Ujenzi/upanuzi wa njia nane Kimara-Kibaha una walakini

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,529
NENO LA HAKIBA: Nitahukumiwa kwa nitakachokiandika ujenzi ukikamilika....

Kuna tofauti kubwa kati ya
Kujenga
Kukarabati
Kufanya upanuzi
Japo yote haya katika ujumla wake ni ujenzi.... Kujenga na kujenga upya pia kuna tofauti...ukijenga nyumba na baada ya muda ukaibomoa ili ujenge tena huku kunaitwa kujenga upya.... Kuongeza baadhi ya vyumba kwenye nyumba uliyokwisha jenga kunaitwa kufanya upanuzi.... Kurudia kufanya finishing kwenye nyumba na kurekebisha baadhi ya maeneo kunaitwa kufanya ukarabati..... Hata kwenye ujenzi wa barabara kuna kujenga, kujenga upya, kukarabati na kufanya upanuzi
Tuna barabara nyingi nchini nyingine ziko kwenye hatua ya ujenzi, nyingine ukarabati nyingine upanuzi... Bila kujali ni hatua ipi kuna baadhi zimeshakamilika na zinatumika sasa....
Barabara ya Sam Nujoma - Mwenge Ubungo ilijengwa upya.... Barabara ya Morogoro, Ferry mpaka Kimara mwisho ilijengwa upya.... Barabara ya Moroko Mwenge ilipanuliwa....
Kinachoendelea Morogoro Rd... Eneo la kimara mpaka Kibaha stand mpya sio kujenga upya bali ni upanuzi wa kuongeza barabara zaidi kushoto na kulia.... Sio ujenzi mpya... Ni kama ile ya Moroco Mwenge... Barabara ya zamani inabaki haiguswi kabisa, bali inakarabatiwa baadhi ya maeneo
Sehemu pekee ambayo ujenzi mpya unafanyika ni eneo la Mbezi, pale kuna mzunguko wa barabara nyingi unasukwa.... Kwingine kote ni ukarabati na upanuzi na hili ni mpaka kwenye madaraja yote eneo lote la ujenzi
Kitu cha pili ni original plan ya njia 8, nne kila upande na matoleo na flyover za kutosha... Lakini kinachoendelea sasa ni ujenzi wa njia mbili kila upande hivyo ukijumlisha na mbili za sasa jumla zinakuwa sita..... Sasa nane zinatoka wapi? Kwa mtazamo wangu mbili za mwisho, ya sita na saba ni zile service road za vumbi, moja kila upande... Kwa hesabu hizi njia nane zitakamilika.... Ila zenye lami ukiacha mzunguko wa Mbezi zitakuwa mbili kila upande! hizi ndio ujenzi mpya kabisa... Nyingine mbili ni hii ya zamani... Zikarabatiwa tu! Hazijengwi upya!!! Pamoja na madaraja...
Nitahukumiwa kwa hii mada lakini kwa kinachoendelea sasa huu ndio uhalisia wa hicho kinachoitwa njia 8.... Usije kudhani ni nne za lami kila upande.. Kama ile ya Kuala lumpa airport au J'burg to Durban... na nyingine nyingi duniani
Nahitimisha hii mada kwa kujaribu kuangalia weledi, ujuzi, umahiri, ukubwa na uwezo wa kampuni inayofanya ujenzi husika... Haikushindanishwa kwenye tenda ya wazi... Haiwezi kushindana na kampuni kama strabag na nyinginezo... Kazi yake ya ujenzi wa barabara inayojulikana ni ile ya Msata Bagamoyo... Barabara ile ina mapungufu mengi.... Sasa kampuni hii hii ndio inajenga highway ya barabara 8.... Wakati utasema....
Tumeziona flyovers za Ubungo na Tazara... Picha tukizooneshwa mwanzoni na kilichokuja kujengwa hakuna mfanano kabisa..... Nahofia kitu kilekile kinajirudia kwenye ujenzi wa barabara ya njia 8 Kimara Kibaha
Nitahukumiwa kwa mada hii ujenzi/upanuzi ukikamilika.... Lakini kwa sasa picha imeshaanza kujichora!!!!

Jr
 
Ni neno la HAKIBA

Jr

OK sijawahi kulisikia!

Hapo ukiulizwa profession yako nina uhakika kwa 100% haina uhusiano wowote ule na uhandisi wa barabara lkn kama kawaida ya Wabongo kujifanya kujua kila kitu na wazungumzaji wa mambo hata msioyaelewa, nakumbuka mwendokasi ilikuwa hivyo hivyo wataalamu kibao leo hii ndo wa kwanza kuyapanda mabasi, jifunzeni kuongelea mambo ambayo mna ujuzi nayo kwa msioyafahamu kaeni kimya, hiyo inaitwa busara!
 
Mshana Jr wanaposema njia nane maana yake ni hii;
Wanaongeza njia tatu kila upande. Yaani kulia na kushoto kwa barabara iliyopo sasa, barabara ya hivi sasa itaendelea kubaki na itatymika kwa ajili ya mabasi ya mwendo kasi. Hivyo basi, ukichukua hizo tatu za kushoto na tatu za kulia unapata sita, ukiongeza na mbili za meendokasi zinakuwa nane.
kama utajumuisha service road zile za vumbi maana yake zitakua barabara kumi.

Nimeambatanisha ramani kwa uelewa zaidi.
IMG_20181219_111733.jpg
 
Sas a ujenzi wa bongo ni wa hovyo sasa pale mfugale walijenga nin si wangeacha kuna flyover ya vile jmn..!!?


Shida yako unataka muonekano kuliko umuhimu, Mfugale imepunguza foleni sana, uliza watu Pugu na maeneo ya huko wanaoutumua hiyo barabara watakwambia.

Hivyo usichanganye mambo, kama ulitaka uone barabara za juu za maghorofa kubwa kama Tokyo ili roho yako ifurahi kuziangalia na kupiga picha pole sana, hilo halikuwa lengo Serikali yetu, lengo lilkuwa ni kupunguza foleni, na foleni zimepungua!
 
Back
Top Bottom