Ujenzi wa Barabara ya maziwa-External kwa kiwango cha lami waanza @JJMnyika

Mzalendo JR

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,193
515
Tayari taratibu za zabuni zimeshakamilika na mkandarasi anapaswa kuanza ujenzi. Manispaa ya Kinondoni imeshaweka alama ya "X" katika majengo ambayo yatapaswa kubomolewa kuwezesha upanuzi wa barabara husika unaofanywa na Wakala wa Barabara Mkoa wa Dar es salaam (TANROADS).

Tarehe 15 Septemba 2012 nilifanya mkutano wa hadhara Jimboni Ubungo kwenye kata ya Makuburi ambapo pamoja na maswali mengine niliulizwa ni lini ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kutoka Maziwa mpaka External ukiambatana na ujenzi wa daraja katika barabara husika utaanza.

Pamoja na kueleza hatua iliyofikiwa mpaka sasa nilitoa mwito wananchi wote ambayo makazi yao yamewekewa alama ya "X" ikiwa si wavamizi wa barabara wawasilishe kwa Manispaa ya Kinondoni maelezo na vielelezo vyao kwa kuzingatia Wakala wa Barabara Mkoa wa Dar es es salaam (TANROADS) wao wana bajeti ya ujenzi pekee na madai ya fidia kwa wenye uhalali yako chini ya Manispaa ya Kinondoni; tayari 17 Septemba 2012 baadhi ya wananchi wamewasilisha nyaraka zao.

Ikumbukwe pia kuwa kwa kutambua umuhimu wa suala hili nilichukua hatua mbalimbali za kibunge kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2011 ili barabara husika iweze kupandishwa hadhi na kujengwa kwa kiwango cha lami kwa haraka zaidi kwenye mwaka wa fedha 2011/2012 kuliko ilivyopangwa awali.

Niliziandikia mamlaka husika hususan Wizara ya Ujenzi na TANROADS kuzingatia barabara tajwa katika bajeti kwa lengo la kuchangia katika kupunguza msongamano, Wizara ya Ujenzi awali ilisema serikali kuu haiwezi kushughulikia barabara hiyo kwa kuwa iko chini ya Manispaa ya Kinondoni. Lakini, nikaendelea kuchukua hatua zaidi kwa njia za kibunge na za uwakilishi wa wananchi na hatimaye TANROADS ikaingiza barabara hiyo katika vipaumbele vyake na kutenga fedha za ujenzi wa kiwango cha lami kiasi cha shilingi bilioni 1.2.

Aidha, pamoja na kiwango hicho cha fedha kilichotengwa na TANROADS, tarehe 5 Machi 2012 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alieleza kuwa amewasilisha maombi mengine kupitia Mfuko wa Barabara (Road Fund) kwa ajili ya ujenzi wa daraja kubwa zaidi katika barabara hiyo kwenye eneo la Ubungo Kisiwani/External suala ambalo pia kwa nyakati mbalimbali nilihoji utekelezaji wake.

Izingatiwe kwamba tarehe 21 Machi 2012 niliunganisha wananchi kuchangia hatua za dharura za kufanya matengenezo ili kupunguza kero lakini nikasisitza kuwa suluhisho muhimu zaidi ni kupanua daraja la External katika Eneo la Ubungo Kisiwani ili kupunguza msongamano wa magari na kujenga barabara husika kwa kiwango cha lami hatua ambayo sasa inaelekea kuchukuliwa kwa haraka.

John Mnyika (Mb)
18 Septemba, 2012

MIMI: Hiki ndo nilichokua nakitaka Mh. Mbunge, hata hivyo zingatia kuwataarifu wapiga kura wako juu ya yale uliyotuletea humu JF kipindi cha nyuma kidogo. Kwani katika mchango wangu nilisisitiza ujumbe ule na hata huu uwafikie wale wasiojua kusoma wala kuandika, wasiokua na nafasi ya kuperuzi mitandaoni na Bibi na Babu yangu anaeamini hadi leo Nyerere ni raisi wa Jamhuri ya watu wa Tanzania.

HONGERA!
 
Wakazi wa ubungo tumeshasema huyu dogo bungeni atumrudishi kwa kura zetu tena, labda wapange njia zingine.

huwezi kwenda bungeni kutumia lugha za kuudhui na lugha chafu kwa watawala katika kujenga hoja, halafu anaambiwa futa kauli yako uendelee kuchangia ANAGOMA?

wakazi wengi wa Ubungo tumepoteza imani na matumaini na kijana huyu na tunamwambia bungeni tena basi.
 
Kwani ndugu wewe ni nani kuwasemea wana Ubungo wote? Na una uwezo gani kuwashawishi wasimchague Mnyika mwaka 2015 na labda ulichangia vipi kuwashawishi wamchague mwaka 2010? Vinginevyo hiyo ni wishful thinking tu.
 
Wakazi wa ubungo tumeshasema huyu dogo bungeni atumrudishi kwa kura zetu tena, labda wapange njia zingine.

huwezi kwenda bungeni kutumia lugha za kuudhui na lugha chafu kwa watawala katika kujenga hoja, halafu anaambiwa futa kauli yako uendelee kuchangia ANAGOMA?

wakazi wengi wa Ubungo tumepoteza imani na matumaini na kijana huyu na tunamwambia bungeni tena basi.

wewe njegele kweli!, mkiambiwa vichwa mnafugia rasta afu jukumu la kufikiri umelikabidhi kalio mnalalama, who are you by the way to speak on behalf of wana ubungo!!?
 
Vipi hizi za ubungo maziwa zinajengwa kwa msaada wa watu wa ujerumani au Jesuit? manake CDM kila siku mnabeza juhudi za JK katika kuwaletea maendeleo watz.
 
Yeye ni muwakilishi mzuri ndio maana unaona serikali inatekeleza ila kumbukeni kumpa mnyika kura kwa mara ya pili tena. Hebu kumbuka tulipo toka miaka 50 hadi leo bado sehemu hazina barabara we too far frm developing
 
hongera sana Mnyika, hatukuamka saa 11 bure kukupigia kura! Chapa kazi jembe tupo nyuma yako
 
Wakazi wa ubungo tumeshasema huyu dogo bungeni atumrudishi kwa kura zetu tena, labda wapange njia zingine.

huwezi kwenda bungeni kutumia lugha za kuudhui na lugha chafu kwa watawala katika kujenga hoja, halafu anaambiwa futa kauli yako uendelee kuchangia ANAGOMA?

wakazi wengi wa Ubungo tumepoteza imani na matumaini na kijana huyu na tunamwambia bungeni tena basi.

umetuma comment hii uku ukiwa umepakatwa na mmoja kati ya watawala uliowataja hapo juu.
 
JK sidhani hata anajua kuwa kuna hiyo barabara...mi nadhani tumpongeze JJ Mnyika kwa kushupalia hili suala,pili tusimsahau Magufuli kwa juhudi zake binafsi kama Mtanzania kuguswa moja kwa moja na ubovu wa barabara.
 
Wakazi wa ubungo tumeshasema huyu dogo bungeni atumrudishi kwa kura zetu tena, labda wapange njia zingine.

huwezi kwenda bungeni kutumia lugha za kuudhui na lugha chafu kwa watawala katika kujenga hoja, halafu anaambiwa futa kauli yako uendelee kuchangia ANAGOMA?

wakazi wengi wa Ubungo tumepoteza imani na matumaini na kijana huyu na tunamwambia bungeni tena basi.

Kauli ya DHAIFU ndo inakusumbua au sio? Ila hata yy Mkuu anajua ni dhaifu ss sjui ww kama nani unawasemea wananchi wa Ubungo?
 
Back
Top Bottom