UJENZI WA BARABARA KILOMBERO MKANDARASI ANAIDAI SERIKALI?
Mheshimiwa Rais, wilayani Kilombero, mkoani Morogoro, miradi mingi ya kimaendeleo ambayo inatumia fedha za umma haikamiliki kwa wakati. Iko mingi sana lakini kilio hasa ni huu mradi wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami, ya urefu wa kilomita 66.9 tu, Kidatu-Ifakara.
Tangu tarehe 04/05/2018 aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli, aweke jiwe la msingi(azindue ujenzi) huku serikali ikisema ingekamilika mwaka 2020 ajabu hadi leo 2022 mkandarasi bado yuko kujenga tu! Mkwamo uko wapi?
Ujenzi wa hii barabara hadi kukamilika kwake itagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 104.914 ambazo ni ufadhili wa Umoja wa Ulaya(EU) iliyotoa asilimia 49.15 ya gharama ya ujenzi huu, Uingereza(UK) 40.13%, USAID 10.72%, na gharama iliyobaki italipwa na serikali ya Tanzania.
Hii barabara ni ya muhimu katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika ukanda wa Kilombero na Ulanga. Ili mtu afike halmashauri ya wilaya ya Malinyi, halmashauri ya wilaya ya Ulanga, na halmashauri ya Mlimba kutoka Morogoro mjini ni lazima apitie barabara hii hadi mjini Ifakara.
Ujenzi umeanza 04/05/2018, leo 2022, mkandarasi bado yuko site tu kujenga! Mheshimiwa Rais, ama mlio karibu na mamlaka ya urais, lifanyieni kazi hili. Mwendo wa kinyonga wa mkandarasi katika kukamilisha huu mradi unatokana na nini?