Ujenzi wa Chuo cha Muhimbili/Mloganzila Dar, wakamilika

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,490
54,884
Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili /Mloganzila - Dar es salaam wakamilika. Mradi huu umegharimu Dola za Kimarekani milioni 61, ambapo Serikali imetoa Dola milioni 18 na Serikali ya Korea imetoa mkopo wa Dola milioni 43.

Kukamilika kwa Ujenzi wa Chuo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili eneo la Mloganzila kutawezesha wanafunzi 15,000 wa udaktari kudahiliwa na kupunguza tatizo la wataalamu wa Afya nchini.
image.jpeg
 
Hoja hapa siyo wingi wa madaktari bali uwezo wao wa kitabibu.Je, chuo hiki kitaondoa kabisa tatizo la wangonjwa wa Tanzania kwenda kutibiwa Nje ya nchi?
 
Chamazi Mbagala Muhimbili wana eneo kubwa lenye takribani ekari 100, waje wajenge hospital ya wagonjwa wa akili au wajenge chuo cha wafamasia
 
kama unatoka kibaha sehemu inaitwa kibamba chama utaona barabara ya rami inakata kulia.fata hyo road mpaka chuoni
 
Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili /Mloganzila - Dar es salaam wakamilika. Mradi huu umegharimu Dola za Kimarekani milioni 61, ambapo Serikali imetoa Dola milioni 18 na Serikali ya Korea imetoa mkopo wa Dola milioni 43.

Kukamilika kwa Ujenzi wa Chuo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili eneo la Mloganzila kutawezesha wanafunzi 15,000 wa udaktari kudahiliwa na kupunguza tatizo la wataalamu wa Afya nchini.
View attachment 320987

Mkuu hiyo picha ni artist impression au live? Jengo lime/litapendeza!
 
Sidhani kama ni kweli. Juzi nilikuwa mitaa ya karibu na huko mloganzila, nikaona zile cranes za mkandarasi bado hazijaondolewa. Hiyo picha siyo real!
 
HIVI KULIKUWA NA HAJA GANI YA KURUDISHA KOZI YA UDAKTARI UDSM WAKATI KUNA MPANGO MZURI NA ENDELEVU KAMA HUU??? BADO NA MUHIMBILI (MUHAS) IKO VIZURI, BADO KUNA UDOM nk

UKITAWANYA SANA RASILIMALI KWA KITU KILE KILE BASI INAPUNGUZA UFANISI.

Queen Esther

Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili /Mloganzila - Dar es salaam wakamilika. Mradi huu umegharimu Dola za Kimarekani milioni 61, ambapo Serikali imetoa Dola milioni 18 na Serikali ya Korea imetoa mkopo wa Dola milioni 43.

Kukamilika kwa Ujenzi wa Chuo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili eneo la Mloganzila kutawezesha wanafunzi 15,000 wa udaktari kudahiliwa na kupunguza tatizo la wataalamu wa Afya nchini.
View attachment 320987
 
hilo sio jenga bali ni michoro ya jengo la mgonzila ambalo wasouth korea watatoa pesa iwapo CCM itabadilika na kufuata demokrasia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom