SoC01 Ujenzi wa barabara uzingatie kiwango cha lami kilichowekwa

Stories of Change - 2021 Competition

ItsMi

Member
Sep 13, 2021
66
31
Habari ya kwako Mdau,
Kwa siku nyingi sasa kumekuwa na changamoto ya barabara hasa katika maeneo ya mikoani ambapo barabara nyingi za lami zimekuwa zikifumuliwa mara kwa mara. Yaani kila baada ya miezi kwa kuharibika mapema kwa sababu zimejengwa chini ya kiwango cha lami.

Hii imekuwa kero kubwa kwa watumiaji wa barabara. Kwa sababu barabara hizo ndizo zimekuwa zikichochea uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa kutoka shambani na kwenda viwandani kuchakatwa na hatimaye kuelekea kwenye masoko.

Hivyo tunaiomba serikali iweke kiwango stahiki cha lami na iweke usimamizi madhubuti licha ya uwepo wa makandarasi, serikali yenyewe pia inalo jukumu la kusimamia miradi hii kwa ukaribu kwa kuwa fimbo ya mbali haiui nyoka.

Hivyo kwa kufanya hivyo itaondoa kero za kubomoa barabara kila mwaka hii itasaidia kuimarisha sekta za usafirishaji na kuinua uchumi wenye kuleta maendeleo kwa jamii.

Asante kwa kufuatilia makala hii.
 
Back
Top Bottom