Ujenzi wa "flats" 20 za ghorofa nne kwa Tshs bilioni 10, kila flat ni Tshs milioni 500. Twende kazi!

Nimemalizia kujenga nyumba yangu huku Bariadi,quantity survayor alinipa gharama mwaka jana mwezi wa kwanza 60M.Nilipuuza nikaamua kununua cement na kufyatua mimi mwenyewe,vifaa vyote nilikaba penalt na 99.99% hakuna aliyeninunulia kitu next month naezeka nimegharimikia kwa 5.2M pekee. Naamini kuja kumaliza kila kitu nitatumia 15M tu
weka picha basi,isije kuwa ya udongo,vyumba viwili na bado hujapaua.
 
Nimemalizia kujenga nyumba yangu huku Bariadi,quantity survayor alinipa gharama mwaka jana mwezi wa kwanza 60M.Nilipuuza nikaamua kununua cement na kufyatua mimi mwenyewe,vifaa vyote nilikaba penalt na 99.99% hakuna aliyeninunulia kitu next month naezeka nimegharimikia kwa 5.2M pekee. Naamini kuja kumaliza kila kitu nitatumia 15M tu

Muongo mkubwa...kadanganye watoto...mijitu mizima inaposema uongo inaboa sana...

Labda uwe unajenga choo...and i mean choo kikweli...eti kuezeka 5.2mil,labda hela ya fundi hiyo,au umeezekea fito..mbao za saohill tu ukatizi na hicho ki 5.2mil...bati za vipande ndio kabisa sahau....eti nyumba nzima 15mil...itakua umejenga banda wewe unadhani nyumba...archtect kakuelekeza nyumba wewe umeenda jenga banda,
 
Kila kitu kiko sawa na TBA hawahitaji malipo yoyote kama ofisi wao wapo kazini kama kazi zingine za kila siku.

Wajenzi nchi hii mmewaibia sana watanzania ktk gharama za ujenzi.

Nenda Africa ya Kusini kaangalie gharama za ujenzi wa nyumba ziko chini sana na nyumba ni imara sana MTU anaweza kumiliki bila shida yoyote.

Sasa mtoa mada unafikiria dili tu hakuna kitu kingine.

Flat hazibomoki ziko imara na zitadumu .
 
Kweli Raisi tunaye mambo anayoyafanya hayajawahi kufanywa na Kiongozi yeyote duniani
source:clouds tv
mkuu kusema ukweli na upenzi wa Mungu,,hawamu hii Rais tumepata,,ukitaka kujua ilo nitajie jina la mtoto wa rais Magufuli?nitajie kiwanja au kioski cha mtoto wa rais Magufuli?sasa ingawa sio vyote vilivyosemwa juu ya ridhiwani ni kweli ila kuna vipo vya kweli,,sasa ridhiwani kawai fanya wapi kazi?mshaara wake sh ngapi mpaka awe na mali zile?kafanya kwa mda gani?

Ukitaka kuthibisha kwamba sasa hivi tumelamba dume,,ulisikia hotuba ya mzee Mwinyi wakati wa sherehe za Uhuru?nanukuu "miaka 30 tuliyokaa sisi madarakani hatufikii mwaka 1 uliokaa wewe kwa utendaji" lakini pia fatilia hotuba ya Trump wakati anaapishwa,,hana tofauti na anayosema kila siku rais wetu,,

Daima namwombea sana Rais wetu,,Mungu amlinde na kumsimamia azidi kutenda na kutoa haki kwa wanyonge kwani tulinyonywa na kuibiwa sana tena sana haswa hawamu ya 4,,ile ni hawamu ya nyoka na inapaswa kulaaniwa daima.
Kwanza naomba kuweka wazi kuwa mimi ni Engineer na nimeshiriki miradi kadhaa ya ujenzi katika mikoa mbalimbali hapa Tanzania.

Nimejikuta nikitamani sana kwenda kuukagua ujenzi unaoendelea pale UDSM ambao ni (typical lay out) ya flats 20 huku kila flat ikiwa na ghorofa nne. Kwa mantiki ya "typical lay out ina maana kila flat imegharamiwa sawa, hii ni kusema kuwa kila flat imegharamiwa kwa Tshs milioni 500?

Ikumbukwe kuwa TBA ni consultant tu ambaye inamlazimu kutafuta main contractor na huyo main contractor ambaye ni mjenzi pia atafute sub contractors kwenye upande wa plumbing na electrical. TBA amejithibitisha mbele ya rais Magufuli kuwa tender document ya contractor pamoja na subs aliowatafuta haikufika Tshs bilioni 10 kwa flats zote maana na yeye ni lazima kwenye hiyo bilioni 10 apeleke wakaguzi site na vikao vya kila muda kwa mujibu wa taratibu pia ni lazima abaki na akiba kama mfanyakazi anayetakiwa kuendesha ofisi. Any way swala la usafiri limeepukwa kwa kuwa mradi upo kilomita chache tu kutoka zilipo ofisi za TBA.

Sasa kweli kila flat imegharimu Tshs milioni 500 kwa kila kitu? Building structure + plumbing + electrical installations? Ubora wa jengo?

Kwenye mambo ya ujenzi kama haya huwa kuna kitu tunaita "additional works" yaani kutokana na mabadiliko ya bei za vifaa, kukosea kwenye quotation, kuongezeka vitu vya ziada inamlazimu mkandarasi kuandika "claim" ya kuomba fedha zaidi kutokana na hilo.

Pengine huu mradi wa Tshs milioni 500 kwa kila flat una "claims" kibao za additional works ila tutakuja kuambiwa kuwa zimetumika tu Tshs milioni 500 kwa kila flat. Nani atakagua? Mchakato wa ujenzi na taratibu zilifuatwa?

Hata ukinichinja nipo tayari kuliko kuamini kuwa pale UDSM flat moja ya ghorofa nne imegharimu Tshs milioni 500 hadi kukamilika!

Wakuu, naahidi kuwa hii thread nitai-update baada ya kutembelea ujenzi wa UDSM hapo jumanne wiki ijayo. Naahidi kuwa nitadadavua kila kitu na mwisho tukubaline kuwa kama ni sahihi kudanganywa kuwa kila block imegharimu Tshs 500 milioni mpaka kukamilika. Nitakagua ubora wa jengo na nitaweka humu kila kitu! Mods naomba mnilindie thread yangu.
 
Sasa unatuaminisha nini labda mkuu??? Majungu tu hizi gharama unazopiga usisahau kua Magufuli amekua waziri wa ujenzi kwa miaka kumi (10) he knows what he is doing na pale UDSM kuna civil engineers and others kama electrical wote nafikiri kama kuna makosa either students au wahadhiri wangekua wameshaleta hata uzi na ujenzi unamalizika.

Njoo ukague ukitaka ila watu kama nyie haters will be there unamaanisha wote pale wasomi na Rais ambaye naye amekua waziri for ten years wasielewe wewe na huko unakotoka sijui hata barabara ya mliman unaifahamu uje kukagua na kutupa tathmin.. Shame on you!
 
K

Kila kitu kiko sawa na TBA hawahitaji malipo yoyote kama ofisi wao wapo kazini kama kazi zingine za kila siku.

Wajenzi nchi hii mmewaibia sana watanzania ktk gharama za ujenzi.

Nenda Africa ya Kusini kaangalie gharama za ujenzi wa nyumba ziko chini sana na nyumba ni imara sana MTU anaweza kumiliki bila shida yoyote.

Sasa mtoa mada unafikiria dili tu hakuna kitu kingine.

Flat hazibomoki ziko imara na zitadumu .

Mkuu unacompare ujenzi wa nchi nyingine na ingine,hapo ndio unafeli...

Jaribu ku-compare ujenzi Dar es Salaam na hapo Moshi tu uone gharama zinapopishana kama mbingu na ardhi...

Na pia labour charge hua ni ndogo all the way,tofauti inakuja kwenye materials ndio bei zinabadilika kupita maelezo

Mfano mdogo tu,lori la mchanga mende ya 15m3 Dsm ni 200,000/= wastani...Moshi lori ndogo ya 4m3 tu ni 200,000/= wastani...ili nibebe mchanga wa kunitosha moshi kufikia 15m3 natakiwa Lori 4 zilizojaa za 4m3...

Kwa lugha nyepesi kabisa natakiwa shilingi 800,000/= mjini moshi kupata mchanga 15m3 wakati Dar es Salaam nahitaji 200,000/= tu kupata 15m3 hiyo hiyo...

Lete argument ingine..hii imeisha!
 
Mkuu hiyo nyumba ina vyumba vingapi?
Bedroom tatu na master moja,seating room,jiko,store,korido,choo na bafu na varanda mbili.
Nilifyatua tofari 4500 kwa mfuko mmoja ratio ya tofari 28-30 concrete.
Quantity surveyor aliandika tofari 1@1200 mimi kwa gharama zangu ni 700Tsh.Mchanga alisema trip moja 150K mimi nikapata kwa 45K peke yake,maji alisema trip moja kwa 20K mimi nikapata 5K peke yake.
Wakati wa ujenzi mbao za matumizi nilipasua miti yangu kwa shilingi 3500 kwa ft 7.Kila kitu nilinunua mimi,baba alianza kusimamia mwanzoni nikaona analegeza nilimpiga chini nikawa incharge wa kila kitu mimi japo niko mbali nilifanikiwa
 
Sasa unatuaminisha nini labda mkuu??? Majungu tu hizi gharama unazopiga usisahau kua Magufuli amekua waziri wa ujenzi kwa miaka kumi (10) he knows what he is doing na pale UDSM kuna civil engineers and others kama electrical wote nafikiri kama kuna makosa either students au wahadhiri wangekua wameshaleta hata uzi na ujenzi unamalizika.

Njoo ukague ukitaka ila watu kama nyie haters will be there unamaanisha wote pale wasomi na Rais ambaye naye amekua waziri for ten years wasielewe wewe na huko unakotoka sijui hata barabara ya mliman unaifahamu uje kukagua na kutupa tathmin.. Shame on you!
Na mimi pia nimesoma UDSM kitivo cha Uhandisi
 
Haiwezekani kwa block zile cost iwe 10Billion. Inasemekana Mkurugenzi wa TBA anashindwa kumfuata Mkuu wa kaya maana thamani imefika 26Billion. Professionally ktk project hiyo lazima kulikuwa na provisional item and Prime cost sum kama Electrical, plumbing, etc. Provisional item can be boundary wall, external works etc the procedure there must be a quotation and can be more or less compared to those indicated in the bidding document. There mustbe some variations and remeasurements, TBA wasitudanganye
 
Bedroom tatu na master moja,seating room,jiko,store,korido,choo na bafu na varanda mbili.
Nilifyatua tofari 4500 kwa mfuko mmoja ratio ya tofari 28-30 concrete.
Quantity surveyor aliandika tofari 1@1200 mimi kwa gharama zangu ni 700Tsh.Mchanga alisema trip moja 150K mimi nikapata kwa 45K peke yake,maji alisema trip moja kwa 20K mimi nikapata 5K peke yake.
Wakati wa ujenzi mbao za matumizi nilipasua miti yangu kwa shilingi 3500 kwa ft 7.Kila kitu nilinunua mimi,baba alianza kusimamia mwanzoni nikaona analegeza nilimpiga chini nikawa incharge wa kila kitu mimi japo niko mbali nilifanikiwa
Piga vizuri gjarama mkuu
 
Back
Top Bottom