MTENDAHAKI
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,013
- 1,443
Nimepata fursa ya kuandika haya Muda huu!
Nimekusikia Mh. JPM ukitangaza nia ya kujenga bwawa hilo kubwa la umeme. Kwakweli hilo ni jambo jema sana, na kwa namna ninavyokufahamu ukishatamka jambo kinachofata ni utekelezaji! Nataka nikuhakikishie kwamba wahandisi wa kitanzania hawajashindwa kusanifu na kujenga bwawa hilo!Kilichokosekana ni nia ya dhati ya kuwekeza kwenye mradi huo kutoka serikali zilizopita!
Nina hakika katika watumishi wa umma wa kitanzania (wahandisi wa ujenzi (civil), maji na umwagiliaji (hydology and irrigation), umeme (electrical), mitambo(mechanical), mazingira (environment), computer and all other fields including social scientists)! walioko serikalini na sekta binafsi wanaweza kutimiza azma hiyo kwa haraka na muda mfupi wakipewa fursa!
Ni jambo zuri kujifunza kwa waliotangulia (Ethiopia) lakini ni jambo kubwa zaidi watanzania wakifanya maana watatakiwa kufanya na sehemu zingine ambazo zina fursa hii! Faida nyingine ni gharama itakuwa nafuu zaidi wakitumika watanzania na hasa watumishi wa umma (kwa sababu wanalipwa mishahara hivyo wanahitaji uwezeshaji wa kawaida tu) kama ambavyo wamekuwa wakitekeleza miradi mingine mfano barabara, madaraja, mabwawa ya maji na miundombinu mingine!
Kwa namna ulivyo na nia ya dhati, watumishi hawa wa umma hawatakuangusha kamwe. Unapokuja ugeni kutoka Ethiopia tafadhali mawaziri wa Maji, Nishati, Mazingira, kilimo na wengineo wawe wameunda team ya wataalamu wa kuambatana na ugeni huo. Hawa wale kiapo cha utii na uadilifu kama wajumbe wa tume ulizounda na waonyeshe kujiamini na kuwa na uhakika wa kutekeleza hiyo kazi kwa muda mfupi kwa kadri inavyowezekana! Ni lazima wapewe muda maalum wa kukamilisha kazi zote za usanifu wa awali na wa kina ikiwa ni pamoja na kutengeneza michoro yote ya mradi na ujenzi.Ninaamini hii ndiyo namna bora ya kukabili jambo hili!
Bwawa hili sio tu kwamba litasaidia kuzalisha umeme wa kutosha na wa gharama nufuu bali pia litainua sana kilimo cha umwagiliaji (downstream)kwa kutumia maji ambayo yataachiwa kutoka kwenye turbines!Ndio maana ni muhimu sana bwawa likaambata na miundo mbinu ya kupeleka maji mashambani na majumbani mwa watu! Bila shaka kwa pamoja tutafika!
Hapa kazi tu!
Mtendahaki
UPDATES
Nimekuelewa na Tunakushukuru Mr President kwa kuwaamini wataalamu wazalendo. Wahandisi wa kitanzania msituangushe na wataalamu wengine mtakaokuwa kwenye timu mmepewa fursa ya kuonyesha kwamba pakiwa na political will nyie ni bora kama Marekani, UK, Brazil, China etc. Political will imeonyeshwa na Mh. Rais na sisi tukaonyeshe utaalamu wetu kwa kusanifu na kujenga bwawa bora kabisa kwa gharama ndogo kabisa. Naamini mnaweza!Msisite kutafuta ushauri mnapokwama hasa kwa wataalamu wa mabwawa na umeme walioko vyuo vikuu vya Tanzania (UDSM (CoET), SUA(DEST), MUST (IST-DCE), etc). Wasalaam