kumi (10) he knows what he is doing na pale UDSM kuna civil engineers and others kama electrical wote nafikiri kama kuna makosa either students au wahadhiri wangekua wameshaleta hata uzi na ujenzi unamalizika.

Njoo ukague ukitaka ila watu kama nyie haters will be there unamaanisha wote pale wasomi na Rais ambaye naye amekua waziri for ten years wasielewe wewe na huko unakotoka sijui hata barabara ya mliman unaifahamu uje kukagua na kutupa tathmin.. Shame on you!

Mkuu mbona povu sana na swearing nyingi sana?

Tupe mchanganuo wako wewe unaoonesha kweli bajeti ni 10bilion,instead umekuja na tirades of swearing bila hoja pingifu...

Sasa tukueleweje ndugu?
 
Back
Top Bottom